Naomba kutoa somo kidogo pale mwili unapotengana na roho

Kama anazungukwa na maji anapumuaje?

Maana tunapofanya Ultrasound these days tunasikia mpaka mapigo ya moyo kwa sauti ya juu, moyo unapiga vipi kama havuti pumzi?

Anapumua vipi kama amezungukwa na maji?

Kingine wale walioishawahi kubeba Mimba (wanawake) wanaelewa kwamba kuna miezi ikifika unaweza kuzungumza na kiumbe wako aliyepo tumboni na akarespond (kushika Tumbo kwa mkono wa kuume na kuongea)

Hii yote inawezekana vipi?

Jurjani
Naam, nimeitikia wito.
 
Daah aya mambo ya roho na mwili haya kila mtu ana lake.
Anaejua naomba anijibu hili kulingana na imani yake.

Kuna dhana kwamba mtu akifa roho yake inaenda eidha kuzimu au peponi. Lakini pia kwenye hizi hizi dini zetu mbili kubwa hapa nchini kuna dhana kwamba Issa(sijui kama nineandika sawa) ambae kwa upande mwingine ni Yesu atarudi duniani na kuwatenga wema na waovu kulingana na matendo ya kila mmoja.

Sasa je hizo mtu akifa roho yake inaenda huko kuzimu au peponi ama inamsubili masihi mpaka arudi. Na kama zinaenda uko kuzimu au peponi si inakua ni hukumu tayari sasa huyu masihi anapokuja anawatenga tena kulingana na matendo yao ilhali roho ya mtu ilijitenga tayari wakati amekufa.

Na je uko kuzimu kuna mateso??
Kwanini kuwe na mateso wakati hukumu bado??
Na ni nani anaeamuru huyu aende huku huyu kule ilhali hukumu ya wote bado??
 
Back
Top Bottom