Naomba kujuzwa tofauti za kimaslahi kati ya kufungua kesi ya madai Mahakama za mwanzo na za Wilaya.

mchezo mbaya

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
242
235
Nilishinda kesi ya jinai katika Mahakama ya mwanzo (kuvunjiwa na kuibiwa). Baadae nikashauriwa nifungue kesi ya madai ili nilipwe haki zangu yaani pesa inayolingana na thamani ya vitu nilivyoibiwa. Naombeni msaada wa kisheria au ushauri ili nipate haki haraka na iliyokamilika. Pesa ninayoidai in TShs 3,000,000/= inayoendana na vitu vilivyoibwa. Kingine ni nyaraka ambazo ni hati za nyumba. Naomba kujua ni Mahakama IPI inaweza kunipa haki vizuri?. Na je, Nakala ya hukumu pekee inatosha kuwa ushahidi bila kuwahusisha tena mashahidi?.Maana nasikia kuwa Mahakama za mwanzo zina mipaka yake kimaamuzi ambayo ni tofauti na za Wilaya. Natanguliza shukurani.
 
Unaweza kufungua mahakama ya mwanzo iwapo sheria inayohusika ni ya mila au kiislamu. Kama sivyo inatakiwa uende mahakama ya wilaya au hakimu mkazi. Nakala ya hukumu itakusaidia kuonesha ulishinda kesi dhidi ya wadaiwa wako ila nadhani unahitaji ushahidi zaidi ili kuthibitisha thamani ya hizo mali utazozidai
 
Nashukuru kwa ushauri mzuri mkuu.
 
Back
Top Bottom