Naomba mawazo yenu juu ya mzazi mwenzangu kuhusu mtoto

Rudaguza01

Member
Aug 11, 2017
92
37
Mnamo miaka 5 iliyopita nlikuwa mfanyakazi kwenye kampuni Fulani kule arusha, ilitokea nikajikuta naangukia kwenye mtego wa kimapenz na binti mmoja ambae alinitega kisawa sawa.

Wiki mbili za mahusiano yetu binti aliniuliza kuwa nitamuoa lakn kutokana na kipaumbele cha malengo yangu ya kimaisha kwanza, nlimwambia ukweli kuwa bado hlo suala bado sjaliweka kwenye front page ya maisha yangu kwahyo jibu ni bado mapema sana na hatujafahamiana Tabia zetu kuahidiana kuoana.

Baada ya hapo binti aliniomba kusitisha uhusiano na mimi baada ya kuona kuwa hakuna ndoa.

Kumbe wakati tunasitisha mahusiano yule binti alikuwa ameshashika ujauzito na hakuniambia mpaka akaondolewa kazini hadi pale alipo jifungua ndo akanipgia simu akiniambia alikuwa na mimba yangu na amejfungua na malengo ni kuniuliza kama motto namkubali au namkataa..!

Nilimkubali mtoto nikaanza kusimamia mahitaji yote mavazi, magonjwa na gharama zote zimuhuzo mtoto. Mwaka Jana nimetoka kazini nikakuta ametoweka kwao na mwanangu kwa kisa eti alienda kufanya kazi na mwanetu.

Nlipomtaka alete mtoto amuone baba alidai nitume nauli nikamtumia na ilikuwa juzi tu mwaka huu lakini cha kushangaa amekuja akiwa mjamzito tena na malengo alikuwa anampeleka kwao amuache huko mwanangu ili arudi alikokuwa.

Mtoto saiv ana miaka minne nilikuwa nataka nimtoepo ili akasomee kwenye shule ninayoitaka mimi lakn ninanyimwa mtoto wakati mtoto ananililia sana na pale alipo yupo na bibi mzaa mama yake na hayuko na wazazi wake baba na mama lakn Mimi namhitaji sana japo nipo single bado.

Nifanyeje kumpata ili nimpe huduma zote nikiwa nae karibu? Nitashukuru kwa maoni na ushauri wenu;

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, we ongea na mzazi mwenzako, washirikishe wazazi wa pande zote mbili. Halafu suala la kumchukua mtoto sahau kabisa. Ushasema una maisha ya kisela, kulea mtoto sio kama kunya. Mnaweza kukubaliana mtoto either akae kwa wazazi upande wa mama au upande wako.
 
Umeongea point,watu wanadhan ukiwa na hela tu ya kumlisha na kumvisha bas malez umemliza,wanajidanganya sana,nakuunga mkono kulea mtoto sio kama kunya
 
we nawe mjinga? unakataa kuoa huku unamfua pichu mwenzio

eti huhajipanga

mbona mtoto kaja na unalea hadi unamlilia umchukue? je hapo ulijipanga na hilo?

wanaume wengine mnawaharibia mabint future zao angali wadogo

bint anaishia kupandwapandwa km punda.
 
ungempata MTU wa ustawi wa jamii...angekupa taratibu zote
 
Pole sana mkuu, we ongea na mzazi mwenzako, washirikishe wazazi wa pande zote mbili. Halafu suala la kumchukua mtoto sahau kabisa. Ushasema una maisha ya kisela, kulea mtoto sio kama kunya. Mnaweza kukubaliana mtoto either akae kwa wazazi upande wa mama au upande wako.
Mkuu Unaweza mchukuwa Mwanao na hakuna wa kuweza kukuzuia kama ukiestablishi sababu za Mazingira hatarishi ya Makuzi ya Mtoto.. na Kwa Ujumbe wako Mtoto yuko kwenye Mazingira hatarishi tena Makubwa. Hivyo Cha kufanya Ongea na huyo Mama kuwa kwa kuwa ana commitment na Mahusiano Mengine then huna haja yakumbebesha majukumu ya kumlea Mtoto akupe uishi naye wewe kwa njia utakayoona inakufaa ila siyo kwenda kumtupa Boarding...

Kingine anayesema haiwezekani basi huyu hajui Malezi nini au Anadhani Malezi ya Mtoto ni Mpaka kuwepo Jinsi ya Kike Mahali pa Makuzi.. Siuyo Sababu. Mtoto anaweza kulelewa mahala popote as long as Kuna Mapenzi kwa Mtoto. Na Kwa jinsi watoto walivyo siku hizi kuzijua haki zao Mapema Ile Dhana ya Kuwa Mtoto ni Mama ilishapitwa na wakati .

Kijana kama utahitaji Msaada wa ziada juu ya hili suala karibu. Ila Malezi ya mtoto siyo Mama Bali Malezi ya mtoto ni Mapenzi ya Mlezi kwa Mtoto.
 
Ahsante kwa ushauri wako.
 
Wiki mbili za mahusiano yetu binti aliniuliza kuwa nitamuoa lakn kutokana na kipaumbele cha malengo yangu ya kimaisha kwanza, nlimwambia ukweli kuwa bado hlo suala bado sjaliweka kwenye front page ya maisha yangu kwahyo jibu ni bado mapema sana na hatujafahamiana Tabia zetu kuahidiana kuoana.

Baada ya hapo binti aliniomba kusitisha uhusiano na mimi baada ya kuona kuwa hakuna ndoa.
Week mbili na amepata mimba?????? Au sijaelewa na una uhakika huyo mtoto ni wako kweli?
 
we nawe mjinga? unakataa kuoa huku unamfua pichu mwenzio

eti huhajipanga

mbona mtoto kaja na unalea hadi unamlilia umchukue? je hapo ulijipanga na hilo?

wanaume wengine mnawaharibia mabint future zao angali wadogo

bint anaishia kupandwapandwa km punda.
Siyo hvyo ndugu. Tulikutania kazin na kingne suala la mimba lilikuja kama surprise bila kulipangilia na nlipo toka kazn nliwafuata mama na mwanangu ili tuanze familia pamoja ndo akawa ametoweka kwao na mwanang na matokeo kule alikokwenda ametokako akiwa na ujauzito wa pili wa mtu mwingine ambapo mwanangu amempeleka kwa wazazi wake na kisha kurudi kwa huyo ambae ambae yuko na mimba yake na namba za simu kabadilisha.
 
Ila na wewe, mtoto wa miaka minne ni mdogo sana kumtenganisha na mama yake, Ila kwakuwa na yeye hakai nae, kuliko kumsumbua bibi bora ukae na mwenyewe, hapo inategemea hekima na busara zako kuongea na mama mtoto wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Week mbili na amepata mimba?????? Au sijaelewa na una uhakika huyo mtoto ni wako kweli?
Ndio mkuu.
Mtoto ni wangu maana tunafanana kama vle mm ndo nliingia tumbon na kutoka na kingne miez ya ujauzito ilikuwa sahihi nilihesabu kwa umakini na vidole nikahesabu.
 
Back
Top Bottom