Naomba mbinu za kukuza ukurasa wangu wa Instagram

elvis richard

Senior Member
Dec 6, 2014
195
205
Jamani ndugu zangu ..
Nimewakutanisha hapa ili tujadili kitu kimoja ambacho nahisi nahitaji msaada wenu wa hali na mali...

Mimi ni kijana ambaye nimejikita katika kujenga brand yangu kupitia mitandao hasa mtandao wa Instagram.

Kikubwa ambacho nimekikusudia na naendelea kufanya sasa hivi ni kukuza brand kupitia video za vichekesho pamoja na memez .

Lengo langu hasa ni kutaka kuikuza page yangu kupitia vichekesho kama nilivyosema hapo awali. Kupitia page yangu, nataka niwe na uwezo wa kutangaza biashara za watu na hatimaye kuwa ambasador wa bidhaa za wafanya biashara mbalimbali na hivyo kujiongezea kipato.

Lakini shida inakuja kwamba imekuwa ngumu sana kwa page yangu kukua. Namaanisha followers pamoja na views zimekuwa chache sana kwa kila post ninayo ituma.

Katika videos zote nilizopost ni moja tu ndiyo iliyopata views 2000 tu na si zaidi.

Pia napata followers kwa uchache sana.

Sasa hivi nina followers 624 tu ...kitu kinachoniumiza sana .

Wataalamu naombeni mnipe shule ya maana ili niweze kutoboa kupitia Instagram ili niweze kufikia lengo langu.

So far ninachokijua ni kwamba ili post ziwafikie wengi zaidi ni kwa kutumia hashtags peke yake.

Naombeni mnijuze ni kwa namna gani naweza kuongeza followers pamoja na views kwenye page yangu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wataalamu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mambo mawili marahisi unaweza tumia

1.uwe na hela promote Instagram watu wataona, kiasi kidogo kama 15,000 wataona maelfu ya watu.

2. Uwe na muda, follow watu maarufu kama diamond, Millard ayo etc Hakikisha akipost kitu tu ndani ya sekunde ya kwanza ujue, kuwa wa kwanza kulike na comment, jina lako litaonekana juu kwa yoyote ataepitia, hapo utapata viffolower kadhaa vya bure.
 
Back
Top Bottom