Naomba kupata utaratibu na viambatanisho vya kupata PASSPORT

Mr Confidential

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,090
2,000
Habari Great Thinkers!

Wiki hii nimejaza fomu kwenye website ya Uhamiaji. Nini natakiwa kufanya baada ya hapo?

Viambatanisho gani natakiwa kuwa navyo tofauti na walivyoorodhesha kwenye website yao?

Natakiwa kusubiri wanipigie simu au niende mwenyewe? Na deadline ni mda gani baada ya kujaza fomu na kulipa ile 20,000.?

Kuna haja ya lawyer? Au cheti cha kuzaliwa kipitie Rita?

Naomba msaada wenu tafadhali maana nimeshajaza fomu na kulipia
lakini sijui ni hatua gani inafuata.

Naomba kuwasilisha

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
22,700
2,000
Kitambulisho cha NIDA, cheti cha kuzaliwa chako na cha wazazi wako, barua ya mtendaji mtaani kwenu, invitation letter

Hivi vitu ni lazima uwe navyo, kimoja kikikosekana hupati PASSPORT
 
Invitation letter sina. Nimeandika naenda Kenya kutembea. Watataka nini hapo?
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,909
2,000
Ngoja wakupe karatasi la wiki mbili au mwezi...
Hahahahaaaa.... hii iliwahi kunikuta mwaka 2016, nilikua disappointed sana. Naona jamaa yetu hiki kitu kinaenda kumkuta.
Kwa uzoefu wangu kwenye haya maombo ya kuomba passport, sababu ya ndugu yetu hapo juu (kwenda Kenya kutembea) ni sababu ''nyepesi mno'' mbele ya watu wa ''uhamiaji yetu'' kumpatia hati ya kusafiria (kile kitabu).
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,909
2,000
Invitation letter sina. Nimeandika naenda Kenya kutembea. Watataka nini hapo?
Umeshalipia ile elfu 20 tayari ?
Kama tayari, basi unatakiwa (kwa maoni yangu) kuwa tayari kuipoteza (kuiacha iende zake) na kuanza maombi upya wakati ukiwa na ''a concrete reason'' ya kuomba nyaraka hiyo.

Ifahamike waze kwamba watu wa uhamiaji wanachukulia ''siriaz mno'' hili suala (pengine kuliko ambavyo ilipaswa kuwa).

Ngoja nije PM nione kama kuna namna ambayo naweza kukusaidia kutengeneza GOOD REASONS za kuwaaminisha hawa jamaa kwa unamaanisha kuitaka nyaraka hiyo.

NB: Natambua kwamba mambo ya PM yanaweza kuambatana na masuala ya utapeli, lakini kuna mambo kadhaa ambayo natakiwa kukuuliza hivyo siwezi kufanyia ''hapa hadharani'' (ninalinda privacy yako).

Pili, natambua kwamba kinachofanyika PM (kama ni chema) kinanyima fursa kwa hadhira kubwa kunufaika nacho. Hili litapatiwa ufumbuzi hapo mbeleni, kwa leo tuanze nawewe.
 
Unazunguka sana na mambo ya PM si useme kuwa we ni KISHOKA

Bongo mmmh
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,909
2,000
Ina maana mwananchi hawezi kukata passport akawa nayo tuu kabatini au mpaka asafiri?

Anaweza na hilo linapaswa kuwa jambo la kawaida sana.
Ni vile idara yetu ya uhamiaji ''inayakuza mambo''
Kwa dunia ya sasa, hasa kwa mtu mtafutaji, unaweza kupata safari muda wowote ule. Sio sawa kwamba unatakiwa kupata safari kwanza ndipo upate passport.
Hii imekaa kijima sana.

Mimi ninaamini kwamba kuwa na passport na kuitumia passport hiyo vizuri au vibaya ni MAMBO MAWILI TOFAUTI.

Hakuna guarentee kwamba watu wakiipata kwa ugumu (kwa mbinde) ndio wataitumia vizuri.
 
Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,820
2,000
Na ndicho kinachenda kutokea, pale migration hawana masihara hata kidogo
Wakati nipo mwaka wa pili nilikutana na hivyo vitu katika kujaza yale makaratasi, sasa nikabidi kugugo taarifa mbalimbali kwa watanzania wanao tafuta pass...

Na kuuliza walio pata pia, mwisho una ng'amua vile waweza fanya, nakumbuka ilinibidi nijaze nchi za nje ya Africa nikasema pia hapa nikitaka kujaza nchi zote duniani itakuwa shida hakutoshi, nikajaza EU countries na kizungu cha kubangaiza, American Countries (ni mwendo wa kujumisha manchi na Asian countries....

Hii sababu ilikuwa kwenda kusoma alafu ukizingatia ni mwanafunzi, nikaenda kwa Dean wa school akanipa barua ya utambulisho... Nilikusanya viambata vyote..

Sababu yangu ni kwenda kusoma hivyo vyeti vyangu vya elimu viliitajika kama viambata muhimu, cheti cha kuzaliwa mzazi sina, na nilikuwa nafanya mzazi hajui lolote, nikaenda mahakamani kuomba affdvt ya kuzaliwa mzazi, nikajaza taarifa zake na kulipia, nikaambatanisha....

Baada ya kukusanya vyote, nikabidi nitafute chuo ambacho nitapata invitation or sijui barua ya udaili wa awali etc... Kuna vyuo wana toa hawana shida hata kama haina hizi nyaraka za kusafiria...

Nikaambatanisha nikapeleka wakazipokea, nikaambiwa baada ya mwezi ila kqmq una haraka basi jiongeze, nikasema nitarejea kwasasa sijabeba pesa ya kutosha kumbe fix sina kitu, hivyo Mimi ilikuwa kupata document tu ya kusafiria na kwa sababu nilikuwa bado nasoma haikuwa na haraka sana....

Hatimae nipo skuli baada ya kipindi napigiwa simu nifike uhamiaji kuchukua hati yangu, nikqkaa tena kama mwezi ndio nikaenda kuifata, sikuwa na haraka sana halafu nilikuwa najipanga sana kutoa sababu za kueleweka na kujifanya msomi kweli kweli kumbe hmna kitu wakawaida tu ila napenda kujifunza vingi na kujua mengi muhimu

Na baada ya zoezi hili ya ubadiliahaji hizi hati, napo halikuwa jambo gumu, niliwasiliana na rafiki wengi tu, SA, China, USA, EU nikapata mialiko ya sikukuu za mwisho wa mwaka na mwaka mpya, nikaambatanisha zote... Nikawqambia nitachagua Mimi wapi pa kwenda au kuanza napo hivyo msiwaze...

Muda mwingine una takiwa kujiamini kupita kiasi, na kucheza na mind ya mwenzio... Soma mind yake ana elekea wapi? Una pamudu au shida?

Una weza kuwa umepata kitu mleta mada, pambana, anza kwa kujenga urafiki na wageni toka nje, au ndg, jamaa na mqrafiki kama unao, waeleze dhumuni lako

Wengine huwa wana foji barua, ila sijasema utumie njia hii... Sijasema utumie njia hii, ila wapi wanao Foji na niwengi tu...
 
Mr Confidential

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,090
2,000
Hahahahaaaa.... hii iliwahi kunikuta mwaka 2016, nilikua disappointed sana. Naona jamaa yetu hiki kitu kinaenda kumkuta.
Kwa uzoefu wangu kwenye haya maombo ya kuomba passport, sababu ya ndugu yetu hapo juu (kwenda Kenya kutembea) ni sababu ''nyepesi mno'' mbele ya watu wa ''uhamiaji yetu'' kumpatia hati ya kusafiria (kile kitabu).
Daaah. Hadi utoe Mlungula??
 
Mr Confidential

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,090
2,000
Umeshalipia ile elfu 20 tayari ?
Kama tayari, basi unatakiwa (kwa maoni yangu) kuwa tayari kuipoteza (kuiacha iende zake) na kuanza maombi upya wakati ukiwa na ''a concrete reason'' ya kuomba nyaraka hiyo.

Ifahamike waze kwamba watu wa uhamiaji wanachukulia ''siriaz mno'' hili suala (pengine kuliko ambavyo ilipaswa kuwa).

Ngoja nije PM nione kama kuna namna ambayo naweza kukusaidia kutengeneza GOOD REASONS za kuwaaminisha hawa jamaa kwa unamaanisha kuitaka nyaraka hiyo.

NB: Natambua kwamba mambo ya PM yanaweza kuambatana na masuala ya utapeli, lakini kuna mambo kadhaa ambayo natakiwa kukuuliza hivyo siwezi kufanyia ''hapa hadharani'' (ninalinda privacy yako).

Pili, natambua kwamba kinachofanyika PM (kama ni chema) kinanyima fursa kwa hadhira kubwa kunufaika nacho. Hili litapatiwa ufumbuzi hapo mbeleni, kwa leo tuanze nawewe.
Tayari nimekuPM
 
warumi

JF-Expert Member
May 6, 2013
16,282
2,000
Invitation letter sina. Nimeandika naenda Kenya kutembea. Watataka nini hapo?

Labda useme unapeleka gari na uambatanishe na leseni ya udereva.. all in all ni kujiamini kwako tu ndo kutakufanya upewe passport kama ukiwa na kila kitu halafu hueleweki maelezo unajikanyaga hwakupi passport , unatakiwa ujiamini uwe na maelezo yanayoeleweka
 
Jimena

JF-Expert Member
Jun 10, 2015
25,383
2,000
Habari Great Thinkers!

Wiki hii nimejaza fomu kwenye website ya Uhamiaji. Nini natakiwa kufanya baada ya hapo?

Viambatanisho gani natakiwa kuwa navyo tofauti na walivyoorodhesha kwenye website yao?

Natakiwa kusubiri wanipigie simu au niende mwenyewe? Na deadline ni mda gani baada ya kujaza fomu na kulipa ile 20,000.?

Kuna haja ya lawyer? Au cheti cha kuzaliwa kipitie Rita?

Naomba msaada wenu tafadhali maana nimeshajaza fomu na kulipia
lakini sijui ni hatua gani inafuata.

Naomba kuwasilisha

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
Mbona hiyo fomu unayosema umejaza huwa ina maelezo yote??
Hivyo viambatanishi vinategemea na mwombaji husika, ila kuna yale ya kawaida tu ambayo yapo kwa kila mtu,
Kwani hujaona kipengele cha kuattach documents kama barua ya serikali yako mtaa,
Cheti cha kuzaliwa chako na mmoja wa wazazi wako, kitambulisho cha taifa,

Viambatanishi vingine inategemea na aina ya safari unayoenda, ikiwa ni kwa ajili ya matibabu watakwambia vitu vinavyohitajika, kama ni kutembea watakwambia doc za kuambatanisha na kama ni kimasomo pia watakwambia uambatanishe nini na nini,

Baada ya hapo hizo documents zote ulizoambatanisha wakati wa kujaza fomu ya maombi na zingine ambazo utatakiwa kwenda nazo, toa copy zoote kisha peleka kwa mwanasheria au mahakamani, wataverify hizo nakala kisha kuna mahali kwenye hiyo fomu atakujazia kisha atakugongea mhuri na kubandika stamp, baada ya hapo ndio unaenda sasa kwa ajili ya picha na alama za vidole ukiwa na fedha za kulipia yaani ile gharama iliyobakia!
 
warumi

JF-Expert Member
May 6, 2013
16,282
2,000
Na ndicho kinachenda kutokea, pale migration hawana masihara hata kidogo

Pale wanaangalia tu ulivyo vaa, life style yako , unavyojielezea, kuna wengine wakienda tu ku apply na hata hawana document zote wanapewa, wewe kama hueleweki hata uwe na kila kitu hawakupi, wanacheza tu na psychology za watu

Mimi nilienda pale nikajifanya baba angu wazir, nikawa na full confidence mikwara mingi ila wakaninyima, Nikaenda juu nikaonana na mwanasheria nikamganda akasema kesho niende asubuhi, nikaenda akanisaidia na sikumpa hata sh kumi, kujiamini tu kunasaidia pale immigration , kama Uko smart unatengeneza connection na watu pale pale
 
Nakubaliana na wewe! Mi hati yangu ya kwanza kabisa ya kusafiria niliipata bila barua ya mwaliko na sikutoa hata 100,
Kwanza hata maswali sikuulizwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom