Naomba kuongea na wasabato wenzangu: Tunakosea sana

Mubby777

JF-Expert Member
Oct 17, 2018
1,638
5,645
Enzi za wana wa Israeli watu walikuwa wakitenda dhambi wanachukua kondoo safi na kupeleka kwa kuhani wanatubu dhambi zao then kondoo anachinjwa moto kutoka juu unashuka na kuiteketeza hii huashiria sadaka yako imepokeleqa na dhambi zimesameheka

Mtu alikuwa akitenda dhambi ya hadharani esp uzinzi basi hakukuwa na toba alikuwa anaadhibiwa pale pale kwa kupigwa na mawe mpk kufa

Yesu alipokuja duniani tukio kama hilo lilitokea(aliletwa mwanamke mzinzi aliyetenda hadharan na wakamshika na kumpeleka kwa Yesu ili kumpima na Yesu alichora chini kisha akawaamuru asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga mawe yule mwanamke< inasemekana pale chini kila mtu aliposoma aliona dhambi yake imeandikwa we are not sure yet> basi wote wakatawanyika na yule mama akasamehewa dhambi zake)

Yesu alipokuwa msalabani kuna kondoo wa sadaka alikuwa achinjwe but pazia likapasuka na kondoo akakimbia(wakristu tunaichukulia kama ilikuwa ndio mwisho wa kutoa sadaka ya dam ili kusamehewa dhambo zetu kwa sababu dam ya Yesu ilimwagika pale msalabani)

Baada ya ujio wa Yesu Ukristo ukazaliwa na ukawa completely tofaut na Waislaer wa zaman( tukapewa uhuru wa kutubu direct kwa Mungu kupitia Yesu kristo)

Nakuja kwenye point sasa :- Kama yesu alisema asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga yulewanamke na wote wakaondoka maana wote walijua ni wadhambi inaluwaje bado wasabato tunashikilia ule ujinga wa dhambi ya hadharani mti anaadhibiwa hdharani?( ikitokea umezini na ikajulikana basi unafutwa ushirika)

Iv naomba niulize Yesu si alituunganisha na Mungi direct? Kama nimetenda dhambi si napaswa kutubu kwa Mungu wangu? Why wanadam mnasimama sehem ya Mungu na kuhukum? Je nyie mnaomfuta mtu ushirika mnakuwa hamna dhambi? Mnakuwa watakatifu? Kuna tifaut gan kati ya kumfuta mtu ushirika na wale waliokuwa wanapiga mawe?

Wasabato kuna ujinga ukipatwa na dhambi ya hadharan(wamebase kwenye uzinzi tu) unafutwa ushirika na unapaswa ubatizwe tena
Iv kwenye Biblia nan alibatizwa mara ya pili? Iv nikikosea napaswa nitubu kwa Mungu au kwenu? Maana kuniambia nibatizwe tena manake hapo nawaonesha nyie kuwa nimekosea nisameheni nibatize nirud kundini why nyie? Na sio Mungu?

Mimi naona ni makosa makubwa sana kumfuta ushirika mtu kosa ametenda dhambi ya wazi haina tofaut na walivyokuwa wanapiga mawe
Sasa Yesu alikuja wa nini kama bado watu wanahukum?

Mimi ni msabato niliyezaliwa kwenye dini tangu mababu huko na nimekuwa kwenyw misingi kabisa ya dini ila kwenyw hili swala nimepingana na kanisa maana pale kanisan nikiwaangalia sion mtakatifu wote sisi ni wadhambi ni rehema tu ya Mungu iko nasi sasa why tuwe wa kwanza kuhukum wenzetu wakat tumwzuiwa kuhukumu?

Mtu anakukalia koon kisa umefumwa unazim wakat yeye ana michepuko kibao

Mimi 2008 nilikuwa kwenye baraza la kanisa mahali flan huko Mkoa wa Mara jamaa mmoja akaoa sogea tukae wakaita baraza kumfukuza
Aisee niliwacharura sababu wale wazee wote nilikuwa najua michepuko yao" ambaye anajua sijui maovu yake amfute ushirika huyu mtu au ambaye ana mstari wa kwenye biblia unaosema watu wafunge ndoa ya cheti kwa vuongozi wa dini atoe hapa" tulisumbuama but atlast nilishinda na jamaa hakufutwa ushirika na maisha yakaendelea

My advice( em tuache kuwa mahakimu wakat sisi wenyewe si wakamilifu pls)
Mtu akitenda dhambi iwe ya hadharan au ya kujificha mwachen amalizane na Mungi wake mwenywwe
 
Heee nilikuwa silijui hili, kah vipi walevi, waongo, wasengenyaji nao wanafutwa??
 
Kumfuta mtu ushirika haimaanishi kuwa ametengwa au ameachwa na Kanisa, bali ni dhihirisho la wazi kuwa Kanisa haliungani na na dhambi ambayo huyo muumini amefanya. Hata hivyo, baada ya ushirika wake kufutwa, waumini wanatakiwa kuwa karibu zaidi kumsaidia rafiki huyu airejee Toba. Kwa nini kufutwa ushirika?

Hebu fikiri unajitambulisha kama Mkristo lakini ni Mlevi, Mzinzi, Mwizi au Muuza madawa ya kulevya. Unaendelea na utumishi kanisani kujiita wewe ni Mkristo. Hii inachafua picha ya kanisa na kuwafanya wengine waamini kuwa wakristo wapo hivyo.

Kanisa linaposimama na kukemea uovu huo, ni kuuthibitishia ulimwengu kuwa huo uovu uliofanyika kanisa haliungi mkono. Kumbuka kabla ya kubatizwa uliapa kutunza mwenendo WA kikristo, pindi unapoamua kwenda kinyume na kiapo cha ukristo, lazima kanisa lisimame kukemea. Barikiwa rafiki
 
Kumfuta mtu ushirika haimaanishi kuwa ametengwa au ameachwa na Kanisa, bali ni dhihirisho la wazi kuwa Kanisa haliungani na na dhambi ambayo huyo muumini amefanya...
Kwa hiyo dhambi ni moja tu uzinzi
 
Enzi za wana wa Israeli watu walikuwa wakitenda dhambi wanachukua kondoo safi na kupeleka kwa kuhani wanatubu dhambi zao then kondoo anachinjwa moto kutoka juu unashuka...
Mungu hayupo.

Hizi nyingine mnazoziita dini ni jitihada za watu kujibu maswali wasiyoweza kujibu na kutawalana tu.

Ukielewa hili, hayo mengine hayatakusumbua.
 
Hawafuti ushirika kwa dhambi ya uzinzi tu, wanafuta kwa dhambi zingine pia endapo itathibitika kweli mlengwa alimentary hiyo dhambi.

Kwetu kule kuna mtumishi alifutwa ushirika kwa dhambi ya wizi wa zaka na sadaka, yeye alikuwa mhazini mkuu wa kanisa, walipofanya internal audit ikagundilika past na shaka kuwa aliminya pesa za kutosha, akakiri na kusema atarudisha, pamoja na kupewa mda wa kurejesha pesa lakini karipio la mdomo halikutosha, alipigwa pini(kufutwa ushirika) hadi alipoungama na kutiwa majini tena.

Hakuna mkamilifu, ila ni muhimu kufanya hivyo kwa ustawi wa kanisa.
 
Kumfuta mtu ushirika haimaanishi kuwa ametengwa au ameachwa na Kanisa, bali ni dhihirisho la wazi kuwa Kanisa haliungani na na dhambi ambayo huyo muumini amefanya...
Nadhani mleta mada analia na unafiki baina yetu. Ni jambo jema, tena sana kukemea tunapoona mwenzetu anaanguka, lakini tufanyapo hivyo, je, sisi wenyewe ni wasafi?

Hilo ndio analohoji mleta mada. Haitakuwa na maana yoyote tukisimama kukemea wenzetu ilhali sisi wenyewe tu wachafu, na huu ni unafiki mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Tutoe kwanza boriti ndani ya macho yetu, ndipo tutaona na kutoa kibanzi kwenye macho ya wenzetu.
 
Enzi za wana wa Israeli watu walikuwa wakitenda dhambi wanachukua kondoo safi na kupeleka kwa kuhani wanatubu dhambi zao then kondoo anachinjwa moto kutoka juu unashuka na kuiteketeza hii huashiria sadaka yako imepokeleqa na dhambi zimesameheka....
Kufutwa ushirika ni adhabu ambayo ipo kufuatana na dini ya wasabato, na hilo hutakiwi kulihoji kwa sababu lipo kulingana na msingi wa dini husika. Mbali na hilo, muumini anafutwa ushirika (hafukuzwi ushirika) ili ajirekebishe na kupelekea ajirudi na hatimaye arudi tena kwenye misingi inayotakiwa kiroho na kidini pia. Labda hilo jingine la kubatizwa mara ya pili ndiyo linaweza kuwa liko kidini zaidi na si kiroho kwa sababu sidhani kama kuna maandiko matakatifu yanayothibitisha hilo. Unless labda kuna maandiko matakatifu yanayo-support utaratibu huu.

Kikubwa hapa kumbuka kuwa dini ni utaratibu aliojiwekea mwanadamu ili autumie katika mchakato mzima wa kumtafuta Mungu. Kwa hiyo kufutwa ushirika ni utaratibu ulioko kwenye dini hiyo na uko sawa kabisa, provided mtu hajafukuzwa ushirika kanisani. Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi na hivyo hayupo muumini anayeweza kufukuzwa ushrika kanisani kwa sababu ya kutenda dhambi ambazo madhara yake yanaendana na mwenye kutenda dhambi hiyo tu na si vinginevyo.

Still, kuna exceptions ambazo zinaweza kupelekea mtu kufukuzwa ushirika na ambazo lazima ziendane na uvunjaji wa sheria za nchi pia. Utafukuzwa kanisani tu iwapo itathibitika kuwa uwepo wako Kanisani unaendana na ku-compromise maisha ya kiroho ya waumini wengine ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria za nchi kunakoweza kupelekea Kanisa husika kuonekana lina-compromise sheria za nchi, kitendo ambacho kinaweza kupelekea Kanisa hilo kufungiwa na Serikali. Kwenye situations kama hizi lazima mshirika utafukuzwa Kanisani. Usitenganishe sana Dini na Serikali kwenye maslahi ya waumini/ wanachi wao, Dini na Serikali huwa vinafanya kazi kwa ukaribu sana. Ndiyo maama cheti cha ndoa kinaweza kutolewa Kanisani halafu Serikali ikakitambua kuwa ni halali

Kwa upande mwingine, utaratibu aliojiwekea Mungu kumtafuta mwanadamu unaitwa WOKOVU; na hivyo wokovu na dini ni vitu viwili tofauti; wokovu ni mmoja tu kwa watu wote, wakati dini ziko nyingi na tofauti tofauti. Hata hapo ulipo wewe siku hii unaweza ukaamua ukaanzisha dini yako, utakuwa uko sawa kabisa. Kikubwa kabisa na cha msingi kinachotakiwa kuwepo kwenye dini yoyote ile ni kule kuhakikisha kuwa muda wote dini hiyo inamhifadhi muumini kwenye njia ya wokovu kuanzia sasa na hata milele na hivyo kumpelekea auone uzima wa milele!
 
Heee nilikuwa silijui hili, kah vipi walevi, waongo, wasengenyaji nao wanafutwa??
Kwenye biblia kuna zile amri kumi za mwenyezi Mungu. Na tunafundishwa kwamba katika hizo amri kumi hakuna dhambi kubwa na ndogo, kwamba zote zipo sawa. Cha kushangaza kwenye maisha ya wanandoa imetajwa dhambi moja tu ya uzinzi kwamba ndiyo inayoweza kupelekea wanandoa kuachana.

Yaani hata mwanandoa akienda kinyume na amri isemayo usiue na akawa anaua watu kwa makusudi bado mwanandoa mwenzie hapaswi kuachana nae! Yaani dhambi ya kuua mtu kwa makusudi kweli ndiyo ilingane na uzinzi unaoleta furaha kwa wahusika wawili?!

Kuua kulingane na anaesema uongo kwa mfano mtumishi anapomdanganya mwajiri wake kwamba leo hatafika kazini kwa vile anampeleka mwanae hospitali wakati ukweli ni kwamba mwanae si mgonjwa?
 
Kumfuta mtu ushirika haimaanishi kuwa ametengwa au ameachwa na Kanisa, bali ni dhihirisho la wazi kuwa Kanisa haliungani na na dhambi ambayo huyo muumini amefanya....
Upuuzi, Nikitenda dhambi nitatubu, kama kanisani mpo watakatifu tupu nitasali na familia chini ya mti
 
Bado mnazunguka pale pale

Je kuna tofaut gan kati ya nyie mnaofuta mtu ushirika na wale waliokuwa wanapiga mawe? Dhambi ya hasharani iv nyie mnaomfuta mwenzenu ushurika ni wasafi? Mna dhambi ngap sirini?

Sasa hapi mnamforce mtu ajifanye msafi kwenu ili abatizwe na kurejeshewa ushiriki wakat toba ni kati ya mtu na Mungu wake hamuon mnafamya unafik?

Mimi ninaamin nikikosea napasw nitubu kw Mungu wangu kwa dhati na sio kuwafurahisha myie
 
Dini inapunguza uwezo wa kufikiri. mtoa mada hili fikirisho lako litabeba baadhi ya waumini wanaopenda kudadisi.
 
Dhambi zote ni sawa ila watu wanafikiri dhambi kubwa ni kuua na uzinzi.
Kama mtu ni muumini wa kawaida anatubu kwa Mungu wake anaendelea kusali kama ni kiongozi anasimamishwa kuongoza kwa muda fulani kisha anaendelea kuongoza kama ni tabia endelevu anavulishwa kiongozi na kuwa muumini wa kawaida ila hayupo mtu yoyote anayeweza kumfukuza mtu kusali kanisani.
Uongozi una utaratibu na kanuni zake na siyo kila mtu anaweza kuongoza.
Siku hizi watu wanaabudu dini kuliko Mungu ndiyo maana usije ukaashangaa ukasikia mtu anasema dini yake safi wakati kwenye dini yake kuna waumini walevi, wauaji, wasengenyaji, wazinzi n.k
 
Enzi za wana wa Israeli watu walikuwa wakitenda dhambi wanachukua kondoo safi na kupeleka kwa kuhani wanatubu dhambi zao then kondoo anachinjwa moto kutoka juu unashuka na kuiteketeza hii huashiria sadaka yako imepokeleqa na dhambi zimesameheka

Mtu alikuwa akitenda dhambi ya hadharani esp uzinzi basi hakukuwa na toba alikuwa anaadhibiwa pale pale kwa kupigwa na mawe mpk kufa

Yesu alipokuja duniani tukio kama hilo lilitokea(aliletwa mwanamke mzinzi aliyetenda hadharan na wakamshika na kumpeleka kwa Yesu ili kumpima na Yesu alichora chini kisha akawaamuru asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga mawe yule mwanamke< inasemekana pale chini kila mtu aliposoma aliona dhambi yake imeandikwa we are not sure yet> basi wote wakatawanyika na yule mama akasamehewa dhambi zake)

Yesu alipokuwa msalabani kuna kondoo wa sadaka alikuwa achinjwe but pazia likapasuka na kondoo akakimbia(wakristu tunaichukulia kama ilikuwa ndio mwisho wa kutoa sadaka ya dam ili kusamehewa dhambo zetu kwa sababu dam ya Yesu ilimwagika pale msalabani)

Baada ya ujio wa Yesu Ukristo ukazaliwa na ukawa completely tofaut na Waislaer wa zaman( tukapewa uhuru wa kutubu direct kwa Mungu kupitia Yesu kristo)

Nakuja kwenye point sasa :- Kama yesu alisema asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga yulewanamke na wote wakaondoka maana wote walijua ni wadhambi inaluwaje bado wasabato tunashikilia ule ujinga wa dhambi ya hadharani mti anaadhibiwa hdharani?( ikitokea umezini na ikajulikana basi unafutwa ushirika)

Iv naomba niulize Yesu si alituunganisha na Mungi direct? Kama nimetenda dhambi si napaswa kutubu kwa Mungu wangu? Why wanadam mnasimama sehem ya Mungu na kuhukum? Je nyie mnaomfuta mtu ushirika mnakuwa hamna dhambi? Mnakuwa watakatifu? Kuna tifaut gan kati ya kumfuta mtu ushirika na wale waliokuwa wanapiga mawe?

Wasabato kuna ujinga ukipatwa na dhambi ya hadharan(wamebase kwenye uzinzi tu) unafutwa ushirika na unapaswa ubatizwe tena
Iv kwenye Biblia nan alibatizwa mara ya pili? Iv nikikosea napaswa nitubu kwa Mungu au kwenu? Maana kuniambia nibatizwe tena manake hapo nawaonesha nyie kuwa nimekosea nisameheni nibatize nirud kundini why nyie? Na sio Mungu?

Mimi naona ni makosa makubwa sana kumfuta ushirika mtu kosa ametenda dhambi ya wazi haina tofaut na walivyokuwa wanapiga mawe
Sasa Yesu alikuja wa nini kama bado watu wanahukum?

Mimi ni msabato niliyezaliwa kwenye dini tangu mababu huko na nimekuwa kwenyw misingi kabisa ya dini ila kwenyw hili swala nimepingana na kanisa maana pale kanisan nikiwaangalia sion mtakatifu wote sisi ni wadhambi ni rehema tu ya Mungu iko nasi sasa why tuwe wa kwanza kuhukum wenzetu wakat tumwzuiwa kuhukumu?

Mtu anakukalia koon kisa umefumwa unazim wakat yeye ana michepuko kibao

Mimi 2008 nilikuwa kwenye baraza la kanisa mahali flan huko Mkoa wa Mara jamaa mmoja akaoa sogea tukae wakaita baraza kumfukuza
Aisee niliwacharura sababu wale wazee wote nilikuwa najua michepuko yao" ambaye anajua sijui maovu yake amfute ushirika huyu mtu au ambaye ana mstari wa kwenye biblia unaosema watu wafunge ndoa ya cheti kwa vuongozi wa dini atoe hapa" tulisumbuama but atlast nilishinda na jamaa hakufutwa ushirika na maisha yakaendelea

My advice( em tuache kuwa mahakimu wakat sisi wenyewe si wakamilifu pls)
Mtu akitenda dhambi iwe ya hadharan au ya kujificha mwachen amalizane na Mungi wake mwenywwe
Pole sana Mtumishi. Au yamekukuta?

Anyaways. Maandiko yanasema kama ndugu yako akikukosea ongea nae, akikubari yanaisha, asopofanya hivyo nenda na mtu mwigine, asipokubali peleka kwenye baraza kisha harmashauri. Kwanza nenda kasome miongozo ya kanisa kuhusu kufutwa ushirika. Ni ngumu mno na si rahisi.
Binadamu wanatenda dhambi, zingine za siri zingine live. Lakini yote hayo hukumu ni kwa Mungu.

Ili dini iwe dini lazima kuwe na utaratibu wa namna ya kuishi. Huwezi ruhusu mtu afanye uzinzi, wizi, uongo hadhalani na ukawa unamchekelea tu, litakuwa dangulo na si kanisa.

Habari ya kusema umezaliwa kwenye dini anza kujifunza upya, maana watu wa namna hii wamegeuza dini na kuwa kama tamaduni zao wala hawashituki.

Kasome Mwongozo wa kanisa vizuri ili uelewe kwa nini mtu afutwe ushirika. Ulivyo andika inaonekana unaishiaga kusikiliza tu na hujawahi kusoma mwenyewe.

NAKUOMBEA. NAWE OMBA.
 
Back
Top Bottom