Naomba mnijibu swali langu jamani ni la jiografia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mnijibu swali langu jamani ni la jiografia

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ndume, Jan 15, 2011.

 1. n

  ndume Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa kawaida kuna mwaka mkubwa na mdogo,ikiwa mkubwa una siku 366 na mdogo una siku 365 na robo.Ikiwa mwaka mpya unaanza tar 1/1 kila mwaka saa 6:00 usiku na unaisha saa 5:59 usiku tar 31/12 kila mwaka.Utata upo hapa kwenye mwaka mdogo ambao una siku 365 na robo. Je,ni kwa nini kuna robo na wakati siku ina masaa 24 na nikipiga mahesabu kwa mimi sioni robo.Je hiyo robo imepatikana vipi jamani wasomi,naombeni majibu nisaidike jamani.
   
 2. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  hiyo robo huwa inafidiwa kwa kuweka mwaka wenye siku 366 ambapo hutokea mara moja kila baada ya miaka minne na hiyo tarehe si nyingine bali ni tarehe 29 ya mwezi wa february ambayo hujitokeza mara moja kila baada ya miaka 4 kufidia hilo pengo.
   
 3. n

  ndume Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  sawa nimekupata utata upo hapa mwaka mkubwa mwezi wa pili unakuwa na siku 29 na mdogo unakuwa na siku 28 tunaona kuna tofauti ya siku moja na siyo robo sasa naomba unifahamishe hiyo robo inafidiwa vipi mpaka mwaka mdogo uwe na robo ndani yake,maana robo ni masaa 6 sasa yamepatikana vipi.
   
 4. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  tafuta kwenye google au wikipedia. pia soma kuhusu international date line
   
 5. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kinachofanyika ni makadirio; Dunia inakamilisha mzunguko wa kulizunguka jua kila baada ya siku 365 na robo. Ikaonekana kuwa italeta usumbufu kuhesabu hiyo robo. Ikaamuliwa hizo robo siku zikusanywe ili kufanya siku moja nzima, hivyo kusababisha kuwepo kwa mwaka mfupi wenye siku 365 na mwaka mrefu wenye siku 366 unaotokea kwa kila miaka minne.
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni maelezo mazuri. Kwa maneno mengine kama alivyosema mmulizaji kuwa robo ni saa 6, kwa hiyo dunia hukamilisha mzunguko wa kulizungua jua kila baada ya saa 8766, ambazo kama utazigawa kwa 24 utapata siku 365.25. Hapa robo ni hii .25 ambayo inakuwa usumbufu kuiingiza kwenye hesabu ya mwaka; kwa hivyo huwekwa kila baada ya miaka 4.
   
 7. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  ndio maana mwaka mrefu hutokea mara moja kila baada ya miaka 4 ili kufidia hayo masaa 6
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mi napanua swali lako kwa nn kuna mwaka mrefu na mfupi
  nimesahu jiographia kidogo lakini tofauti inatokana na kuzingatia issue nyingi kama

  • mzunguko wa dunia kwenye jua
  • kuna mambo ya mwezi
  • na ujue dunia sio perfect sphere na ime tilt kwenye mhimili wake
  kutokaa na sababu hizoo jibu jepesi hiyo roboau mwaka mrefu na mfupi iliwekwa kufidia diff za iliyopo isilete matatizo katika majira ya mwaka.

  la sivyo baada ya miaka kadhaa tungekuta masika tanzania inakuwa september na kingaz kinakuwa december au january.

  But hili jibu nimetoa bila kudesa naweza kuwa niko very wrong. ngoja ni google

  Aksante kwa swali zuri. lakini swali kwako pia umepiga mahesabu gani hayo utuonyeshe .

  haya majibu ya wataalam kutoka google http://www.timeanddate.com/date/leapyear.html
   
 9. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ni swali zuri zuri na lilojaa majibu ya kina....asanteni kwa elimu hii
   
Loading...