Kizazi cha google hadi barua unataka copy an paste... changamsha akili fikiria unataka andika jambo gani kuhusu hiyo barua then labda kwa msaada wa format wa barua za kuombea kazi watu tukusaidie. Mambo mengne tusibweteke vijana EAC inakuja epuka kuwa tegemezi hadi kula mwenyewe baadae utashindwa kwa kusema hujui mdomo upo wapi.
Ni uvivu au? yaani barua tumejifunza kuandika tangu tukiwa primary...... sasa ata kama mimi HR nataka kukuajiri wewe inawezekana kweli... kama barua ni shida report utaweza kweli.... ni mawazo tu, barua ni kitu cha kuandika mwenyewe
Okay format yake huwa kama hivi ifuatavyo. Nitaweka namba kuashiri ndio kinachoanza mpaka mwisho na natumai itakuwa msaada kwako kaka mkuu.
1. Utaanza na anuani yako (adddress) ambayo hii itakaa upande wa kuliwa wa karatasi yako ya barua ya kazi. Na vitu vya kuzingatia ni jin lako kamili, sanduku la posta, mjini, nchi, na utamaliza na namba zako za simu pamoja na barua pepe kama utakuwa nayo.
2. Utaandika anuani ya sehemu unayopeleka hiyo barua yako. Kwa mfuatano kama wa namba 1 ila kumbuka tu kuwa hapo utaiandika barua inaenda kwa nani kwa kuandika cheo chake HR, GM, CEO nk. NB: hii itakaa upande wa kushoto
3. Utafungua barua kwa kuandika Dear sir/ madam / ambayo utaandika chini ya anuani ya ofisi chini japo ruka mstari mmoja.
4. Kichwa cha habari ambayo inakuwa na YAH: au ref: kwa lugha ya kiingereza na utaandika dhumuni lako katika kichwa hicho cha habari.
5. Utaandika barua yenyewe chini ya kichwa cha habari. Kumbuka kuanza kwa aya kwa kila jambo lenye uzito aidha unaelezea sifa yako au elimu au jambo lolote lile.
6. Ni Saini yako ambayo itakaa upande wa kushoto wa aratasi yako
Nadhani kwa uchache utakuwa na official letter nit and clear kwa maudhui uliyolenga. Hope itakiwa msaada japo kwa uchache. Asante.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.