Naomba kujuzwa utaratibu na gharama za kusafirisha maiti kwa ndege ndani ya Tanzania

Spa Africa

Member
Mar 8, 2018
24
57
Wakuu naomba kujua kwa wale wenye ufahamu,eti ni vitu gani natakiwa kukamilisha ili niweze kusafirisha maiti toka mkoa mmoja kwenda mwingine kwa kutumia ndege?

Je kwa makadilio gharama inaweza kuwa bei gani ili niweze kuusafirisha mwili?Na je ni lazima kukodi ndege kama tunavyofanya kwenye kukodi magari tunapopeleka maiti mkoani au unaweza kupakia tu kwenye ndege ya abiria?

Naomba msaada kwa wale wenye uelewa.Asante
 
Ni kujipanga tu,kama hutaki kuipa "usumbufu" maiti yako kwenye milima ya Sekenke Shelui Singida au mlima Nyoka kule Mbeya,unaweza kuisafirisha kwa ndege.Bahati nzuri katika usafiri wa ndege sio lazima ukodishe ndege binafsi kama tunavyokuwa tunakodisha magari pale Biafra kwa huko Dsm.

Usafiri wa ndege unaweza kutumia ya abiria tu,na maiti ikasafiri kama mzigo,kwani kimsingi mwili wa mtu ukishafariki,unakuwa-treated kama Cargo tu.

Kwanza unatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo(labda wawe wamebadili,maana nina miaka kama minne toka nisafirishe maiti ya jamaa yangu kwenda Mwanza).Nyaraka hizo ni hizi;

1)Embalming Certificate.Hii ni hati ya uthibitisho kuonyesha kuwa mwili wa marehemu umekuwa treated na madawa(chemikali) ili uweze kuuwa wadudu,kutoa harufu na kuepuka umwagikaji wa "fluid" toka ktk mwili wa binadamu.Hapa inajumuisha kumwagia manukato marehemu,kumvisha begi la plastiki kuondoa uwezekano wa damu na maji kumwagika kwenye ndege.Wazee wenzangu wanajua ile "Local Embalming" ambayo huwa tunafanya tunapowasitiri wenzetu.Mabingwa wa "Embalming" ni Wamisri na jamii za watu wa dini ya Kiislamu.Mafirauni walifanyiwa hii na kuwekwa kwenye mapiramidi kwa miaka mingi sana.

2)Death Certificate.Hii ni nyaraka mojawapo inayotakiwa.Nadhani kila mtu anajua kwanini hii inahitajika na wapi inapatikana.

3)Affidavity.Hii nafikiri husainiwa na Dr aliyethibitisha kuwa mgonjwa/mtu amefariki kwelikweli(Wanaoelewa zaidi watanisahihisha).Kuna maiti huwa zinakurupuka mkiwa angani au hata njiani mkiwa mnazipeleka kwao kuzika,so lazima ithibitishwe kuwa anayebebwa amekata kamba kwelikweli na harudi tena.

4)Handling Fee(Nadhani haizidi laki mbili).Hii hutolewa kwa ile kampuni itakayoi-handle maiti inapofika eneo la mizigo,kuipima kilo na hatimaye kuikokota mpaka kwenye ndege.

5)Malipo ya maiti kwa kilo.Sasa gharama huwa inategemea na uzito wa maiti.Sasa kama ndugu ana mwili kama ule wa Pepe Kale,hapo ndio ndugu lazima mjichange sana,maana hii hujumuisha uzito wa mwili wa marehemu jumlisha na jeneza.Nakumbuka ilikuwa shilingi 7000 kwa kilo,so kama maiti ana kilo 100 na jeneza kilo 40,basi ni kilo 140x7000.

Mkuu mleta mada,unaweza kuwa umepata mwanga hata kama kuna vigezo vinaweza kuwa vimebadirika,lakini hii nafikiri ndio "procedure" ya huko nyumbani.
 
Back
Top Bottom