Naomba kujuzwa tiba ya tatizo la kutoona mbali

Steph JK

Senior Member
Sep 14, 2018
103
106
Habari wadau,

Nimeanza kupata tatizo la kutotambua mtu aliyezaidi ya mita hamsini naweza kumwona Kama mtu yule pale lakini nashindwa kumtambua ni Nani hata Kama namjua.

Naomba msaada wa hili kabla ya tatizo halijawa kubwa zaidi.
 
Nenda kapime kwanza macho upewe mewani kisha uendelee kutafuta tiba ya tatizo
 
Habari wadau
Nimeanza kupata tatizo la kutotambua mtu aliyezaidi ya mita hamsini naweza kumwona Kama mtu yule pale lakini nashindwa kumtambua ni Nani hata Kama namjua. Naomba msaada wa hili kabla ya tatizo halijawa kubwa zaidi
TATIZO LA KUTOONA MBALI



Tatizo la kutokuwa na uwezo wa kuona vitu vilivyo mbali ni changamoto ya uonaji inayowasumbua watu wengi sana Tanzania na duniani kwa ujumla.

Changamoto hii hutambulika kwa mtu kushindwa kuona vitu vilivyo mbali. Watu hawa wanapoangalia mbali hushindwa kutambua taswira zilizo mbali.

Tatizo la kutokuwa na uwezo wa kutoona vitu vilivyo mbali hutokea pale macho au jicho linapokuwa kubwa au sehemu ya jicho inayoruhusu mwanga wenye taswira kuingia ndani ya jicho; yaani cornea, kuwa imekunjika kuliko kawaida hivyo kushindwa kuelekeza mwanga wenye taswira kutua kwenye eneo la nyuma la jicho linalohusika na kusafirisha kile kinachoonekana kwa ajili ya kutafsiriwa kwenye ubongo.

Hali hizi mbili husababisha mwanga wenye taswira unaoingia kwenye jicho kutoweza kufikia eneo la nyuma ya jicho yaani retina.

Hii husababisha retina kushindwa kupeleka taarifa zenye taswira kwenye ubongo na matokeo yake hushindwa kutafsiri taswira ambayo mtu anajaribu kuitazama. Matokeo yake ni wewe kushindwa kutambua unatazama nini.

Mpaka sasa sababu ya kwa nini watu wengine wanakuwa na macho makubwa, haijajulikana ila kuna hisia kuwa hali hii hutokana na vinasaba na ndiyo maana tatizo hili huoneakana zaidi kwenye familia zenye watu wenye tatizo hili.

Watu ambao kwenye familia kuna historia ya tatizo hili ndio wako hatarini kukumbwa na hali hii. Kama mzazi mmoja au wote wawili wana tatizo hili (na wanavaa miwani) basi kuna uwezekano wa karibu asilimia 95 kwa mmoja wa watoto kuwa na tatizo hilo pia.

Wengine ni watu wanaotumia muda mwingi sana kujisomea na wale wanaokosa muda wa kutoka nje na kupata fursa ya kuangalia mbali mara kwa mara.

Dalili za kutokuwa na uwezo wa kuona mbali ni kushindwa kutambua taswira halisi ya vitu vilivyo mbali, kufinya macho au kukunja sura mara unapotaka kuangalia mbali, kuumwa kichwa kutokana na kutumia nguvu nyingi kujaribu kutambua taswira ya vitu vilivyo mbali na kushindwa kuona nyakati za usiku.

Kwa watoto changamoto hii mara nyingi hutambulika tangu mtu mwenye tatizo hili akiwa mdogo kabisa kiumri au anaonekana akiwa amekunja uso au kufinya macho au anasogea karibu na runinga wakati anatazama au darasani mtoto anaonekana akisogea karibu na mwalimu.

Dalili ya tatizo hili kwa watoto pia ni kutofahamu kabisa yanayoendelea mbali na mahali alipo au kufikicha macho mara kwa mara.

Tatizo hili hugunduliwa kwa vipimo vya kawaida tu vya macho vinavyopatikana katika hospitali maalum za matibabu ya matatizo ya macho.

Vipimo hivi hupatikana kirahisi zaidi tukilinganisha na vipimo vya kupima tatizo la kutoona vitu vilivyo karibu.

Hata hivyo mtu yeyote mwenye matatizo ya macho anapaswa kwenda hospitali ili kuchunguzwa na kupatiwa matibabu sahihi. Mgonjwa yeyote wa macho anapaswa kuepuka kutumia miwani hata kama inaonekana kumsaidia kutatua tatizo hadi amepatiwa na mtaalamu hospitalini.
TATIZO LA KUTOONA MBALI

Mkuu ukitaka matibabu yake Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona kw adawa zangu za asili.
Ukiwa na Shida yoyote ile.
 
Akisha enda kupima Miwani hawezi tena kuona mbali pasipo na kuvaa miwani . Inakuwa amesha jitibia yeye anataka kujuwa sababu ba dawa wewe una mwambia aende kupima miwani?
😂Ahsante mkuu kwa kuniweka sawa lakini wewe pia umeninukuu tofauti sijamwambia akapime miwani bali akapime macho najua ndio tiba yake akienda uko atapata tiba hiyo na hajataka kujua sababu ya tatizo bali ametaka tiba, mtibie mkuu asivae miwani.
 
Mimi sioni karibu. Ni mwendo wa miwani tu na lasik surgery naiogopa kinyama...
Kichwa kina magonjwa ya ajabu ajabu sana, macho yamenitesa kwa muda mrefu,miaka sita sasa navaa miwani. Mwaka jana nimeenda kwa kinyozi nashangaa ananibadilishia kimo cha kunyoa, nikamuuliza kulikoni? Ananiambia "mzee, hapa juu nywele hamna kabisa,kuanzia sasa nitakuwa nakunyoa za kuota".

Yaani naumwa (sioni mbali)macho, naumwa (kipara) nywele.
 
Kichwa kina magonjwa ya ajabu ajabu sana, macho yamenitesa kwa muda mrefu,miaka sita sasa navaa miwani. Mwaka jana nimeenda kwa kinyozi nashangaa ananibadilishia kimo cha kunyoa, nikamuuliza kulikoni? Ananiambia "mzee, hapa juu nywele hamna kabisa,kuanzia sasa nitakuwa nakunyoa za kuota".

Yaani naumwa (sioni mbali)macho, naumwa (kipara) nywele.
Kipara siyo ugonjwa bana. Nadhani ni hela tu zimekukubali sasa unaota kiupara cha kipapaa. God is good
 
Back
Top Bottom