Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Naam, Mimi ni mwanachama wa muda mrefu hapa kwenye ukurasa wa Siasa. Nimetoa mchango wangu kwa umoja huu kupitia ukurasa huu. Nimerekebisha baadhi ya mambo kutokana na hoja zangu na niseme tu nimekuwa nikifarijika sana pale ninaposhauri au kutoa hoja ikaleta positive impact kwenye jamii.

Nimefika kikomo cha kushiriki nanyi, nimefika wakati ambao bila ridhaa yangu nawajibika kukaa pembeni bila kuandika Wala kuona chochote kuhusu hata wale watakaosoma ujumbe huu. Nafika ukomo na nauona ukomo wangu.

Ninapoaga leo hapa tarehe 23/06/2021 saa 23: 15 usiku naaga kwa uchungu mkubwa kwamba moja ya Jambo nililopigania kwenye jukwaa, kwenye jamii na kwenye mitandao ya kijamii halijafanikiwa kutokea na naamini sitoweza kushuhudia likitokea. Jambo ilo si jingine Bali ni KATIBA MPYA YA JMT.

Nilitamani nimshirikishe Mwalimu Nyerere juu ya hatua hii huko alipo endapo ningekutana naye lakini nasikitika kwamba sitoweza kumwambia chochote juu ya agenda hii. Ni maumivu makubwa.

Niliipigania Katiba baada ya kuona kwamba mfumo wakusimamia haki nchini haupo Tena kwenye mategemeo ya sheria za nchi. Mfumo huo toka enzi ya Mkapa hadi leo hii awamu ya sita umebaki kutawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja ambayo ni maamuzi ya Mkuu wa nchi.

Niliipigania Katiba mpya baada ya kuona taifa langu linazidi kuongeza Kinga za kushtakiwa kwa kundi la wanasiasa na Watumishi wa umma. Mkakati huu wakutochukuliwa hatua za kisheria kwa viongozi utaliua taifa na ndipo nilipoona natakiwa kusimia hoja ya Katiba mpya itakayotamka na kutekelezwa kwa amri au takwa la binadamu wote wapo sawa chini ya sheria.

Nilijaribu na naondoka bila kuiona, naamini waliobaki watazidi kuisimamia hii na itapatikana kabla Taifa halijapoteza kabisa imani miongoni mwa wananchi na kuanza kusambaratika.

Ninaponyamaza na nikiwa katika maumivu makubwa nimepata nguvu yakuuandikia ulimwengu kwamba Tanzania inahitaji katiba mpya.

Kwa Mhe. Rais, kwa Hali ilipofikia Sasa, maendeleo pekee unayoweza kuwarithisha Watanzania wakiwemo watoto wako na wajukuu ni katiba mpya. Jenga barabara, vivuko nk lakini tambua kiu ya umma wa Watanzania inahitaji katiba inayotokana na kizazi kilichopo Sasa.

Wasaidie Watanzania, wape katiba mpya. Anzisha mchakato, la sivyo kelele na mwangwi wa kilio cha Watanzania kitaambatana nawe Kama kinavyoambatana na mzee Kikwete hata baada ya kustaafu. Naondoka mie, nakuomba Jambo naamini sitoiona katiba hiyo ila wape wananchi katiba mpya.

Niwashukuruni sana na niwaombe msisite kuendelee kumkumbusha kuhusu maumivu yangu juu ya Tanzania mpya. Endapo lolote litatokea may be ntarudi ila nimefika ukomo. Mwenyenzi Mungu mtoa maarifa na njia akawajaze ufunuo na maono ya mwisho mwema Kama Mimi. Mkaondoke mkiwa kwenye toba na siyo mkiwa dhambini.

Naitwa Beatrice Kamugisha (nick name), naandika kutoka Regency Dar es salaam Tanzania.
 
Mkuu tatizo ni nini? Hapo Regency unasumbuliwa na nini kwa muda gani? Nakuomba utubu mazambi yako yote kama unahisi upo katika hatua za mwisho za kufariki. Sisi wote njia yetu moja,ni suala la muda tu
 
Asee, nimepata mstuko wa moyo na nafsi gafla nikakumbuka kumbe sisi wanadamu tuna muda mchsche tu wakuishi hapa dunia tuki mess up kidogo tu tunakosa maana nzima ya maisha na dhumuni letu maishani.

Aijui beatrice anasumbuliwa na nini mpaka anatuaga lakini sad part ni kutoeka kwake bila kutimiza malengo yake.

Kuu beatrice be strong.
 
Mkuu ushaambiwa katiba sio biblia wala msahafu, usemi huu unamaanisha kwamba hata katiba mpya ikipatikana bado watungaji au walindaji wa katiba hiyo wataivunja, na hakuna kitachofanyika. Katiba na sheria zilizopo kuanzia ya serikali na za vyama vya siasa ni mara ngapi zimekuwa zikivunjwa bila wahusika kuchukuliwa hatua.

Mfano chadema katiba au sheria yao ilikuwa inaruhusu mwenyekiti kukaa katika uongozi kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano, Mbowe alipoingia akaivunja katiba na sheria ya chama kwa kubandua kile kifungu kimya kimya bila kufuata utaratibu unaohitajika na mpk leo chama kiko kwenye mikono yake, anafanya atakavyo bila kuchukuliwa hatua na mwanachama wa aina yoyote ndani ya chama.

So mtu wa aina hii hata ikipatikana katiba mpya na akawa raisi bado ataivunja hiyo katiba aidha kwa kuendelea kubaki madarakan kimabavu au kufanya jambo lolote lenye masilahi na yeye bila kufuata sheria wala katiba kama alivyofanya kwenye chama chake. Kwahiyo swala la katiba halina msingi sana kwa sababu hata tuliyo nayo sio mbaya ila tatizo baadhi ya watungaji na walindaji wa katiba ndio wabaya kwa kuivunja watakavyo.

Swala la katiba linatumika kama uchochoro kwa wapinzani, ili watapokuja kushindwa vibaya katika chaguzi zijazo, basi ionekane kuwa tatizo kubwa la kushindwa kwao ni katiba iliyopo na tume ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom