Naomba kutoa somo kidogo pale mwili unapotengana na roho

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,582
Kuna shughuli inaendelea ya kumuaga aliyekuwa rais wetu.

Mungu kila nyakati hutuma Wadhihirishaji wa neno lake duniani kuja kuwaongoza wanadamu ili wamjue Yeye na kumuabudu Yeye. Kila Mdhihirishaji huja kwa wakati wake kulingana na mahitaji ya binadamu kwa wakati husika, ndio maana huwezi kukuta hawa wadhihirishaji wamekuja kwa wakati mmoja.

Kwa mfano alikuja Ibrahim kwa wakati wake, alikuja Zoaroster kwa wakati wake, alikuja Buddha kwa wakati wake, alikuja Krishna kwa wakati wake, alikuja Musa kwa wakati wake, alikuja Yesu kwa wakati wake, alikuja Mohammad kwa wakati wake, alikuja Bab kwa wakati wake na sasa amekuja Baha'u'llah kwa wakati wake.

Pia kuna wadhihirishaji hata huku afrika walikuja kwa nyakati zao. Just because hakuna kitabu chochote kuhusu wadhihirishaji kutokea Afrika haimaanisha Afrika haijawahi kuwa na mitume au manabii. Hawa wote walitumwa na Mungu kuja kuwaongoza wanadamu na mafundisho yao yanalenga na ni relevant kwa watu wa kipindi (zama) husika.

Turudi kwenye mada husika ya kichwa cha habari.
Roho ya binadamu inapotengana na mwili (kifo) huanza safari ya kuelekea kwenye malimwengu mengine ya mwenyezi Mungu. Malimwengu mengine ni kama ulimwengu wa mtoto anapokuwa ndani ya tumbo la mama ake. Anapozaliwa anakuwa ameachana na ulimwengu wa tumboni na anaingia kwenye huu mwingine mmojawapo wa malimwengu ya Mungu.

Mtoto anapozaliwa analia sana kwa sababu ametoka kwenye ulimwengu aliouzoea na ameingia kwenye ulimwengu mwingine ambao haujui. Ndio maana hujawahi kumsikia mtoto akilia akiwa tumboni mwa mama ake japo uwezo wa kulia alikuwa nao na hii ya uwezo wa kulia akiwa tumboni inadhihirishwa na kitendo cha mtoto kulia punde tu anapozaliwa.

Roho inapotengana na mwili, roho hupata tabu sana kuachana na mpendwa wake (mwili). Ni sawa na ndege na kiota chake. Kiota cha ndege kikiharibiwa ndege hupata wakati mgumu sana kuondoka yale maeneo pale kulipokuwa na kiota chake. Japo kiota kimeshaharibiwa lakini ndege huzunguka hapo hapo kwa muda kabla ya kuondoka moja kwa moja na kwenda kutafuta sehemu nyingine ya kutengeneza kiota kingine.

Ndege ataendelea kurudi kwenye hiyo sehemu pale kilipokuwepo kiota ili kupata faraja ya ile sehemu yalipokuwa makazi yake. Mfano huu unafanana na mazingira pale roho ya binadamu inapoachana na mwili. Maandiko ya wadhihirishaji wa Mungu wameliongelea hili. Mwili wa binadamu haupaswi kuzikwa mbali na pale marehemu alipofariki wala hautakiwi kusafirishwa kwa umbali mrefu maana roho yake itakuwa inateseka kukitafuta kiota chake kabla haijakata shauri la kuondoka na kwenda kutafuta kiota kipya.

Roho ya marehemu kabla haijazoea ile hali ya kutengana na mpendwa wake (mwili) na kabla haijaanza kusafiri kuelekea kwenye malimwengu mengine ya Mwenyezi Mungu huwa inazunguka kwenye mwili na kutaka kuendelea kuwepo karibu na mwili, hivyo mwili wa marehemu unaposafirishwa mbali kutoka eneo marehemu alipofarikia roho hupata tabu sana kwa sababu mpendwa wake amekuwa ameondolewa ile sehemu ambayo ingempata na kuendelea kufarijika kumuona.

Haya ni mambo ya imani jamani, naomba msianze kunirarua. Haya ni mambo ya imani na yeyote mwenye imani tofauti na hii yupo sahihi pia.
 
Mkuu vp kuhusu malaika mtoa roho akisha toa roho ya mja anaiacha hapo mwili ulipofika au malaika huondoka na hiyo roho??
 
Back
Top Bottom