Naomba kuuliza maeneo mazuri kwa biashara ndogo ndogo kwa Dar es Salaam

Rmgaya

Member
Mar 19, 2017
39
53
Salaam ndugu zanguni

Kiufupi mimi ni mjasiriamali mdogo katika sekta ya kilimo, nimekuwa mkulima wa mpunga kwa takribani miaka mitano na hata wakati huu niko shambani nikisubiri muda wa mavuno uwadie.

Niko hapa mbele yenu kuomba msaada wa mawazo juu ya wazo langu la kutaka kuhamia Dar baada ya mavuno hasa mwezi June kuja kujishughulisha na ujasiriamali katika biashara ndogo ndogo.

Ombi langu ni kuomba kufahamishwa juu ya maeneo mazuri yenye mpishano mkubwa wa watu ambayo naweza kukodi kizimba cha biashara ndogo tayari kwa mapambano pamoja na Aina ya biashara zenye uhitaji mkubwa kwa wateja walio wengi.

Nilishakuja nikafanya survey kidogo kwa baadhi ya maeneo kama Mbagala rangi tatu, Mbezi darajani pamoja na stendi ya daladala pale pamoja na maeneo mengine lakini bado nahisi nahitaji kufahamishwa zaidi.

NATANGULIZA SHUKRANI

20201031_111920.jpg

 
Back
Top Bottom