Naomba majibu yenu eti EGM ina kaZI GANI

Kwa Bongo kazi haziangalia combination ya Advance!! EGM unaweza ukaja kusoma Economics au BCom kwahyo kazi ni kwako!
 
-economist
-accountant
-acturial
-banker
-geologist
-financial analyst
-marketing industry inakuhusu.
-politician.
 
Haijalishi unachosoma,nilijua kila anayesoma egm anakuwa pilot kumbe wengine wamekuja kuwa wanasiasa
 
swali zuri sana ....nakumbuka nlisoma CBG bila kujua future yake na yote hiyo na hiyo yote ni kwa sababu nilikosa mtu wa kunshauri

back to topic
anaeza Fanya
architecture, banking and finance,bcom,some engineering hasa za sua,planning na nyingine nyingi
 
Hakuna combination ya A-level inayolipa yenyewe kama ilivyo.kwa kuwa hakuna ajira zinazotambua form six pekee . Ila fikilizaidi ya form six.A-level ni kama kidaraja tu kwenda kwenye elimu ya chuo.
 
EGM ni hatua tuu ya kuelekea kwny taaluma kama uchumi, ualimu, uhasibu, ufundi mchundo n.k. Unachotakiwa ni kufanya vizuri ktk hatua hii ili uweze kuwa na choice nzuri ktk hatua zinazofuata!
 
Kama unapenda ualimu soma egm..

kumbe bado upo my son!!!! nlisomaga EGM enzi hizo naleo nafurahia maisha ya chuo, sisomei ualimu...ila kama ningetaka kua mwalimu nafasi nlikua nayo tena nzuri sana!!!!
kupenda ualimu sio lazima usome egm!!! unaeza soma hata pcb, pcm ,hkl na ukawa mwalimu pia tena mzuri tu!!! kwa hiyo mwanagalie mdogo wako alieleta mada na utoe mawazo ya kumwelewesha zaidi.
 
Nataka kuichukua A level. Ila najua kaz zake chache sana

kwanza karibu sana JF.
EGM ni mjumuiko wa economics, geography na mathematics...ukisoma egm na ukafaulu vizuri..basi chuoni unanafasi kubwa sana ya kuchagua fields ambazo utaeza somea. kwa uwepo wa mathematics katika hii kombi wengi waliosoma egm wana uwanga wa kusoma kwanza kozi yoyote ya biashara(accountants, finance n.k) unazifahamu hapa duniani!!! kuna kozi kama sheria, education kote huku wanafit bila shida kama ukifaulu!!!
actuarial sciences,architecture, na kama mdau alivyosema hapo juu kwa baadhi ya vyuo wanapokea watu wa egm katika fields za engineering(na hapa kama umefaulu maths na una background ya physics) unaeza pata nafasi pia....kwenye fields za computer bado hawa watu wana nafasi nzuri tu(japo inategemea na chuo), geology. hizo ni baadhi ya fields tu ambazo mtu wa egm anaeza somea akifika chuoni!!!
kazi kwako kasome ufaulu nafasi unayo na siochache kama ulivyosema!!!!
 
Taxation
Banking
Insurance
B.com
Businesses
Economics
Architecture
Agriculture
Administration
Human resources
Education
Land
Statistics
Laws
Environmental
Planning
Sociology
N.k
 
mie nlisoma egm na chuo nkapiga accntncy.
Na sasa muhasibu mmoja mzuri sana nbaa wanantambua.
So dogo kazana tu na mambo ya ajira achana nae jikite kwenye kusoma ajira utamaliza chuo na bado utasanda mtaani.
 
A Level ni daraja la kukuvusha uende upande wa pili wa mto hasa kitaaluma. So EGM ukikomaa nayo vizuri na kufaulu vizuri itakulipa sana huko mbeleni maana uwanja ni mpana kuchagua uwe nani ilimradi tu umefaulu vizuri. Kaza msuri na mtegemee Mungu atakuwezesha kufanya vyema. All the best.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom