Naomba mnipe ushuuda mlio wahi kutumia mbolea za kisasa kama kweli zina ua ardhi

Mudugu

Senior Member
Mar 17, 2018
129
225
Mimi nimkulima wa kawaida nataka nianze kutumia mbolea za madukani lakini kabla sijaanza kutumia nimeona si vyema kuacha kuwashrikisha wana jf maana humu kuna watalamu na wazoefu wa masuala ya kilimo
Nimekuwa nikisikia kuwa eti mbolea za kisasa zina ua aridhi je nikweli?
Maana shamba langu linaukubwa wa hekari moja nikilima mahindi linatoa magunia mawili kwakuwa halina rutuba
Nikitumia mbolea najua kipato kitaongezeka sasa swali lina kuja je nikija kuacha kutumia mbolea mavuno yataporomoka kwa kasi kwakuwa ardhi imekufa
Nahisi hata gunia mbili nisizipate
Naomba ushauri kutoka kwenu mulio wahi kutumia hizo mbolea na mumeona matokeo gani kuhusu ardhi nikweli inakufa au ni imani potofu tu
 
dolomon

JF-Expert Member
Jun 5, 2018
589
1,000
Kwanza nianze kwa kukupa pole na pongezi vyote kwa Pamoja, pole kwa maana ya hasara uliyokuwa ulipata kwa kuvuna chini ya kiwango, na pongezi ni kwa vile sasa umeamua kuanza kuchukua hatua.

Ni Ukweli usiopingika kuwa kadri shamba linavyozidi kutumika kwa shughuli za Kilimo ndivyo rutuba yake huzidi kupungua. Sasa usitarajie kuwa ipo siku rutuba itaongezeka kama hauna tabia ya kuulisha udongo ili pia ukulishe.

Dhana ya shamba kuharibiwa na matumizi ya mbolea ya viwandani ni ya kweli endapo utatumia mbolea kinyume na maelekezo na si ya kweli kama ukitumia kulingana na maelekezo ya wataalamu wa Kilimo.

Wataalamu wanashauri kuwa kabla ya kuanza kutumika mbolea shambani, ni vyema kufanya kitu kinaitwa 'Soil Analysis ', hiyo itakukuonesha Ni aina gani ya viinilishe vimepungua au havipo kabisa katika udongo wako. Baada ya hapo ndio utashauriwa sasa aina na kiwango gani cha mbolea cha kuweka kwa Kila mmea.

Kwa uzoefu sasa na kwa kutumia jedwali la utafiti wa udongo walilofanya wataalamu chuo cha utafiti wa Rutuba ya Udongo Mlingano, mashamba mengi yana upungufu wa kiinilishe cha Nitrogen ambacho ni muhimu sana kwa kutengeneza chanikiwiti ya mmea, hivyo sasa mbolea ya UREA, SA,DAP na CAN, zinaweza kutumika. Lakini pia ni vyema kujua 'CHACHU', ya udongo wako kwa kufanya kitu inaitwa 'Soil pH test' ili utambue ni mbolea ipi itumike.

Nadhani umeambulia hata japo kidogo cha kuanzia,na wenzangu watajazia palipo pelea. Asante sana.
 
sirmweli

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
1,440
1,500
Mbolea za asili zinatoa virutubisho vichache kwa mda mrefu mfano mbolea ya kuku inaupatia mmea virutubisho kwa kwa haraka sana tofauti na mbolea ya ngo'mbe ndo maana wakulima wa mbogamboga wanapendelea sana mbolea ya kuku.

Lakini mbolea nyingi za kisasa huupatia mmea virutubisho mmea kwa haraka sana hivyo unatakiwa uiweke kila unapopanda mimea yako.Mimi siamini kama zinaua ardhi

Pia angalia YouTube au Google utapata maelezo mazuri zaidi kuhusu mbolea.
 
Asante sana mkuu kwakunipa elimu natumaini umesaidia na wengine ubarikiwe sana
 
Mudugu

Senior Member
Mar 17, 2018
129
225
Mbolea za asili zinatoa virutubisho vichache kwa mda mrefu mfano mbolea ya kuku inaupatia mmea virutubisho kwa kwa haraka sana tofauti na mbolea ya ngo'mbe ndo maana wakulima wa mbogamboga wanapendelea sana mbolea ya kuku.

Lakini mbolea nyingi za kisasa huupatia mmea virutubisho mmea kwa haraka sana hivyo unatakiwa uiweke kila unapopanda mimea yako.Mimi siamini kama zinaua ardhi

Pia angalia YouTube au Google utapata maelezo mazuri zaidi kuhusu mbolea.
Asante sana sirmweli
 
sirmweli

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
1,440
1,500
Mimi nimkulima wa kawaida nataka nianze kutumia mbolea za madukani lakini kabla sijaanza kutumia nimeona si vyema kuacha kuwashrikisha wana jf maana humu kuna watalamu na wazoefu wa masuala ya kilimo
Nimekuwa nikisikia kuwa eti mbolea za kisasa zina ua aridhi je nikweli?
Maana shamba langu linaukubwa wa hekari moja nikilima mahindi linatoa magunia mawili kwakuwa halina rutuba
Nikitumia mbolea najua kipato kitaongezeka sasa swali lina kuja je nikija kuacha kutumia mbolea mavuno yataporomoka kwa kasi kwakuwa ardhi imekufa
Nahisi hata gunia mbili nisizipate
Naomba ushauri kutoka kwenu mulio wahi kutumia hizo mbolea na mumeona matokeo gani kuhusu ardhi nikweli inakufa au ni imani potofu tu
Pia wauzaji wa mbolea wengi wanauelewa wa matumizi sahihi ya mbolea hivyo basi umwambie kuwa unataka kulima zao gani yeye atakushauri utumie mbole IPI kwa matokeo bora.

Usije ukaweka mbolea ya kiwandani kwenye mmea mchana. Uweke kwenye 11 jioni.
 
UNIVERSE

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
555
500
Wengi wamechangia vizuri hapo juu. Labda tu kwa kuongezea, hio ardhi yako tayari inaonekana imeshachoka Sana. Mbolea za viwandani sidhani kama zinatatizo endapo zitatumiwa kulingana na maelezo ya wataalamu, hivyo ni muhimu sana kutumia ili kuongeza kipato.
Jambo la msingi ambalo kwa uzoefu wangu nimeliona ni kwamba ardhi ikiwa imechoka sana basi hata mbolea za viwandani zinaweza zisilete matokeo yanayoridhisha labda iwekwe nyingi sana kwa vipindi tofauti. Hivyo ni vizuri ukamwaga samadi na kuchanganya vizuri na udongo huku ukiisindikiza na mbolea za viwandani. Samadi ina umuhimu mkubwa kwa sababu inaboresha muundo wa udongo ili kutunza virutubisho na uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu.
 
spodo

Member
Feb 22, 2009
90
125
Kwa kuongezea zaidi kwa yaliyosemwa ni kweli mbolea za viwandani zinaharibu udongo na kwa aina mbili. Kwanza mbolea za viwandani zinashusha pH ya udongo, yani inaongeza acidity Kama vile mbolea ya SA. Pia mbolea ya kiwandani inapowekwa kwny udongo mabaki ya mbolea ya nayobakia baada ya kudissolve kwenye soil solution yanaaffect soil microorganisms activities na ndio maana watu wanakwambia ukitumia mbolea za viwandani kwa muda mrefu zinachosha udongo. Ili mmea uote na uzae mavuno unahitaji chakula ambavyo ni virutubisho vinavopatikana kwenye udongo. Lakini sio kila udongo unavirutubisho vya kutosheleza ili mmea ukue na kuleta mavuno maturity. Hapo Sasa dhana ya kuweka mbolea za viwandani ilikuja ili kutoa virutubisho vinavyohitajika na mmea Lakini kwenye udongo vipo kidogo au hamna kabisa. Sifa ya mbolea ya kiwandani ni Ina dissolve kwenye maji kwahiyo ikiwekwa kwenye udongo virutubisho vinapatikana kwa haraka na urahisi kwa mmea lkn madhara yake ni Kama nilivyoeleza hapo juu.
Ila sifa ya mbolea za wanyama na mimea zinachukua muda mrefu kuoza na kumeng'enywa ili virutubisho vipatikane na mmea.
Kwahyo in short plan tumia mbolea za viwandani ili uweze kuvuna mazao yako vizuri Ila in long term plan lazima uaze kuweka mbolea za wanyama kwenye Eneo lako. Na mbolea za wanyama zinafanya ardhi yako ilirudi kuwa kwenye rutuba vizuri ingawa itakuchukuwa muda kutegemea hali halisi ya eneo lako. Na Kama Eneo lako litakuwa na acidity sana itakubidi utumie chokaa ya kilimo kupindisha pH kwenye slightly acidity or neutral
 
spodo

Member
Feb 22, 2009
90
125
Kwa ushauri wangu kutokana na uzoefu wangu wa hii kazi cha kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kupima udongo wa shamba lako. Maabara ziko zinzofanya hiyo kazi. Kwa huku nyanda za juu kusini sisi ndio tunaopima udongo hapa mbeya, Uyole kituo cha utafiti kilimo ambacho ni cha serikali chini ya wizara ya kilimo. Kwa morogoro nenda SUA na kingine ni mlingano, Tanga. Ukifanya soil analysis majibu yako unayapeleka kwa soil scientist akufanyie interpretation za soil analysis results. Na kwa sehemu hizo zote nilizokutajia wanazopima kuna soil scientists. Interpretation itakuambia shida ni Nini na ufanye nini ilikurudisha shamba lako like lenye rutuba pia utumie mbolea gani na kwa kiasi gani Hizi za viwandani ili upate mavuno ya kutosha. Pia utumie kiasi gani cha mbolea za wanyama na chokaa kiasi gani Kama kuna acidity nyingi ili shamba lako liwe lenye rutuba.
Ushauri kwa wadau Ambao wapo kwenye kilimo au wanataka kuingia kwenye kilimo. Usiingie shambani kulima bila kupima udongo wako. Tusifanye kilimo cha mazoea. Huwezi kufanya kilimo cha kuotea kila siku utegemee mafanikio. Dhumuni la kuwa Hizi mbolea hasa za viwandani ili kuweza kuweka au kuongeza virutubisho ambavyo vimepungua au hamna kabisa kwenye udongo. Swali utajuaje virutubisho vilivyopungua au havipo kabisa bila ya kufanya soil analysis?

Asante,
 
mbwewe

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
3,019
2,000
Laiti hao wataalamu tukiwatumia ipasavyo na tukapata soko la uhakika la mazao yetu na uhakika tutaumaliza kbsa umaskini
Kwa ushauri wangu kutokana na uzoefu wangu wa hii kazi cha kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kupima udongo wa shamba lako. Maabara ziko zinzofanya hiyo kazi. Kwa huku nyanda za juu kusini sisi ndio tunaopima udongo hapa mbeya, Uyole kituo cha utafiti kilimo ambacho ni cha serikali chini ya wizara ya kilimo. Kwa morogoro nenda SUA na kingine ni mlingano, Tanga. Ukifanya soil analysis majibu yako unayapeleka kwa soil scientist akufanyie interpretation za soil analysis results. Na kwa sehemu hizo zote nilizokutajia wanazopima kuna soil scientists. Interpretation itakuambia shida ni Nini na ufanye nini ilikurudisha shamba lako like lenye rutuba pia utumie mbolea gani na kwa kiasi gani Hizi za viwandani ili upate mavuno ya kutosha. Pia utumie kiasi gani cha mbolea za wanyama na chokaa kiasi gani Kama kuna acidity nyingi ili shamba lako liwe lenye rutuba.
Ushauri kwa wadau Ambao wapo kwenye kilimo au wanataka kuingia kwenye kilimo. Usiingie shambani kulima bila kupima udongo wako. Tusifanye kilimo cha mazoea. Huwezi kufanya kilimo cha kuotea kila siku utegemee mafanikio. Dhumuni la kuwa Hizi mbolea hasa za viwandani ili kuweza kuweka au kuongeza virutubisho ambavyo vimepungua au hamna kabisa kwenye udongo. Swali utajuaje virutubisho vilivyopungua au havipo kabisa bila ya kufanya soil analysis?

Asante,
 
PUNJE

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
354
250
Ndugu Madugu; tafuta muda fuatilia Historia ya Ismani. Unaweza kupata mwanga kidogo kuhusu madhara ya aina hiyo ya mbolea. Kwa ufupi tu ni kuwa, udongo unatakiwa uwezeshwe kujirutubisha kiasili. Kama ilivyo kwa viumbe vyote duniani. Kwani udongo nao unaishi; na ni Hai.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom