Naomba Kutoa Hoja, Bunge la katiba livunjwe

bunge linahitaji semina zaidi na kikubwa lazima mariano yawepo
 
Kama wazee wanapima vijana kwa kipimo walichopimiwa wao then kiwango kimeshuka, kama vijana wanaopata elimu wanaona wenyewe kuwa inawasaidia then hakijashuka.

Japo si mzee wala kijana najua kuwa watu wanakuwa wabinafsi zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Asipotokea mtu wa kureverse hii (hopefully JK) tunaishia pabaya very soon.

Tatizo la elimu kama lipo kwa nini halishughulikiwi? Ina maana hakuna wataalamu? Mbona kila siku wanasomeshwa?

Tunasomesha wataalamu wengi sana hatutakiwi kuwa na sector isiyokuwa na wataalamu WA KUSOLVE PROBLEMS. Sio kuandika mada.

Ni aibu kuzuzungumzia hili jambo miaka nenda rudi.

Let us do it, find a solution and stick to it.

Sasa mh mjumbe, tatizo lililopo ni kwamba tangu awali hawa wajumbe malengo yao hayakuwa ktk kutaka katiba itakayokidhi mahitaji ya watanzania, walianza na posho na sasa wanataka na siku ziongezeke, kila siku ni malumbano ktk jambo rahisi kulitatua, unadhani semina wanazopewa haziwasaidii kupunguza malumbano yasiyo na tija pale bungeni?
 
Kuna viwatu vya kutowa kama sendeka lusinde basi

Nakuunga mkono mjumbe Ole Sendeka atolewe, ni mtu mzima ila hana busara.
Ni mbishi anajifanya kila kitu anakijua, anaboa hajijui tu, bora leo alivyopewa makavu live.
 
siungi mkono hoja yako mleta mada. bunge lisivunjwe hadi tushuhudie ngumi zikitembea mjengoni. siku hiyo imekaribia sana

Leo ilikuwa almanusra na ngumi zipo njiani tuvute subira wajumbe.
 
Mimi nadhani sasa ni wakati muafaka wa kuwapima akili viongozi wa nchi hii, kuna uwezekano mkubwa wanaumwa.Haiwezekani wawe tofauti na jamii kila wakati,mfano wananchi wanasema laki tatu kwa siku ni nyingi wao wanasema ni ndogo,kama sio ugonjwa ni nini?
 
Mh Mwenyekiti wa muda wa bunge la katiba,nikiwa kama mjumbe wa bunge la katiba kupitia Jamii Forums,naomba kutoa hoja kwamba BUNGE LA KATIBA LIVUNJWE na Mh Rais atoe ridhaa kwa wananchi kuipigia kura rasimu hii ya pili ya katiba.
kwani inavyo onekana sasa kupitia bunge hili la katiba hatutaweza kupata kile tulichokuwa tukikitaraji.
Mh Mwenyekiti Naomba kutoa Hoja.


Mh mtoa hoja, kuvunjwa haitatutendea haki wananchi bali kitu kinachotakiwa Bwana Pandu atumie madaraka alopewa kuwaadhibu wote wasiofuata utaratibu. Pia atoe nafasi hata kwa wajumbe wengine waongee sio kila siku ni Sendeka na wenzake. Cha msingi ajue kuwatumia wajumbe wote 600 na ushee waliopo bungeni.
 
Mh mtoa hoja, kuvunjwa haitatutendea haki wananchi bali kitu kinachotakiwa Bwana Pandu atumie madaraka alopewa kuwaadhibu wote wasiofuata utaratibu. Pia atoe nafasi hata kwa wajumbe wengine waongee sio kila siku ni Sendeka na wenzake. Cha msingi ajue kuwatumia wajumbe wote 600 na ushee waliopo bungeni.

hata kama Mh mwenyekiti atafuata kanuni,taratibu na sheria za bunge la katiba naona bado kutakuwa na migogoro ya kutengenezwa ili tu kuongeza siku za kuishi Idodomea.nadhani unajionea mwenyewe mambo yanavyokwenda
 
Back
Top Bottom