Naomba kuungwa mkono kuiomba Serikali iwakumbuke wahanga wa DECI na walipwe fedha zao

Oct 31, 2016
37
15
Miaka inakwenda siku zinapita , Maisha yana zidi kuwa magumu kisa yaweza kuwa mambo mengine lakini kwa kuwa tuliwekeza kwenye kupanda mbegu DECI miaka ya 2007,2008,na 2009 nalaani kuwa walioizuia DECI ndio wanaosababisha maisha haya kuwa magumu. Tena niwambie heri mimi kwani sikujiunga mwanzo! Niliingia mwishoni! Wako Watumishi wa Serikali (Walimu, Manesi, Waganga Wahudumu na wengine wengi), Wafanya Biashara, Wakulima ambao wameuza nyumba, magari mashamba na mali nyinginezo nyingi na wako hata ambao pengine waliishia mahakamani kutokana na kusimamishwa ghafla mpango huo. Nawaomba nguvu wana Jamii Forum saidia kupaza sauti ili watu wapate fedha hizi hali ni mbaya! Serikali ilizuia mpango huo na ikafunga kesi ambayo hivi sasa imekwisha yapata miaka miwili iliyopita. Kwa fununu fedha hizi zilikuwapo Je Serikali na Mahakama mnataka wale Jamaa wa DECI wapotee na fedha hizo?
 
kaka hilo sahau, wanaoidai CCM wenyewe wanaambiwa kamdaini kikwete sembuse DECI, mi nilipoteza 8m
 
Huo ulikuwa UZUZU, zaidi ya kuwapa pole sidhani kama kuna namna serikali inaweza kujihusisha na janga LA kujitakia!
 
Huo ulikuwa UZUZU, zaidi ya kuwapa pole sidhani kama kuna namna serikali inaweza kujihusisha na janga LA kujitakia!
Serikali iliuunga mpango wa DECI kwa kufungua matawi ya DECI haiwezekani isikachangia watu kupoteza. Tafadhali naomba wale wenye positive mind wachangie nata support yenu ili tutengeneze petition kwa hiyo wale wakatisha tamaa kabla ya kuandika kumbuka kuwa hapa tunajaribu kutetea maslai ya Wtanzania masikini wapatao milioni 10 waliokuwa wamejiunga na DECI
 
Huo ulikuwa UZUZU, zaidi ya kuwapa pole sidhani kama kuna namna serikali inaweza kujihusisha na janga LA kujitakia!

Mfuko huo una wahanga wapatao milioni 10 ambao hivi sasa wanataabika hatuwezi kuwaacha bila kuwasaidia kwa sababu yoyote ile. Fedha hizo zipo! Kwa hiyo we unaona bora wasirudishiwe wenyewe hata kama zipo?
 
Deci ilikuwa ni Pyramid Scheme, Pyramids zinategemea kuingia kwa watu wapya. The moment inaposimama tu ndio hapo hapo inaporomoka inakufa. Kulipwa haiwezekana kwakuwa wanaodai wengi pesa zipo kidogo!!! Watalipa kwa kutumia formula gani? Na je uhakiki utafanyika vipi? maana Deci sio benki kwamba ina kumbukumbu nzuri.
 
Kwa hiyo serikali itumie hela zetu za walipa kodi izigawe kwa waliocheza DECI? Haiwezekani.
 
Tangu lini umeskiaa serikali ya chichiem inarudishaga hela hiyo sauzi kabisa....
Si unaona wazee wa jumuiya ya afrika mashariki mpaka leo jiiiiiii

Ova
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom