Naomba kujuzwa taratibu za kuwaandikisha watoto mali kisheria

mafoleni

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
220
371
Ndugu zangu,

Naomba msaada kwa anaeelewa taratibu za kuandikisha watoto mali kisheria. Mimi nina kajumba kangu ila nataka niwaandikishe wanangu wawili. taratibu zipoje? au unachukua tu karatasi unaandika kama wosia.

Nisaidieni jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna muundo maalumu wa kuandika wosia lakini kuna vitu lazima uvizingatie ili kuweza kuandika wosia ulio halali na unaoweza kutekelezwa kisheria.

1) Testamentary capacity
Hii ni hali ya mtu ambae anaandika wosia kuwa na ustadi wa kisheria na kiakili wa kuandika wosia huo.

2) Umiliki wa mali na Wanufaikaji
Lazima kuonyesha nani mmiliki wa mali hizo, wapi zilipo mali hizo na kwa uwazi mgawanyiko wa mali hizo kwa wanufaikaji.

3) Tarehe, Sahihi na mashahidi.
Lazima kuandika tarehe, lazima kuweka Sahihi kwenye kila ukurasa wa wosia wako huku ukiwa na mashahidi wasio pungua wa nne ambao na wao lazima waweke Sahihi.

4)mtekelezaji
Lazima kumuandika jina, kumfahamisha mtu huyo kuhusu uteuzi huo na jukumu lake ni kuyafuata na kuyatekeleza maagizo ya wosia wako kama ulivyo andika.

5) utunzaji salama
Lazima utunze wosia wako sehemu salama na ambayo inafahamika, ili wosia wako uweze kupatikana kwa wakati husika pindi unapo hitajika.

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom