Naomba kujuzwa uhusiano wa simu na radi

Mwalimu Truth

Member
Feb 15, 2015
57
62
Habari wana Jf.Naomba kuuliza,hivi ni kweli kutumia Simu wakati wa Mvua yenye ngurumo za radi kuna madhara yoyote yanaweza kumkuta mtumiaji?Simu na radi kuna uhusiano gani kitaalamu katika inshu za mionzi nk?

Binafsi,pengine kutokana na ujuzi mdogo,sioni kama kuna uhusiano wowote na iwapo radi ingekuwa inasababisha madhara kwa watumiaji wa simu basi Wabongo wengi tungepoteza maisha.

Mwenye utaalamu na facts za Kisayansi naomba anifahamishe kuhusu suala hilo maana kuna taarifa nimeona ikizagaa mtandaoni kuhusu mtu mmoja kupata madhara wakati akitumia simu yake mvua ikiwa inanyesha.
 
Ukielewa kwanini radi inaunguza vifaa vya umeme basi huta uliza hata hilo swali.

Simply ni kwamba

Radi ni + chargers so huwa inaunguza vitu kwa sababu Dunia/ earth ni - charges

So nadhani unaelewa + na - zikigusana nini kinatokea.

So simu pia ina umeme. so radi ikipiga ule umeme ambao unasafiri wirelessly unaweza kuingia kwenye simu na kuunguza simu.

Kanuni hii ndiyo ambayo inatumika na radi katika kuunguza vitu.

Imagine simu inatumia Volt 9 radi inapiga na kuzalisha Milions Volts na kuingia kwenye simu je utabaki salama??

Hiyo idea yako ya mionzi haihusiki kabisa na hii scene
 
Back
Top Bottom