Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,049
- 24,428
Wanajf, bila shaka popote linapotajwa jina la ndege aina ya Tausi, basi bila shaka moja kwa moja zinakuja fikra za kuwaza ikulu! Na hii ni kwa sababu, ndege hawa wamekuwa maarufu zaidi kufugwa kule magogoni,na hivyo si rahisi kuwakuta sehemu nyingine kama majumbani au hata katika mbuga zetu!Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere bila shaka ndiye aliyekuwa muasisi wa kuwafuga hawa ndege aina ya Tausi ikulu, na Marais waliofutia wote waliendeleza utamaduni wa kuwafuga na kuwatunza!
Katika awamu hii, Rais Magufuli amekuwa akiwahusudu sana hawa ndege na inaonyesha anawapenda sana! Alimpa Rais wa Kenya, Mh. Kenyata lakini vile vile alimpa masharti baada ya kumpatia!
Katika ikulu mpya inayotengenezwa Dodoma, amehakikisha hawa ndege wanakuwa katika eneo hilo ili kuenzi utamaduni wa kuwafuga ambao ulianzishwa na Baba wa taifa!
Sasa, je hawa ndege tofauti na umbo lao la kuvutia ni sababu gani hawa ndege inawafanya wawe maarufu hivi, kiasi cha kufikia kufugwa tu ikulu?
Ni kwa nini hawa ndege hugawiwa viongozi wakubwa tu, mfano Rais mstaafu Kikwete ametangaza kupewa na Rais Magufuli, pamoja na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere?
Je kuna siri gani juu ya hawa ndege inayowafanya watunzwe kwenye maeneo sensitive kiasi hicho?
Vipi, kuna watu binafsi wanaowafuga kama bata, kuku n.k?
Je, raia wa kawaida akitaka kuwafuga, kuna utaratibu wa kufuata ili awapate, na atawapata wapi zaidi ya ikulu? Wanajf, naamini hiki ni kisiwa cha maarifa, na wapo wajuvi wanaojua kuhusu hili, hebu mtutoe tongotongo tafadhali!