Naomba mniombee mchumba wangu tumefikia kutoa mahari na kuvalishan pete kanikataa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Pole
najua ulitaka kujuiuliza didy anavuta wa pili nini hapana airuhusu
kuna mtu katupigia jana kwenye maombi akiomba tumsaidie jamani na hilo tatizo
hapo juu ..najua ni gumu kulikubali lakini nikaona niwashirikishe wapendwa
tumsaidiaje na jua mawazo yaakao yatasaidia wengi waliokumbwa na tatizo hili
na watakaoukumbwa na tatizo kujua jinsi gani ya kukabiliana nalo...mawazo yako tutayaheshimu
binafsi nisingependa kutoa yaliomo moyoni naitaji kupata mawazo tofauti hili tatizo naona sasa
limekuwa linaongezeka kila siku

unahisi ni yeye pekee hata wewe ambae ujaoa ama kuolewa yaweza kukutokea ati sikuombei baya
ila ukisoma hapa utajua kumbe hata likitokea ni mapenzi ya mungu hujui kama alikuwa si wako
unataka kulazimisha
 
Acha ujinga changamka tafuta mwingine,mabinti wa JF wako kibao hawana wachumba,anza humu humu...
ala!! Kalagha baho..
 
Pdidy mawazo ya Mungu si mawazo ya wanadamu na njia za mungu si kama njia za wanadamu.Pia ikumbukwe kwamba japo kuwa ishmaeli alikuwa ni mtoto wa Ibrahimu lakin Mungu hakumpa mibaraka aliyompa Isaka na hata akadiriki kujiita Mungu wa abraham isaka na yakobo, sasa mwambie huyu binti amshukuru sana Mungu wala asiombe kukemea mapepo wala nini bali amshukuru tu Mungu kutoka moyoni na atoe sadaka ya kukataliwa na mchumba mbele za Mungu. halafu atulie amwone Mungu atakavyo fanya.
 
Last edited by a moderator:
Mshukuru Mungu kwa kilajambo,mhoji vzuri kaachini tulia,halaf kama msimamo ni huo wala usilazimishe ndoa,na pia mshukuru kwa kuwa amekukataa nje yandoa,ni heri kuliko angekutenda ndani ya ndoa,ubarikiwe.
 
Pole sana na Mungu amekubariki kwani aliyokutendea mchumba wako ni zawadi kwako kama kadhamiria msimamo wake wa kukuacha, Kamshukuru Mungu kwani Maisha ya sasa ni ya Tamaa na yasiyompendeza Mungu, natumaini amekuandalia mwingine mtakaye saidiana katika maisha.
 
Pdidy mawazo ya Mungu si mawazo ya wanadamu na njia za mungu si kama njia za wanadamu.Pia ikumbukwe kwamba japo kuwa ishmaeli alikuwa ni mtoto wa Ibrahimu lakin Mungu hakumpa mibaraka aliyompa Isaka na hata akadiriki kujiita Mungu wa abraham isaka na yakobo, sasa mwambie huyu binti amshukuru sana Mungu wala asiombe kukemea mapepo wala nini bali amshukuru tu Mungu kutoka moyoni na atoe sadaka ya kukataliwa na mchumba mbele za Mungu. halafu atulie amwone Mungu atakavyo fanya.

Honestly haya mambo yanatuchanganya sana..........naongeza miaka 3 ndipo nioe
 
Honestly haya mambo yanatuchanganya sana..........naongeza miaka 3 ndipo nioe

ahaa platozoom mbona unasahau kwamba bado hapo utakua unaahirisha tatizo tu? ni sawa na kusema leo japo ni zamu ya kufua sifui adi kesho kwasababu nahofia mvua na kusahau kwamba kesho hujui kama itanyesha ama haitanyesha.

swala hapa siyo kuahirisha tatizo ila nikulikabili and that is what we call manship.
 
Last edited by a moderator:
ahaa platozoom mbona unasahau kwamba bado hapo utakua unaahirisha tatizo tu? ni sawa na kusema leo japo ni zamu ya kufua sifui adi kesho kwasababu nahofia mvua na kusahau kwamba kesho hujui kama itanyesha ama haitanyesha. swala hapa siyo kuahirisha tatizo ila nikulikabili and that is what we call manship.

Hiyo miaka mitatu ni ya kuongeza ujuzi zaidi na kuandaa mwili na roho
 
tena ye si ashukuru kamuacha kuvisha pete? mwaka hu nafikiri march nilimpigia simu rafiki yangu mwanza akaniambia yuko k
wenye kikao cha wanakamati ya harusi wanarudisha pesa za wachngiaji coz bwana harusi mtarajiwa kamkataa binti tena binti ni boss mwenye nafasi nyeti serikalini.imagine what the hell we live.
 
Mh tafuta mwingine tuu ila kabla hujafanya hivyo jiangalie wewe mwenyewe kwanza .
Ndoa haina majaribio au rehearsal. mdada atakuwa ameona kuna vitu hawezi kuishi navyo maisha yake yote kwako.

Jiangalie kwanza ukiona uko sawa then tafuta mwingine. Ndoa hailazimishwi mkuu
 
pole sana, majaribu ni mtaji, tulia mshukuru mungu naamin hakuwa wako, usikate tamaa.
 
Mwanamke akikukataa si unaachana nae,kwani ana nini cha kukufanya mpaka umuombe Mungu "a-intavini" hapo?Aaaaarrrgggghhhh!
 
Mwanamke akikukataa si unaachana nae,kwani ana nini cha kukufanya mpaka umuombe Mungu "a-intavini" hapo?Aaaaarrrgggghhhh!

tena mnaosemaga hivi ndo wale mkikataliwa mnakunywa sumu kabisa bora hata huyu amemkumbuka Mungu:flypig:
 
Pole
najua ulitaka kujuiuliza didy anavuta wa pili nini hapana airuhusu
kuna mtu katupigia jana kwenye maombi akiomba tumsaidie jamani na hilo tatizo
hapo juu ..najua ni gumu kulikubali lakini nikaona niwashirikishe wapendwa
tumsaidiaje na jua mawazo yaakao yatasaidia wengi waliokumbwa na tatizo hili
na watakaoukumbwa na tatizo kujua jinsi gani ya kukabiliana nalo...mawazo yako tutayaheshimu
binafsi nisingependa kutoa yaliomo moyoni naitaji kupata mawazo tofauti hili tatizo naona sasa
limekuwa linaongezeka kila siku

unahisi ni yeye pekee hata wewe ambae ujaoa ama kuolewa yaweza kukutokea ati sikuombei baya
ila ukisoma hapa utajua kumbe hata likitokea ni mapenzi ya mungu hujui kama alikuwa si wako
unataka kulazimisha

Mi nafikiri ni jambo la kumshukuru Mungu kama amekukataa mapema kabla ya ndoa. Inawezekana huyo angekuja kuwa msumbufu na kukufanya uione ndoa chungu na maisha hayana maana.

Cha msingi usimlazimishe atakuja kukutesa baadaye, badala yake pambana na moyo wako ukubali kuwa huyo si wako tena na urudi taratibu nyuma na kuanza pilika za kutafuta mwingine ili Mungu akupe yule ambaye hata kukataa tena!

Pole.
 
Back
Top Bottom