Naomba mjadala wa wazi na Zitto kuhusu usaliti ndani ya chama

Status
Not open for further replies.

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
Kuna Mijadala Mingi inaendelea, ya wazi na isiyo ya Wazi. Mingine inaumiza, mingine ya Kipropaganda, mingine ya kuchafuana, mingine ya watu wasiojua nini kinaendelea, mingine inafadhiliwa.

Ninaomba kwa sasa kama kweli Zitto sio msaliti, Mimi ambaye namheshimu sana kama Kiongozi katika Chama changu, ambaye muda mwingi nilimpa fursa ya kuja St. Augustine University kama Kiongozi kuja kuhutubia, tumempa heshima, tunamsheshimu lakini naona sasa anachotaka kuwaaminisha watanzania mara zingine kimekuwa na utata. Licha ya mimi kujitoa katika mijadala mingi inayohusu mambo hayo anayodanganya kwa kumheshimu, sasa naona haoni aibu.

Zitto ajitokeze sasa aseme kuwa hakumsaidia Mohamedi Dewji Mbunge wa Singida Mjini wakati wa uchaguzi Mkuu 2010, ajitokeze na Dewji Mwenyewe tuweke mjadala huu wazi kwa manufaa ya nchi yetu.

Nimechoka. Ukweli utatuweka huru, tunahitaji mabadiliko
 
Hakuna mjadala Zitto ni msaliti namba moja akishirkiana na CCM kuichakachua CHADEMA lakini ameshtukiwa mapema mchana kweupe na ndo maana muda mwingi maccm wametumia kumsaidia huyu pandikizi.
 
Acha kuwa kama kuku mwenye kideri,mavi yakimganda nyuma hayatoki mpaka anakufa.Babu yako slaa keshafunga mjadala.Mbona hujiulizi kuwa siku 14 zimepita ama lah.!?
 
Isango,

Najua ulikua mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema jimbo la Singida Mjini.

Jimbo ambalo mgombea wa CCM alipita bila kupingwa kisha baadae Mkurugenzi wa tume akatangaza kuwa upo kwenye kinyang'anyiro na uchaguzi ukafanyika kwa ushindani.

Mwenyekiti aliyepita akishirikiana na kiongozi "Mhusika" walituhumiwa kushiriki hujuma hii ya kuuza jimbo!
 
Last edited by a moderator:
Achana na huyo zitto.. watu tushamtema siku nyingi... mtu na akili zako timamu huwezi kukubaliana na mambo ya zitto
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naona wanaojua ukweli kwamba zzk akifanya mdahalo wataumbuka wanatoa komenti za kijinga zisome uone
 
Issango,

Najua ulikua mgombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema jimbo la Singida Mjini.

Jimbo ambalo mgombea wa CCM alipita bila kupingwa kisha baadae Mkurugenzi wa tume akatangaza kuwa uchaguzi utafanyika.

ben kuna point ulikuwa unadrive hapa go ahead ili issango afunge
 
Zitto anajiona ni genius na watanzania wote ni wajinga na mazuzu wasioelewa mambo!!

Mwisho wa Zitto utakuwa mbaya sana,kashapindikizwa udini na mkulu!!!
 
Kama kweli atajitokeza katika mjadala huu nitaamini ni kweli, zitto anakipenda chama, lakini kama hatajitokeza nitajua yaleyale mambo yake, sarakasi za kinafiki tu!
 
Huyu Mh. Zitto inaonekana alikuwa anafanya kazi mpaka za Mwenyekiti, Katibu mkuu na Kamati Kuu ya CHADEMA!.

Kitu kinachonishangaza ni kuwa, katika hizi kazi zake, yale mabaya yote anayabeba yeye lakini mazuri yote wanabebeshwa Kamati Kuu, Katibu Mkuu na Mwenyekiti Taifa.

Hivi mipaka ya kiutendaji ya CHADEMA iko wapi mpaka kiongozi mwingine afanye kazi za viongozi wengine?.

Hizi hoja hizi!

Mkiambiwa CHADEMA haijajipanga, mnaanza kupiga kelele.
 
hawezi kuthubutu, zitto ni muoga sana ! Na kwa vile NCHIMBI kachinjiwa baharini ndiyo kabisaaa !
 
Status
Not open for further replies.
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom