Naomba kuuliza, je waafrika weusi hatunyanyaswi nchi za bara la Asia?

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,169
2,000
Nimeshuhudia sehemu maandamano makubwa sana kipindi hiki cha hivi karibuni baada ya mtu mweusi kuuwawa na polisi weupe huko Marekani, bwana Floyd.

Baada ya hicho kifo watu wameandamana nchi nyingi za bara la Amerika na Ulaya.

Nimeona tshirts, posters na matangazo kibao ya black lives matter sehemu nyingi za Ulaya na Marekani lakini sijaona maandamano ya mtindo huo nchi za Asia.

Sijaona maandamano hayo Saudi Arabia, Yemen, Kuwait, India, China, Korea Kusini, Bahrain, Indonesia, Burma, Taiwan, Japan, Urusi, Pakistan, Malaysia na nyingine.

Juxi hapa wakati huu wa corona waafrika wametendewa vibaya sana huko china kwa kulazimishwa kupimwa corona, kukaa karantini kwa lazima na mambo kama hayo. Sikuona WHO au AU inakemea wala kutoa tamko.

Tumekua tukiona video footage za waafrika wakiteswa na kuuwawa nchi za mashariki ya kati na Asia kila mara.

Swali langu, mbona hatukuandamana kupiga unyanyasaji wa rangi asia, mbona sikuona maandamano ya kupinga unyanyasaji nchi za Asia.

Huko ulaya hata wangungu waliungana na weupe kupinga unyanyasaji wa dola na wa rangi, weupe wa asia hawakuona hilo?
 
Chabrosy

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,360
2,000
Wakati nasoma shule ya msingi tulikuwa tunasoma na watoto wa kike wa waarabu na wahindi wale watoto wa waindi na waarabu wakike walikuwa wanaruhusiwa kufuga nywele na kusuka ila cha kushangaza watoto wa kike wa waswahili hawaruhusiwi kufuga wala kusuka nywele eti kisa nywele zao azikui ni kipilipili kwaiyo wanyoe tu mkuu wa shule alikuwa akisema sasa huu si ubaguzi wa rangi huu why ngozi nyeupe asuke ile ngozi nyeusi anyoe....ubaguzi upo sana tuu hapa kwenye mashule...
 
mangonifera indica

JF-Expert Member
Dec 2, 2017
766
1,000
Tena huko ndio balaa... Nina rafiki anasoma masters yake moja ya nchi za Asia anasema maisha huko kwa watu weusi ni magumu sana
 
Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
850
500
Wahindi ni wabaguzi sana hata wakiwa ulaya au Canada tabia zao za kibaguzi hawaziachi
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
5,182
2,000
Nimeshuhudia sehemu maandamano makubwa sana kipindi hiki cha hivi karibuni baada ya mtu mweusi kuuwawa na polisi weupe huko Marekani, bwana Floyd.

Baada ya hicho kifo watu wameandamana nchi nyingi za bara la Amerika na Ulaya.

Nimeona tshirts, posters na matangazo kibao ya black lives matter sehemu nyingi za Ulaya na Marekani lakini sijaona maandamano ya mtindo huo nchi za Asia.

Sijaona maandamano hayo Saudi Arabia, Yemen, Kuwait, India, China, Korea Kusini, Bahrain, Indonesia, Burma, Taiwan, Japan, Urusi, Pakistan, Malaysia na nyingine.

Juxi hapa wakati huu wa corona waafrika wametendewa vibaya sana huko china kwa kulazimishwa kupimwa corona, kukaa karantini kwa lazima na mambo kama hayo. Sikuona WHO au AU inakemea wala kutoa tamko.

Tumekua tukiona video footage za waafrika wakiteswa na kuuwawa nchi za mashariki ya kati na Asia kila mara.

Swali langu, mbona hatukuandamana kupiga unyanyasaji wa rangi asia, mbona sikuona maandamano ya kupinga unyanyasaji nchi za Asia.

Huko ulaya hata wangungu waliungana na weupe kupinga unyanyasaji wa dola na wa rangi, weupe wa asia hawakuona hilo?
Asio ndio kubaya zaidi kwa ubaguzi wa rangi. Kule hata hiyo nafasi ya kuandamana hakuna tena mtamalizwa kwa mabomu mfie mbali. Ndio maana kule waafrika hawaandani ni kama hapa nchini siku hizi huwezi kuandamana, utafia barabarani ni udikteta ulivyo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom