Naomba kusaidiwa haya kuhusu Online TV

May 13, 2020
5
3
Ndugu zangu naomba msaada:
1. Jinsi ya kufungua online TV
2. Jinsi ya kupata pesa kupitia Online TV
3. Ni aina gani ya vifaa vizuri vya kutumia na wingi wake.
4. Ni aina gani ya watu wakuendesha hii kazi na wingi wake
5. Maudhui yangu kufungua online TV ni kuitangaza moja ya Tasnia hapa nchini lakini mchanganyiko na habari zengine jamii kwa ujumla

Mwenye msaada wa dhati kabisa naomba kusaidiwa.
 
Ndugu zangu naomba msada
1 .jinsi ya kufungua online TV
Ukiwa na e-mail ya gmail, sign in kwenye youtube akaunt, kama unatumia kompyuta bonyeza upande wa juu wa kulia kwenye icon ya e-mail kuna option ya kutengeneza channel
2. Jinsi ya kupata pesa kupitia online TV
Hela inapatikana kwa njia ya matangazo, kwa channel nyingi wanategemea matngazo ya google adsense(kuna vigezo vinahitajika hapa)
3. Ni aina gani ya vifaa vizuri vya kutumia na wingi wake.
Inategemea na aina ya contents ya niche yako, kwa mfano channel yako inazungumzia games za mpira za android hapa simu yako inaweza kuwa inatosha, na app ya screen recording labda na video editing software kama adobe premiere.
4. Ni aina gani ya watu wakuendesha hii kaz na wingi wake
Hapa Unamaanisha nini? ila mtu yoyote anaweza endesha, unaweza kuwa channel inafundisha jinsi ya kupiga mswaki vizuri na ukapata audience
5.maudhui yangu kufungua online TV ni kuitangaza moja ya Tasnia hapa nchini lakin mchanganyiko na habari zengine jamii kwa ujumla mwenye msaada wa dhat kabisa naomba kusaidiwa.
Kuwa specific usijaribu kucover kila kitu, ila youtube sio rahisi kiivyo inahitaji muda tena kama channel mpya na wewe sio maarufu sahau kuhusu pesa kwa mwaka wa kwanza na ujikite kuikuza channel yako.
 
Daaa nashukuru sanaa kiongozi tena sanaa namba 4 nilikua naamanisha wataalamu kwamba wa habari yani staki niwe na ilimradi chanel nataka iwe bora na ya kuaminika
 
Ukiwa na e-mail ya gmail, sign in kwenye youtube akaunt, kama unatumia kompyuta bonyeza upande wa juu wa kulia kwenye icon ya e-mail kuna option ya kutengeneza channel

Hela inapatikana kwa njia ya matangazo, kwa channel nyingi wanategemea matngazo ya google adsense(kuna vigezo vinahitajika hapa)

Inategemea na aina ya contents ya niche yako, kwa mfano channel yako inazungumzia games za mpira za android hapa simu yako inaweza kuwa inatosha, na app ya screen recording labda na video editing software kama adobe premiere.

Hapa Unamaanisha nini? ila mtu yoyote anaweza endesha, unaweza kuwa channel inafundisha jinsi ya kupiga mswaki vizuri na ukapata audience

Kuwa specific usijaribu kucover kila kitu, ila youtube sio rahisi kiivyo inahitaji muda tena kama channel mpya na wewe sio maarufu sahau kuhusu pesa kwa mwaka wa kwanza na ujikite kuikuza channel yako.

Mimi nlivoona anaulza tu njia ya kupiga ela nkajua tayar youtube itamshinda
 
* Naamini unataka kuanzisha ONLINE TV na sio YOUTUBE CHANNEL.

Ila kama unataka kuanzisha Youtube Channel, ni rahisi;

1. JINSI YA KUFUNGUA: Sign up kwa kutumia barua pepe yako ya Gmail.
*Kisha kalipie leseni TCRA.
2. JINSI YA KUPATA PESA:
  • ADSENSE: Unahitaji kuwa na subscribers 1,000 na view time ya masaa 4,000 ndani ya miezi12 kabla hawakuwezesha ku-monetize video zako.
  • UZA BIDHAA, 'MERCHANDISE' na HUDUMA.

    Wasome watazamaji wako wanataka nini na kisha wauzie kitu cha thamani kwao.
  • FANYA AFFILIATE MARKETING.
  • INGIA DEALS NA BRANDS KUBWA NA SPONSORSHIPS.
  • CROWDFUNDING n.k
3. VIFAA: Camera HD, mic, Lighting system, na software za ku-edit video & picha.
4. WATU: Unahitaji watu kukusaidia kurekodi video, ku-edit na ku-manage mitandao ya kijamii kama huwezi kuvifanya hivi vitu wewe mwenyewe.
5. MAUDHUI: Kuna chaneli nyingi sana hivi sasa - unahitaji kuwa mbunifu sana ili kuwavutia watazamaji.

Lakini kama unataka kuanzisha online TV;

NAMNA YA KUANZISHA INTERNET/ ONLINE TV.
*Assuming kwamba una mtaji mdogo na kwahiyo utaanza ukiwa jeshi la mtu mmoja. Na si lazima ufuate mfululizo kama nilioupanga mimi.

HATUA YA 0: Kwa 'heshima na taazima'(Taadhima) nenda kawaone TCRA kwanza.
Mjanja huwa anatatua matatizo, mwenye busara huwa anayaepuka matatizo. Unataka mjanja au mwenye busara? Ukifika kwa hawa jamaa waambie kusudio lako la kuanzisha Online TV - watakupa muongozo rasmi, vigezo na masharti. Labda kama wewe huishi hapa kwetu, Tanzania.

HATUA YA 1: Liweke vizuri wazo lako ili ujue wapi unakotaka kuelekea.
Utajuaje kama umeliweka vizuri? Well, kama huwezi kulielezea kwa sentensi moja au mbili likaeleweka basi bado hujajua unachokitaka. Jiulize maswali haya;
  • Unataka kupata nini kutokana na hiyo online TV yako?
  • Ni maudhui gani unataka kuyatoa?
  • Yapi yatakiwa masaa yako ya kazi?
  • Ni wakati gani utakuwa live na muda gani utarusha vipindi ambavyo ni pre-recorded?
  • Tengeneza ratiba ya matukio na topics.
HATUA YA 2: Nunua domain.
Nashauri ununue 'domain name' mahsusi kwaajili ya online TV tu. Domain za 'Dot TV (.tv)' zimekuwa maarufu sana kwa masuala ya TV. Lakini; unachotakiwa kufahamu ni kuwa .tv haiwakilishi 'television'. Kiuhalisia .tv ni extension ya Tuvalu, taifa lililopo katika visiwa vya Polynesia.

HATUA YA 3: Ajiri watu - tengeneza timu kwaajili ya ku-design na ku-code website.
  • Inatakiwa kuwa kama website zingine. Utofauti ni kuwa; katikati ya website weka TV kubwa inayo-stream video au matangazo mubashara (live).
  • Weka sehemu za matangazo ya wadhamini wako.
  • Weka sehemu ambayo watazamaji wako wanaweza ku-browse bidhaa na huduma zako, kufahamu zaidi kuhusu wewe, kuwasiliana na wewe na vitu vingine vya namna hiyo.
  • Hakikisha una-update website yako mara kwa mara ili kubadilisha matangazo n.k.
HATUA YA 4: Tengeneza eneo la kurekodia.
Naamini utakuwa unafanya vipindi aina zote; yaani pre-recorded na live videos, kwahiyo ni muhimu ukawa na sehemu maalumu ya kurekodia ambayo imepambwa inavyotatikana na ina vifaa vyote muhimu kwaajili ya kuhakikisha video zako zinakuwa na ubora.

HATUA YA 5: Nunua vifaa kwaajili ya video recording video na live broadcasting.
Unaweza kupata hivi vifaa vyote kwa chini ya TZS 5,000,000/=
  • HD camera ni lazima.
  • Vifaa vya audio: microphone, headphone, 'clipped microphone', au unaweza kuamua ukanunua vyote 'wireless'.
  • Vifaa kwaajili ya lighting: Chagua vifaa bora kwa utashi wako.
  • 'Green screens'. (Hizi zinasaidia kurahisisha kazi ya ku-edit video na picha za kawaida.)
  • 'Teleprompter'; Hii utaihitaji ikiwa tu utataka kuendesha vipindi vyako kwa kutumia 'script'.
  • Unganisha camera yako na computer yako, na jiandae kwenda live!... Camera -check ,.... lights - check.... voice - check.... tunaenda hewani baada ya sekunde 5 - 4 - 3 - 2 -..
HATUA YA 6: Tafuta host mzuri wa website yako ambae anaweza ku-handle bandwidth na video streaming mfululizo.
*Kama wapo humu watajitokeza, au la tafuta mtandaoni utawapata.

HATUA YA 7: Anza kurekodi videos ambazo utaziweka katika station yako.
Si lazima uwe na video nyingi au ndefu ili uanze. Unaweza kuanza na video moja au mbili - cha muhimu ni kuanza. Fuata muongozo uliojiandalia wewe mwenyewe kuhusu maudhui utakayoyatoa ukiwa live na yale utakayorekodi.

HATUA YA 8: Kumbuka si lazima uwe na maudhui ya kutosha kuruka 24/7.
  • Unaweza ukapiga masaa manne ya maudhui ambayo ni pre-recorded kila siku, masaa mawili ya kwenda live na matangazo unachanganya humo humo.
  • Rudia hayo maudhui yaliyoruka live kwa masaa sita.
  • Masaa mengine 12 yaliyobaki kuwa mbunifu - weka mziki au chochote unachoona kinawafaa watazamaji wako.
Si nyakati zote utapata watazamaji wa kutosha. Hivyo ni vizuri kujua 'peak hours' zako. Hakuna haja ya kurusha kipindi endapo huna watazamaji.

HATUA YA 9: Host baadhi ya matukio live.
Live events ni njia nzuri ya kuvutia watazamaji. Utofauti ni kuwa utakuwa una-host tukio kwenye website yako mwenyewe.

HATUA YA 10: Promote chaneli yako kila mahali.
Na ninaposema kila mahali, namaanisha kila mahali.
  • Weka link kwenye Website, kwenye mitandao ya kijamii mpaka kwenye sms za watu ukiweza!
  • Toa 'taarifa kwa vyombo vya habari' za kutosha. Kuwa msumbufu, acha masihara!
  • Fanya 'partnership' na watu wengine kwa malipo ya 'free advertising'.
HATUA YA 11: Teka mji, kuwa mfalme wa online TV!
Kadiri TV yako inavyozidi kuwa maarufu - anza kuongeza tuvitu vitu na fursa za kupiga hela;
  • Matangazo (Paid advertising).
  • Manbango kwenye website yako.
  • Tangaza bidhaa na huduma zako mwenyewe.
  • Andaa maudhui yaliyodhaminiwa (Sponsored contents).
  • Usiogope - ita watu wazito kwenye interviews zako. Nani ajuaye, labda unaweza kuja kuwa Salama Jabir au Milard Ayo ajaye!
Kisha anza kuajiri kadiri ya mahitaji yako; endapo unahitaji foot soldiers wa kuwinda matukio mtaani au unataka co-hosts, au unataka timu ya production, au unataka social media managers, au unataka script writers, au unataka 'wahariri', au unataka business managers n.k. Angalau ifahamike kuwa idadi ya watu na aina ya watu unaowahitaji inategemea na malengo, mahitaji halisi na bajeti yako.

Ruksa kunikosoa. Naomba kuwasilisha.
 
Hivi ukitaka kureply itokee hivi unafanyaje?!
 
Nimekuelewa bro nina swali kuhusu youtube channel
Me nimdau wa kuangalia mambo mbali mbali youtube kuna option ya ku upload video, je niki upload video hiyo itakuwa ni channel teyali au kunakingine chakufanya?

Je na nikitimiza vigezo kuwa na subscribers 1000 na 4000 hrs na sijafika 12 months inakuaje hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother computer virus hakika nayachukua hayaa kabisa na siku nitakutafuta ndugu na Kama waweza nitumia mawasiliano sio mbaya nina ndoto kubwa ya acha alama kwenye Tasnia yangu kuitangaza Brodher salute sanaa.
 
Shukrani sana mkuu, umefafanua kwa kadiri ulivyoweza, asante kwa muda wako, najua umewasaidia wengi pa kuanzia.
 
Ukiwa na e-mail ya gmail, sign in kwenye youtube akaunt, kama unatumia kompyuta bonyeza upande wa juu wa kulia kwenye icon ya e-mail kuna option ya kutengeneza channel

Hela inapatikana kwa njia ya matangazo, kwa channel nyingi wanategemea matngazo ya google adsense(kuna vigezo vinahitajika hapa)

Inategemea na aina ya contents ya niche yako, kwa mfano channel yako inazungumzia games za mpira za android hapa simu yako inaweza kuwa inatosha, na app ya screen recording labda na video editing software kama adobe premiere.

Hapa Unamaanisha nini? ila mtu yoyote anaweza endesha, unaweza kuwa channel inafundisha jinsi ya kupiga mswaki vizuri na ukapata audience

Kuwa specific usijaribu kucover kila kitu, ila youtube sio rahisi kiivyo inahitaji muda tena kama channel mpya na wewe sio maarufu sahau kuhusu pesa kwa mwaka wa kwanza na ujikite kuikuza channel yako.
Nakubal San mkuu nmepat kaulew na mm umo
 
Back
Top Bottom