Naomba kujuzwa Mkoa na Wilaya Bora ya kuishi kwa utulivu na kuwa na maendeleo

Kigoma maisha yapo chini ila service ni shida, mfano mitandao simu ni shida.
Kigoma mjini mitandao ya simu yote haina shida,labda unasema vijijini huko mbali...Ila akiishi mjini mambo safi chakula(samaki wa wakubwa watamu Tz nzima..pale SOKONI kwa baba Levo..jioni!!!,makazi,usafiri rahisi,benki zipo na dola inapatikana hata kwa watu kimagumashi,boda Kongo,Burundi na Zambia kibiashara hali ya hewa nzuri mvua za kutosha,beach na hotel zipo,maeneo yaliyotulia kama mjimwema kwenda popote ni rahisi sana.
 
Kiuhalisia mji ni Dare es salaam tuu, Kwa hapa Tanzania , miji mingine utasota Sana mpak network ya maisha ije isome shidaaa, miji mingine ukitoboa watu wote wanakufahamu unakuwa monitored vibaya sana, Dsm watu ni wengi hata ukitoboa huwez julikana kama umetoboa , usinitch mdogo , DSM mzunguko wa Pesa ni mkubwa sana ni wewe Tu kuongeza speed, miji mingine ina changamoto ya ukabila asikudanganye mtu, ila kama kazi yako ya kujifungia chumban tuu , nenda Moshi
Moshi pazuri, changamoto inayoukumba huo mji kwa siku za hivi karibu ni hali ya hewa, Moshi inakubwa na tatizo la joto...kuna wakati moshi joto linakuwa kali sana kupindukia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazani mkoa wa Iringa manispaa, au Wilaya ya Kilolo ni sehemu nzuri na tulivu kuishi. Gharama za maisha ziko chini japo sina hakika na ubora wa Network. Hautojutia kuishi Iringa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nataka nihamie hapo. Nina laki 5... biashara gani naweza kufanya? Vyumba bei gani huko? Maisha yapoje kiujumla

Sent using Jamii Forums mobile app

Karibu sana. Kwa laki tano unaweza kupeleka machungwa na kutauza kwenye mabasi na wenzio pale chalinze njia panda. Vyumba bei inatofautiana m.f self ya vyumba vitatu huku ni 45,000 tu, ila njoo na kuku weusi wawili na mkojo wa ngiri, bila hivyo ukilala utajikuta nje.
 
Mkoa gani ambao mtu anaweza kuishi ikiwa anajishughulisha na shughuli za mtandaoni na kuhitaji utulivu na gharama ndogo ya maisha maana kuna kupata pesa nyingi halafu ukajikuta yote inatumika kwa mahitaji ya kila siku kwani hapa nilipo (Dar) ni kama gharama ya maisha kila siku ni kubwa pesa nyingi inatumika.

So unaweza kuwa na uzoefu na mkoa gani ambao kwa mtu wa online business akaweza kuishi.

Mkoa wenye internet ya kasi especially TTCL na Tigo

Huduma za kibenk equity na rate ya exchange ya dollar iwe nafuu kidogo.

Shughuli zangu hazitegemei watu zaidi walionizunguka

Pia uhakika wa umeme.

Pia utulivu na uwezekano wa mtu kuwekeza na maana maisha yanabadilika unachotegemea leo kinaweza kukwama.

Gharama ya maisha (upatikanaji wa chakula kwa bei rahisi)
Mkoa wa Geita
Wilaya ya Chato
 
Chato, kila kitu kimejaa hadi alama za punda milia barabarani na zaidi ya yote kuna mbuga za wanyama hadi simba na chui-duma. Huna haja kulipa gharama kubwa kwenda kuwaonesha wanao
 
Karibu sana. Kwa laki tano unaweza kupeleka machungwa na kutauza kwenye mabasi na wenzio pale chalinze njia panda. Vyumba bei inatofautiana m.f self ya vyumba vitatu huku ni 45,000 tu, ila njoo na kuku weusi wawili na mkojo wa ngiri, bila hivyo ukilala utajikuta nje.
Chalinze na Morogoro wapi bei ya vyumba Iko juu?
 
Back
Top Bottom