Naomba kuuliza: Msaada wa haraka kuhusu Western Union Bank

TheMeek

JF-Expert Member
Mar 12, 2016
460
397
Ndugu Wanajamvi,

Tafadhali , naomba kuuliza kuhusu utaratibu wa kupokea pesa zilizotumwa kwa njia ya Western Union.

Kiufupi, nimetumiwa pesa kutoka Marekani; aliyetuma kasema katuma check. Pia akaniambia niende Branch yeyote ya Western Union Bank hapa nchini kuzichukua. Akasema nikifika na kuwatajia Jina langu + kuwa na vitambulisho , watanipa Fedha hizo.

Hakunipa Security Code Number (MTCN) wala Test Question/Answer.

Nimejaribu kwenda Postal Office hapa wilayani...wakaniambia haiwezekani bila kuwa na MTCN. Nikaamua kwenda mkoani Bank ya Postal, nikapewa jibu hilo hilo.

Nimejaribu kumpa mtumaji taarifa hizi kaniambia , njia aliyonitumia hizo pesa haiitaji kuwa na Security Code Number...,

Wadau naomba kuuliza maswali yafuatayo;-

1. Je hapa Tanzania hasa Mkoa wa Mwanza , kuna Bank ya Western Union? ( au ni mawakala tu)

2. Je ninaweza kuzipata hizo pesa pasipo kuwa na Security Code Number?

3. Nisaidieni ni sehemu gani Mwanza nikienda naweza kuzipata pasipo kuwa na Security Code Number.

4. Je ninaweza kuzipata pesa Hizo kwa kuwa na vimbulisho, Jina la mtumaji, mahali zinapotoka na Jina langu?

Huyu aliyenitumia amenitumia meseji muda sio mrefu anataka nimwambie kama bado Western Union Bank wananisumbua,; Nimeshindwa kumpa jibu...,

Tafadhali, Naombeni mawazo yenu...
 
Huyu aliyenitumia amenitumia meseji muda sio mrefu anataka nimwambie kama bado Western Union Bank wananisumbua,; Nimeshindwa kumpa jibu...,

Tafadhali, Naombeni mawazo yenu...
Sasa umeshindwa vipi kumpa jibu wakati jibu lipo wazi kuwa bado wanakusumbua? Ni mtu unayemwamini na kumfahamu? Western Union SIO bank ila ni agent wa kutuma na kupokea fedha. Na mtu yoyote anaweza kuwa agent akifanya mkataba nao. Ngoja nipitie machimbo nitakuja na jibu la kina zaidi.
 
Haiwezekani kupokea pesa western union bila ya kuwa na MTCN,nimesha wahi kupokea pesa mara nyingi bila ya kuwa na test question na answer,lakini MTCN ni LAZIMA.

Angalia isije aliyekutumia details ni tapeli na hakufanya hivyo,simply mwambie akutumie sender's copy.
Naamini umeelewa kama bado,basi endelea kuuliza!!
 
Sasa umeshindwa vipi kumpa jibu wakati jibu lipo wazi kuwa bado wanakusumbua? Ni mtu unayemwamini na kumfahamu? Western Union SIO bank ila ni agent wa kutuma na kupokea fedha. Na mtu yoyote anaweza kuwa agent akifanya mkataba nao. Ngoja nipitie machimbo nitakuja na jibu la kina zaidi.
Asante Ndugu. Namuamini huyo MTU. Huwa ananitumia pesa. Safari hii katumia njia ya Western Union,... Hapa ndipo shida imeanzia.

Nimejaribu kusoma tovuti ya Western Union , nimeona maelezo ya MTCN

In cash, in your bank account, on a prepaid card or (in select countries) on your phone—ask your sender to use the delivery method that's most convenient for you.

Cash: Visit an agent location near you with your government-issued ID. You'll also need to ask the sender for the tracking number (MTCN). Find an agent location.

Read more at Receive Money | Western Union
 
Sioni option yoyote ya kutuma fedha kutoka USA kuja Tanzania kwa kutumia cheque kama anavyodai jamaa yako. Wewe wasialina nae kwa maelezo zaidi. Mwambie yeye awasiliane na Western ili watatue hili tatizo. Huduma yao ya wateja ni nzuri sana na wako very fast ku-clear up any misunderstandings or mistakes. Yeye ndiye mwenye ufunguo wa tatizo lako. Majibu uliyopewa hapo Mwanza na agents wa Western ni ya ukweli kabisa.
 
Western Union sio bank hivyo hakuna branch yake. Ni kampuni inayojihusisha na kutuma / kupokea hela kwa kutumia mawakala mbalimbali yakiwemo ma bank kama KCB, CRDB, DCB, Tanzania Postal Bank nk
 
its funny, western union wana option mbili za kutuma hela "transfer per minute or kwa mobile phone". Na hiyo security code ndio ya muhimu na lazima wanaitoa hata in case unataka fatilia status ya hela uliyotuma. Mi nahisi jamaa hajakutumia hela.
 
Huwezi kupokea pesa western union bila code pamoja na swali la siri,me naendanga tu na kila kitu lakini hata kama mfano unaitwa john magu busungu lakini ukaenda na kitambulisho kinasoma john M,busungu hawakupi.
 
Nimetoka Western Union ; Jina la Sender limekosewa, nimerudishwa. Wameniambia mpaka niwaandikie Jina Kamili la Sender.

Sasa inaelekea week ya pili nazungushwa kutokana na hela hii ( zaidi ya milion kadhaa)

Mara wakatae Initial Name, mara wakubali. Sasa wamesema Sender Name haimatch.

Security Code iko sawa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom