Naomba kutafsiriwa ndoto hii

Lis

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
471
345
Habari, leo nimeamka Sina amani, nimeota ndoto ya kwamba, nimeenda kwa mpenzi wangu nikamkuta rafiki yake ambae simfahamu, lakini akanambia ninaemtafuta ametoka hivyo nimsubirie.

Nikamsubiri kwa muda mrefu bila mafanikio, ila chakushangaza huyo rafiki yake akawa anamtaja katika maongezi kwa jina la kiislam wakati namjua Kama ni mkristo.

Ndoto hi imeniwazisha sana nikawaza yawezekana huyo mpenzi wangu kanidanganya jina au nini?

Pia kiuhalisia Kuna siku nilishaenda kwake nikamkuta rafiki yake aliyesomanae akamuita kwa jina pia tofauti na ninalomtambua nilipomuuliza baadae akanambia Ni jina alilokuwa anatumia shule.

Yaani jimeamka nimekosa imani na mahusiano yangu namuona jamaa Kama msanii flani kutokana nandoto nloota huwenda mungu ananijulisha kitu.jamaa Niko nae kwa mahusiano kwa. Miezi mitano Sasa, tafadhal yeyote anayewezaa kutafsiri ndoto anisaidie tafadhali.
 
Toa tongotongo

Mpaka unajikuta unaliota usingizini?

Kuna mengi ya kufanya
 
Hivi kuna siku ulishawahi kuota umeokota pesa ukiwa usingizini?

Je uilipoamka zilikuwapo?

Hizo ni ndoto tu Mkuu,, ila usimwamini mpnz wako ktk mahusiano kwa 90%.

Mapenzi ni kamari...
 
Mbona mm sikufikiria kuhusiana na nilichoota?

Brain ishakamata ilo tukio la siku ambayo rafiki ya mpenzi wako alipomuita kwa jina jingine hata kama haujaliwaza basi copy yake ipo na imewekwa kwenye brain ndio maana unaweza kukumbuka na kuandika hapa.
 
Jina Ni tofauti na alonambia,
Basi unaliwa kichwa, kuna bibie fulani tulipokuwa tunasoma jamaa yake alimjua kwa jina la Mark, siku yule jamaa kaingia room kwetu na bibie yupo kuna bint karopoka Mathew upo kitambo toka Zenji ujue. Jamaa alipowa vibaya.Kumbe alimdanganya bibie hadi home na mengine mengi.
 
Mwanasaikolojia Mmoja Nguli tu aliwahi kuniambia kuwa nikitaka niishi kwa amani na ayema na Mpenzi wangu basi nihisi kuwa huwa ananisaliti.
 
Wanasema kwamba ukiota ndoto Ni kwamba unajulishwa Jambo lijalo, lililopo na linalokuja, hivyo ndoto Ni halisi.sijui Kuna ukweli hapa
 
Usihofu banah, dini haioi bali ni moyo wa mtu ndiyo unaopenda ba kufikia hatua ya ndoa, dini haiwezi kuwa kikwazo kikubwa sana mkashindwa kuingia kwenye ndoa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom