Naomba mamlaka za Serikali zifanye uchunguzi mamlaka ya maji AUWSA

Billions

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,875
2,000
Habari za kwenu

Naomba kwa niaba ya watumiaji wote wa mamlaka ya maji safi na taka mkoa wa Arusha nilete malalamiko kuhusu huduma za maji haswa katika upande wa kusoma mita na ankara za maji.

Ni siku kadhaa zimepita sasa baada ya sintofahamu iliyotokea katika utumiwaji wa ankara za maji kwa wateja wa maji, ambapo bili za maji hua zinatumwa katika simu kwa wateja, ila siku hio palitokea sintofahamu ambayo hadi sasa haieleweki ni kwa sababu gani

Kwanza uliingia ujumbe kua unadaiwa anakra ya maji kiasi fulani, ghafla ikaja ujumbe mwingine kua wamekosea kutuma ujumbe kwamba ankara ama bili hio ya maji ina makosa. Baada ya muda fulani wateja wakapata ujumbe mwingine ambapo ankara imezidi hata kiwango kile kidogo cha mtumiaji wa maji, yani kama kila mwezi ulikua na matumizi yasiyozidi shilingi elfu 14, basi bili yako inaongezwa maradufu na kua mara tatu ya hicho kiwango.

Tulipoenda ofisini tukaambiwa ya kua eti ndio bili zetu hizo za maji, jamani kama sio ufisadi huu ni nini? Yani ankara za maji unazidishiwa halafu unaambiwa ndio bili na wakati matumizi yako ya maji ni madogo?

Wananchi wengi wamelalamikia jambo hilo na zaidi wamekua wakilalamika kuhusu huduma mbovu ambazo wamekuwa wakizipata. Tunaomba mamlaka za uchunguzi ikiwemo TAKUKURU, AUDITORS wa serikali, na maafisa kutoka serikalini waje kufanya UCHUNGUZI WA KINA katika mamlaka maji safi na taka mkoa wa Arusha. Tunaamini na tuna wasiwasi yanaweza kutwa madudu makubwa kwa sababu sio kwa kuongezewa ankara hizi za maji kupita kiwango. Serikali hii ni serikali makini na naamini kilio cha watumiaji wa maji arusha kitafika mahala husika kwa uchunguzi zaidi.
 

ThemiOne

Member
Mar 9, 2017
35
125
Mkuu kuna utaratibu wa kuapeal... Nenda kwa meneja ikishindikana mkurugenzi ikishindikana peleka malalamiko yako EWURA.. nakuhakikishia haki yako itapatikana na fidia juu...

Kuna kakotabu fulani nadhani pitia hata kwenye tovuti yao kitakuwepo ambacho ndio kama mkataba wako na wao humo ndani kumeainishwa kila kitu
 

Lesoroma

Member
Aug 5, 2011
52
125
Mkuu hiyo siku walikosea kwa watu wengi ila baadae walituma ujumbe WA kuomba msamaha na walirekebisha ila kama unaona Kuna jambo ambalo halijakaa Sawa mwone meneja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom