Naomba kuuliza wataalam wa haya mambo

Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
806
1,336
Ni mwezi sasa umepita toka nikumbane na hili janga.

Nina kawaida ya kuamka saa kumi kwenda kazini

Leo ni mwezi umepita, nilivyofika sehemu ya kupanda gari kuelekea kazini ,mbele yangu naona kuna ice hizi min-bus ,ikasimama mimi nikaipanda ,

Mle ndani ya gari kulikwepo akina mama na akina baba umri ni watu wazima,sikubatika kupata siti na nilisimama mwenyewe,na konda hakwepo kwenye ile gari

Niliwasalimia lkn hata mmoja hakuitika,mi nikasema ni jambo la kawaida

Ukaaji wao wote walinamisha vichwa vyao chini

Nilivyofika barabara kuu nikamwambia dereva nishushe hapo,kweli alisimama nikampa Ela alikataa kupokea mi nikashuka na kuendelea na Safari ya kuelekea kazini,

Jioni nilivyorudi home,huwa nina kawaida ya kwenda kujichanganya na wazee wa kwenye kahawa japo c tumii kahawa ,napenda tu stori zao,

Nikawasimulia,wote walinigeukia na kuniambia una bahati Sana kwenye maisha yako,wengine wakaenda mbali wakasema huko musoma kwenu ulitoka vzr,mimi nikapuzia tu.

Msaada wangu ni Yesu huwa nasali nikiamka na kurudi na ndo kanuni yangu,kwa Mungu kuna ulinzi,na haya mambo yapo.

Mungu ana manguvu sana
 
Duuuh! Nasikia wengi huishia pabaya. Huenda ulidandia hice ya wachawi mkuu. Shukuru mungu sana.
 
Ndani ya hilo gari kulikuwa hamna pulukushani yoyote kama kuchezea simu kuongea wao kwao??
 
Wanaccm hao walikuwa wanaenda uwanja wa Taifa kwenye kampeni
Na konda wa hio gari aliyekataa pesa ya mtoa mada ni huyo jamaa hapo pichani.
JamiiForums409068559_680x455.jpg
 
Duh! JF kila muda ni chai. Siyo asubuhi, mchana wa jua kali ama usiku.

Mtupumzishe tupate hata mlo mmoja wa chakula.
 
Ni mwezi sasa umepita toka nikumbane na hili janga.

Nina kawaida ya kuamka saa kumi kwenda kazini

Leo ni mwezi umepita, nilivyofika sehemu ya kupanda gari kuelekea kazini ,mbele yangu naona kuna ice hizi min-bus ,ikasimama mimi nikaipanda ,

Mle ndani ya gari kulikwepo akina mama na akina baba umri ni watu wazima,sikubatika kupata siti na nilisimama mwenyewe,na konda hakwepo kwenye ile gari

Niliwasalimia lkn hata mmoja hakuitika,mi nikasema ni jambo la kawaida

Ukaaji wao wote walinamisha vichwa vyao chini

Nilivyofika barabara kuu nikamwambia dereva nishushe hapo,kweli alisimama nikampa Ela alikataa kupokea mi nikashuka na kuendelea na Safari ya kuelekea kazini,

Jioni nilivyorudi home,huwa nina kawaida ya kwenda kujichanganya na wazee wa kwenye kahawa japo c tumii kahawa ,napenda tu stori zao,

Nikawasimulia,wote walinigeukia na kuniambia una bahati Sana kwenye maisha yako,wengine wakaenda mbali wakasema huko musoma kwenu ulitoka vzr,mimi nikapuzia tu.

Msaada wangu ni Yesu huwa nasali nikiamka na kurudi na ndo kanuni yangu,kwa Mungu kuna ulinzi,na haya mambo yapo.

Mungu ana manguvu sana

Mshana Jr mpe ushauri.uzi huu alishatoa mshana
 
Mkuu umenikumbusha kipindi naishi Mburahati mara kwa mara nlikua nakumbana na mauzauza hadi kusababisha kununua usafiri binafsi.

Kubwa kuliko ambayo sitokuja kusahau kuna siku nilitoka mida ya saa9 hivi ile paap..! nilikutana na kikundi cha watu pand za madoto sokoni walikua wamevaa mavazi ya rangi nyeusi na wengine nyekundu cha ajabu baada ya kupishana nao nikapata tamaa ya kuwatizama vizuri ila nlipogeuka hata siku waona wakati njia walioongoza ilikua imenyooka.
 
Mm ndo nlikuwa dereva, una bahati tuu la sivyo ningekupeleka maskani kwetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom