Naomba kuuliza; hii symbion power ndo ile Dowans/Richmond ya Lowassa?

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,470
2,644
Wasalam, nakumbuka miaka ile 2005 iliibuka kambuni ya kufua umeme ya Richmond. Kambuni hii baadae ilikujagundulika kuwa ni kampuni hewa kitu kilichopelekea aliekua waziri mkuu wakati ule ndugu lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu.

Baadae serikali hii ya ccm ilibadili jina la Richmond kuwa symbion mitambo ikiwa ni ile ile ya kampuni iliosemekana ni hewa. Leo hii ni 2018 bado ile kampuni ipo na inalipwa na serikali, naomba kuuliza je hii symbion ndo ile Richmond? Je hii symbion ni kampuni halali? Je haramu inaweza kuzaa kitakatifu?
 
Ndiyo Mkuu, ilianza baada ya juudi za kueletewa Mvua kujaza bwawa la Mtera kutoka Thailand kugonga mwamba
 
Ndio hiyo hiyo na mmiliki wake(Dowans) tuliletewa muarabu koko yule sijui walimtoa wapi
 
Ndio hiyo hiyo na mmiliki wake(Dowans) tuliletewa muarabu koko yule sijui walimtoa wapi
Km ndo yenyewe mbona vigogo waliohusika km kikwete wanalindwa?ina maana sheria na mahakama ya mafisadi ni kwa ajili ya wanyonge km rugemalila na Seth?
 
Juzi Yanga wamehongwa 200 Million za Dowans mbele ya Mkwere, Governor wa Jimbo kuu na mbele ya the Mwana Ruangwa
 
Juzi Yanga wamehongwa 200 Million za Dowans mbele ya Mkwere, Governor wa Jimbo kuu na mbele ya the Mwana Ruangwa
Aisee mkuu wa mkoa wenu ana pesa nyingi kuliko kipato chake halisi, cjui anazitoa wapi takukuru wanamuogopa
 
Wasalam, nakumbuka miaka ile 2005 iliibuka kambuni ya kufua umeme ya Richmond. Kambuni hii baadae ilikujagundulika kuwa ni kampuni hewa kitu kilichopelekea aliekua waziri mkuu wakati ule ndugu lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu.

Baadae serikali hii ya ccm ilibadili jina la Richmond kuwa symbion mitambo ikiwa ni ile ile ya kampuni iliosemekana ni hewa. Leo hii ni 2018 bado ile kampuni ipo na inalipwa na serikali, naomba kuuliza je hii symbion ndo ile Richmond? Je hii symbion ni kampuni halali? Je haramu inaweza kuzaa kitakatifu?

Richmond ni kampuni ya mfanya biashara wa asili ya kiindi na Tanzania. Huyu ana kampuni ya printing inaitwa Richmond Printing ipo pale Houston,TX

symbion kampuni ya kusambaza umeme na hii kampuni ilikuwa inasambaza umeme wakati wa vita vya Afghanistan na wamekuwa wanapewa tender zaidi na jeshi la USA sehemu ambazo makapuni mengine hayawezi kuja. Hii kampuni imeanzishwa na wapelezi mmoja CIA ambaye alikuwa balozi na mwengine alikuwa anafanya kazi jeshi la UK. Walikuja TZ baada ya kupewa tender ya kusambaza umeme vijijini chini ya millennium challenge aliyoanzisha Bush lakini vilevile wakaanza kutoa na umeme serikali iliporuhusu wawekezaji baada ya mitambo ya IPTL kuwa na bei ya juu sana
Hivyo ni kampuni tofauti acha uzushi
 
Back
Top Bottom