Naomba kunisaidia hii hali niliyo nayo: Naweza kumsaidia mtu hata kama ninacho kidogo natoa nabaki sina kitu

Trial balance

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
202
159
Jamani najikuta kuwa na huruma sana ya kumsaidia mtu hata kama sina na kama kipo kidogo nakubali kutoa chote nibaki kama nilivyo nitafute kingine japo sijui nakipata wapi mfano kukopesha mtu ela yani hata kama nimebakiwa na buku na mtu kaniazima buku kwa wakati huo nampa tu nabaki bila kitu hii hali imekuwa sugu akilini mwangu yani nashindwa kumnyima mtu na nitakavyompa naonesha kufurahi na kuonesha zipo nyingine haina shida kabisa.

Naomba mnisaidie kupambana na hii tabia najisikia vibaya kumnyima mtu kitu.

Nakubali kuteseka nishinde ata njaa kwa ajili ya mtu.
 
Jiunge na mashirika ya masister utasaidia wengi
Sina kalama ya usister yani hapa nipo chuo lakini nawaza kusaidia ndugu ambao hawajiwez ata kuwapelek fan yoyot ile ila sema napitia vikwazo sana huku ninakosoma mungu anisaidie sana
 
Fanya meditation itakupa Uhuru wa kuwa unavyotaka pia Uhuru wa kutoa kiasi pia kuwa responsible labda bado unategemea wazazi na ndugu sana. Jaribu kuanzisha biashara yeyote ile uone ugumu wa kupata Tsh 1000 hivyo hivyo hutoitoa kirahisi rahisi.

Kusaidia wahitaji ni jambo jema ila unaposaidia na kujiumiza ni dhambi na tatizo unapaswa kusaidiwa sana. Fanya biashara nakuapia utabadilika pia ondoa hali ya kujikweza kwa kujionyesha unacho ili hali huna cha ziada ni tabia mbaya na ni dalili za kuwa masikini wa kutupwa ukitetereka kidogo kimaisha na ukakosa msaada utaumia sana na kujutia kidogo ulichowahi kujaaliwa na kukitapanyaa.

Kataa roho ya umasikini usimpe mtu chakula bali mfundishe namna ya kupata chakula tambua muda unakwenda na haurudi yaliopita sio ndwele waweza kuanza sasa bado hujachelewa.
 
endelea dada na wema wako lakini usizidi uwezo!ni kweli kutoa ni moyo sio utajiri.na pia nnachojua ukitoa nawe unalipwa zaidi na mungu
 
Fanya meditation itakupa Uhuru wa kuwa unavyotaka pia Uhuru wa kutoa kiasi pia kuwa responsible labda bado unategemea wazazi na ndugu sana. Jaribu kuanzisha biashara yeyote ile uone ugumu wa kupata Tsh 1000 hivyo hivyo hutoitoa kirahisi rahisi...
Sina tabia ya kujionyesha Bali kuna hali ya huruma tu inanikuta nishawahi Fanya kazi nakupata salary lakini nikinunua kitu ata kama kidogo ntakula na wezangu kidogo kidogo na kama mtu akinikopa ela nilitoa ata kama niliona mshahara bado kutoka na nilitoa akiba yangu.
 
Hahahaha binadamu tuna silka za ajabu Sana duh! Sikia Trial balance..Mimi pia nna Hali hiyo na hua najiuliza Sana Ni Nini hiki? Lakini hiyo Tabia nimejifunza kuiacha kwa muda Sasa....kitu Cha kwanza jifunze kusema No.

Kama unasaidia saidia kile Cha ziada sio mpaka uumie Ni dhambi ACHA!..Hiyo Tabia itakupeleka kwenye umaskini na ushangae hao unaowasaidia wanakuangalia tu, tena waanze kukusema na kukukejeli....

Ukijifunza kuhusu binadamu walivyo nakuhakikishia utaacha haraka sana..anyway swali la kizushi....vipi na wanaume hua unawaonea huruma na kuwapa mwili wako hivyo hivyo?
 
Jamani najikuta kuwa na huruma sana ya kumsaidia mtu hata kama sina na kama kipo kidogo nakubari kutoa chote nibaki kama nilivyo nitafute kingine japo sijui nakipata wapi mfano kukopesha mtu ela yani hata kama nimebakiwa na buku na mtu kaniazima buku kwa wakati huo nampa tu nabaki bila kitu hii hali imekuwa sugu akilini mwangu yani nashindwa kumnyima mtu na nitakavyompa naonyesha kufurahi na kuonesha zipo nyingine haina shida kabisa.naomba mnisaidie kupambana na hii tabia najisikia vibaya kumnyima mtu kitu.nakubari kuteseka nishinde ata njaa kwajili ya mtu.
Fanya hayo yote kwa Jina la Yesu Kristo na kwa ajili yake hutapungukiwa na kitu na pia toa kwa ajili ya kazi ya Mungu (Yesu Kristo) utaona maisha yako yatakavyonawiri.
 
Hahahaha binadamu tuna silka za ajabu Sana duh! Sikia Trial balance..Mimi pia nna Hali hiyo na hua najiuliza Sana Ni Nini hiki? Lakini hiyo Tabia nimejifunza kuiacha kwa muda Sasa....kitu Cha kwanza jifunze kusema No. Kama unasaidia saidia kile Cha ziada sio mpaka uumie Ni dhambi ACHA!..Hiyo Tabia itakupeleka kwenye umaskini na ushangae hao unaowasaidia wanakuangalia tu, tena waanze kukusema na kukukejeli....Ukijifunza kuhusu binadamu walivyo nakuhakikishia utaacha haraka sana..anyway swali la kizushi....vipi na wanaume hua unawaonea huruma na kuwapa mwili wako hivyo hivyo?
Duh hapana mwili na kumsaidia mtu tofaut rafik angu
 
Back
Top Bottom