Mama Mzungu
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 215
- 368
Habari za mchana wanajamii,
Naombeni mbinu za kuishi na mume bahili/mchoyo.
Mwanaume ni mchoyo jamani, vitu viikisha ndani atajikausha utafikiri sio yeye ndo baba wafamilia. Umeme unakatika atauchuna na mtalala gizani, asubuhi ataondoka bila kuacha hata mia sijui anawaza mtakula nini, kwakuwa nina mtoto mdogo na wadada wa kazi inabidi niwaachachie pesa za matumizi, gari akiriharibu hatengenezi ng'o na litaendeshwa hivyo hivyo mpaka utakavyoamua kulipeleka gereji mwenyewe.
Nimechoka jamani basi ikokea katoa hela utakuta kaweka 100,000 kabatini na hakwambii kama ni pesa ya matumizi.
Akishatoa hiyo atajikausha hata miezi minne inaweza pita bila kutoa kitu na bado ataendelea kukuomba hela,mara naomba hela nikaweke mafuta kwenye gari, mara naomba hela ya sadaka ili mradi ile aliotoa mpaka iishe.
Basi nikafungua biashara sehemu, akaidakia yeye akaanza kuisimamia, sijawahi ona hata mia kutoka kwenye ile biashara, kodi ya pango ikaisha, hela hata mia, ikabidi nilipie tena kodi, bado sioni kitu yaani kama hakuna biashara inaendelea,ukimuuliza anakuwa mkali
Basi nimeamua kutolipa tena kodi ya pango ikiisha, na TRA Silipi. Nimemsema sana lakini naona habadiliki.
Nimfanyeje mwanaume wa hivi khaaaa
Aisee pole sana, hakuna raha kama kuhudumiwa na mwanaume 🤣🤣. Ina maana huo ustingy umeanza baada ya ndoa? Kama alikuwa hivyo kabla basi ni mzigo wako vumilia tu.
Kama kaanza hiyo tabia sasa hivi basi chunguza hela zake zinaenda wapi. Na hakikisha hata kama hela haachi wewe usitoe kabisa, yaani chuna kabisa ila cha msingi hakikisha wewe na mtoto mnakula msife njaa. Huyo cha uchoyo mwache na uchoyo wake Wala usiumize kichwa, fanya yako na HELA USITOE.
Mimi sipendi wanaume wazembe katikati huduma, ningekutana na huyo mtu 🤣🤣🤣 haki ya Mungu angetoa tu. Nipo tayari kulala giza, chakula hapati Na business zangu hagusi.
I am sorry ila sometimes unahitaji kusimama na kuonyesha msimamo, usisahau kupiga goti kumuombea huyo pepo amtoke. Mimi na support sana kusaidia wanaume katikati shida ila si huo upuuzi. Ni Mwiko kataaa mama, all the best.