gigabyte
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,202
- 5,780
Unapoambiwa mifumo imara maana yake ni kwamba nchi inakua ya wananchi na wote kuanzia rais na taasisi nyingine zote za serikali watawajibika kwa wananchi kupitia taratibu zilizowekwa na kama kuna kasoro au mianya yoyote yakuenenda tofauti na miongozo hatua zinachukulika automatic.Naona kwenye mfumo mnajikita kwenye mifumo inayolinda taasisi za chini zisiingiliwe na rais. Hamtaki kujishughulisha kwamba hizo taasisi za chini zinaweza kutumia hiyo mifumo inayowakingia kifua kufanya mambo ya ovyo kwa kisingizio cha kwamba ni wao ni mihimili inayojitegemea wasiingiliwe.
Kama mnaogopa kwamba katiba inampa rais madaraka makubwa sana na kwa udhaifu wa kibinadamu anaweza akayatumia vibaya, kwa nini msiogope pia kwamba uhuru wa mihimili mingine nao unaweza kutumika vibaya?
Kama inshu ni kuweka sheria kwamba yeyote atakayetumia vibaya ashtakiwe bila kujali yeye ni mhimili gani, swali litabaki nani atamfunga paka mwenzake kengele. Na ikumbukwe sisi raia hatujui kinachoendelea jikoni, tunalishwa tu matango pori na hayo mamihimili. CAG anapokuletea mareport kwamba shirika hili na lile limepata hasara, hatuwezi kujua uhalisia wa kile kilichoendelea nyuma ya pazia wakati akifanya hayo mahesabu.
Wape watu heshima wanayostahili, nayo ni kwamba mifumo inategemea watu.