Naomba kujuzwa ubora na changamoto za Gari aina ya Toyota Pixis Epoch

Oct 18, 2017
25
11
Habari ndugu,

Nimejaribu kupita kwenye website mbali mbali zinazouza used cars kutoka Japan nimekutana na gari aina ya Toyata Pixis Epoch na imenivutia hasa kutokana na ulaji Mdogo wa mafuta (32km/ litre) ila kwavile sina utaalamu kabisa wa magari nimeona niulize kwa anayefahamu kama hizi gari zinachangamoto zozote kwa matumizi ya kitanzania ya kawaida kwa mazingira ya mjini.

Na kama hakuna ni kwanini sioni zikimilikiwa na watu wengi kama ilivyo Passo, IST, Vitz na nyingine zenye mfanano huo.

Natanguliza shukrani.

1591846829863.png

Toyota Pixis Epoch
 
Duh. Sijawahi isikia hii gari. Jilipue tu,kuwa wa kwanza,wewe ndio uwe reference yetu huko baadae. Kila la heri
 
Hiki kigari kizuri sana nilikuwa nashangaa hio economy yake km/l il so far ni kigari ambacho kina engine kama ya suzuki kei (660cc) nadhani watakuwa Toyota wameingia ubia na Suzuki kukitengeneza maana Suzuki ndio wakali wa hizo kazi. 🤣🤣🤣 na wabongo hawajakijua hiko.

Wakikijua tu na kikawa hakina shida kama za Passo! Basi IST soko lake litaelekea kwenye ukomo.
 
Hiki kigari kizuri sana nilikuwa nashangaa hio economy yake km/l il so far ni kigari ambacho kina engine kama ya suzuki kei (660cc) nadhani watakuwa Toyota wameingia ubia na Suzuki kukitengeneza maana Suzuki ndio wakali wa hizo kazi. na wabongo hawajakijua hiko.

Wakikijua tu na kikawa hakina shida kama za Passo! Basi IST soko lake litaelekea kwenye ukomo.
Asante.
 
Hivi matatizo ya passo ni yapi mkuu.
 
Hivi matatizo ya passo ni yapi mkuu.
Mfumo wake wa steering rack upo so delicate. Bushes za mbele zinakufa haraka na inagonga sana mbele hata kama umefanya service leo itakuvumilia sana mwezi balaa linarudi tena.

Plus engine ya passo nguvu haina especially ukipakia watu watano katika gari including driver then uwashe AC kana kuwa kazito sana karibia ya kuzimika maeneo ya miinuko.

Si kagari imara sana kukaa nako eneo ambalo unapita kila siku zaidi ya kilometers kuanzia tatu maana hayo matatizo ya bushes kuisha na gari kugonga huwa yanaanzia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom