Naomba kuuliza kuhusu hawa mbu wa sasa

bobdizo

Senior Member
Jun 28, 2014
137
50
Hivi hawa mbu wa sasa ndio wale waloletwa Muhimbili wakawa wanafugwa kwa kazi maalum ya kuwala sijui au kuzuia mbu wa malaria wasizaane? Maana mtaani kumekuwa na ongezeko la mbu wakubwa kupita kiasi.

Mwenye kujua anijuze please
 
Mkuu kama ni mbu wa kufugwa ni lazima watakuwa wamenona hawawezi kuwa sawa kama hawa wa uswahilini
 
Hawa mbu wanaushirikiano sana aiseee.
Ukiweka net utakuwa wamefunua upande mmoja au wameweka matobo ili wapite.
Ukiwsh feni ili kuwa sukuma utakuta feni imezimwa au wamechomoa wakshndwa hayo utakuta feni ipo imechomekwa haijazimwa ila haiwaki ukiwa washa taa utagundua umeme umekata hasa sijui wenzao wengine wapo Tanesco.
Sasa sema usilale, watakuja na nyimbo zao masikioni wataaimba na kupiga vinanda hadi
Ila nilichogundua dawa yao ni moja tu nayo ni
1462762990450.jpg
 
Hata mm nilikuwa najiuliza mbu gani hawa?? Kwanza mbu huwa na tabia ya uoga, akija kutua kukuuma lazima avizie umetulia humuoni.,,ila hawa wa sasa anakuja direct kama nzi na anatua anakuuma kisha anaondoka...mnaweza rushiana ngumi na akawa anazikwepa na kulazimisha hadi akuume....jaman kuna tatzo kwa mbu wa sasa..
Pia wakikuuma unabaki na kidonda sio kipele tena.....tunaomba bora mturudishie mbu wetu wa mwanzo tulizoea wanatuvizia tu...na wakikuuma unapata muwasho tu sio hawa wa sasa
 
Tatizo sehemu nyingi za wakazi(hasa wa jiji la Dar) wanaishi karibu na majalala. Ni sehemu chache watu wanaweza kujisifu wanaishi mahali pazuri.
 
Kumbe wahanga wa tatizo la mbu tuko wengi eeh.... kiukweli hawa mbu wamekosa aibu wala woga yaani wanajiamini ile mbayaa
Poleni wahanga! Nunueni ile kitu inayowapiga shot sijui inaitwaje akikusogelea unampa mgusisha kituu utasikia paah..
 
Back
Top Bottom