Naomba kuuliza: Hivi kwanini Walimu hupanda Madaraja bila kusoma ilhali Watumishi wengine wa Umma hawapandishwi?

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,579
2,000
Wapo Watumishi wasiopanda Vyeo wakiambiwa hawajasoma Kozi Fulani kwa miaka 20 tangu waajiriwe. Wanafanya kazi kwa Ufanisi wanajaza OPRAs lakini hakuna cheo wala Kuongezwa Mshahara.

Huwa wanahusishwa tuu kwenye Scheme of Service zikifanyiwa marekebisho. Hivi Utumishi hawaoni haja ya kuhoji mlundikano wa wasiopanda Vyeo kwenye Database zao.?

Ni udhalilishaj na dharau Senior Mtumishi kulingana au kupitwa Mshahara na Junior mwenye sifa sawa. Walimu wao kila baada ya miaka 3 hupandishwa Madaraja bila Kozi.
 

noiselessly hunter

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
4,124
2,000
Ya walimu unayajua weye? Hivi wajua kusomesha ni kazi ngumu Sana, wewe hiyo kazi yako unaifanya Kama wasingekua walimu ungeijua hiyo, ya walimu yaache.
 

Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,073
2,000
Ungekuwa unajua mwalimu wa digrii analipwa mshahara na posho shiling ngapi ukilinganisha na mtumishi wa kada yoyote mwenye cheti au diploma wa Tanesco, nic, nhif, MNH, NHC, NSSF,LAPF, na mashirika mengine usingekuja kuandika huu uzi

pengine ungeshikwa na tumbo la kuhara afu ndo ukaja kuandika. Maana anachokipata mwalimu kwenye mshahara na posho hakifiki robo kwa anachopata mlinzi mwenye cheti cha fomu 4 kwenye taasis kama izo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom