Naomba kuwa Rais Dikteta wa Tanzania

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,452
SIFA ZANGU 1 NI MZALENDO HALISI NA MPENDA MAENDELEO YA WATANZANIA

Naombeni mniulize maswali ili mjue kama mtanichagua nitawafanyia nini watanzania.

Niko serious
 
Natambua Kuwa Urais Ni Heshima Kubwa Sana Ktk Dunia Kupita Zote, Hivyo Nitakuwa Muadilifu Kwa Wananchi Wangu Ktk Kipindi Chote Cha Utawala Wangu Nikiamini Kuwa Baada Ya Kustaafu Wananchi Watanipa Heshima Ya Utakatifu Kabla Sijafa
 
Huwezi kuvunja rekodi ya mbio za mita 100 wakati hata kutambaa hujaanza, wee vipi?

Jee, ushaukwaa angalau ukatibu kata? Inabidi upitie ngazi zote kuanzia kata, tarafa, wilaya, mkoa na hadi taifa.

Hata Kikwete mwenyewe ukuruta aliupitiaga. Kalagha bahoo!
 
mahakama si imeshapitisha wagombea binafsi au hujajua?
 
True dictators do not say they want to be dictators (Caesar, Amin)

Those who say they want to be dictators, by that statement alone, reveal that they do not have what it takes to be a dictator.
 
sasa wewe unanijua au una tu asili ya kubisha?

Tutakuulizaje maswali kama hatukujui? Weka wasifu wako hapa kwenye forum na utambie kwanini tukurushu (sio tukuchague) kuwa dikteta. Labda ungeweka na picha ili kwa wale wanaokufahamu wapate kuchangia kwa wingi.
 
Naomba uulize nitaifanyia nini nchi na tena uanishe ni ktk nyanja gani hayo ndiyo maswali ninayotaka na siyo habari ya kuniambia eti kama nilishakuwa katibu kata.

Maana unanikumbusha mbali sana nilipokuwa naishi tanzania ramani yangu ya ujenzi wa jengo langu ilishindikana kutoka site kwa sababu diwani mmoja hakuipa baraka nilipokuja kufuatilia nikagundua yule diwani hajui kusoma wala kuandika na ramani yangu niliitengeneza chuo kikuu cha Dar tena aliyenifanyia ile kazi ni Engineer mkongwe na mzoefu, nilipomfuata diwani ili anieleweshe ni wapi imekosewa akaniambia nondo zilizowekwa zilikuwa ni nyingi kwa hiyo jengo lingeweza kuanguka kwa uzito, nilipoonyesha mshangao diwani akaniambia niongee kwa herufi kubwa.

kwi, kwi kwi
 
naomba uulize nitaifanyia nini nchi na tena uanishe ni ktk nyanja gani hayo ndiyo maswali ninayotaka na siyo habari ya kuniambia eti kama nilishakuwa katibu kata.

For the sake of argument hebu tuambie from A to Z "ungeifanyia nini nchi" ?
 
Weekend imeshaanza naona...wewe si umesema ni Raia wa Kenya inakuwaje tena?

naomba unielewe kilichonitoa tanzania ni hasira sababu ya kukerwa na hawa mabwana watawala mbumbumbu na wenye ulimbukeni wa mali lakini kama mkionyesha nia ya kunichagua nitarudi kuja kuwanyoosha hao wezi mnaowafuga mafisadi na ktk kipindi kifupi mtajisikia mko mbinguni kama hamtaki basi mtaendelea kuteseka mpaka yesu atakaporudi, na sijui ni lini atarudi
 
naomba uulize nitaifanyia nini nchi na tena uanishe ni ktk nyanja gani hayo ndiyo maswali ninayotaka na siyo habari ya kuniambia eti kama nilishakuwa katibu kata.maana unanikumbusha mbali sana nilipokuwa naishi tanzania ramani yangu ya ujenzi wa jengo langu ilishindikana kutoka site kwa sababu diwani mmoja hakuipa baraka nilipokuja kufuatilia nikagundua yule diwani hajui kusoma wala kuandika na ramani yangu niliitengeneza chuo kikuu cha dar tena aliyenifanyia ile kazi ni engineer mkongwe na mzoefu,nilipomfuata diwani ili anieleweshe ni wapi imekosewa akaniambia nondo zilizowekwa zilikuwa ni nyingi kwa hiyo jengo lingeweza kuanguka kwa uzito, nilipoonyesha mshangao diwani akaniambia niongee kwa herufi kubwa. kwi,kwi kwi

Wewe ndio utuambie utaifanyia nini nchi yako. Tupe sera zako. Sera za elimu, afya, ulinzi, kilimo, ufugaji, siasa etc. What are your policies? Je ziko tofauti na za chama kilichoko madarakani? Ziko tofauti na za vyama vya upinzani hapa nchini? Vipi mfumo wa serikali yako? Utakuwa na baraza kubwa kiasi gani la mawaziri? Utakuwa na mfumo gani wa kiutawala? Utakuwa na mikoa au majimbo?
 
For the sake of argument hebu tuambie from A to Z "ungeifanyia nini nchi" ?

unaona sasa?ndiyo maana nakuambia punguza jazba unapotaka kuuliza kitu nyama hatari nimesema unapouliza swali uainishe ni ktk nyanja gani labda nikisema nyanja hunielewi yaani namaanisha labda elimu, ulinzi ulinzi mali ya uma,kilimo, madini afya nk
 
Wewe ndio utuambie utaifanyia nini nchi yako. Tupe sera zako. Sera za elimu, afya, ulinzi, kilimo, ufugaji, siasa etc. What are your policies? Je ziko tofauti na za chama kilichoko madarakani? Ziko tofauti na za vyama vya upinzani hapa nchini? Vipi mfumo wa serikali yako? Utakuwa na baraza kubwa kiasi gani la mawaziri? Utakuwa na mfumo gani wa kiutawala? Utakuwa na mikoa au majimbo?

samahani nitakuwa najibu mdogo mdogo maana nikiweka zote pamoja watu wataona uvivu kusoma. ninaposema nitakuwa rais dikteta simaanishi kuwa dicteta kwa wananchi nina maanisha dikteta kwa viongozi wabadirifu, Kwanza nikiingia tu kitu cha kwanza ningeanza kwa kupunguza bajeti ya serikali yaani magari yoote ya serikali ningeyapiga mnada kwa watu binafsi ningeacha la kwangu na waziri mkuu tu.pili ningewaondolea ulinzi mawaziri wote isipokuwa waziri mkuu maana najua kama waziri anatenda kazi kwa uaminifu hana haja ya kuhofia kudhurika kama wanavyofanya namibia hakuna ulinzi kwa waziri yeyote wala dereva,sitaki ubishoo ndani ya serikali yangu
 
Dikteta hana maneno mengi, anaongea kwa vitendo zaidi. Hata hivyo, wananchi walioonya uhuru hawawezi kukubali kutawaliwa na dikteta. You need to be strategic politician.
 
nisingeteua mbunge yeyote tena utaratibu wa kuchagua wabunge ungekuwa kama wa big brother africa bba yaani unachaguliwa kwa mapendekezo ya wananchi tu sitaki unafiki wala sitaki mbunge auze au kuweka rehani nyumba yake kwa ajili ya kuhonga wanachama ili wamchague wakati anajua kabisa hata akiwa mbunge mshahara hautamtosha kununua nyumba kama ya zamani,maajabu haya ndugu wananchi
 
Dikteta hana maneno mengi, anaongea kwa vitendo zaidi. Hata hivyo, wananchi walioonya uhuru hawawezi kukubali kutawaliwa na dikteta. You need to be strategic politician.

nimesema udikteta wangu si kwa wananchi ni kwa viongozi fisadi na hili nitawaelewesha wananchi mpaka walielewe maana sihitaji kuchekana nyani kama jk mbona huelewi bro.!
 
Back
Top Bottom