Naomba kuuliza: Lini Serikalini itaruhusu usafirishaji wa vifurushi vya madini


B

bullion

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2014
Messages
313
Likes
84
Points
45
B

bullion

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2014
313 84 45
Wakuu heshima zenu,

Hapo zamani kabla ya zuio la makinikia, serikali kupitia wizara ya nishati na madini, ilikuwa inaruhusu usafirishaji wa vifurushi au michanga ya madini nje ya nchi. Vifurushi vingi vilikuwa vya madini labda ya copper, lead na mengineyo. Lakini baada ya zuio la makinikia serikali ilisitisha pia usafirishaji wa vifurushi vingine, je baada ya mazungumzo ya makinikia kufikia sehemu nzuri, serikali haina mpango wa kuruhusu usafirishaji wa madini mengine. Hii ni kwasababu wachimbaji wadogo wengi wana vitalu, lakini ni vya resource ndogo, je wasaidiwe vipi kwa hali hii.

Ombi langu, serikali wizara ya madini ingeangalia namna nzuri ya kurusuhu swala hili ili kuwasaidia wachimbaji wadogo wazawa na kuendelea kushughulikia swala la makinikia.

Nawasilisha
 

Forum statistics

Threads 1,238,766
Members 476,122
Posts 29,329,736