Naomba kujuzwa Mkoa na Wilaya Bora ya kuishi kwa utulivu na kuwa na maendeleo

Mkuu sogea tu hapo Bagamoyo ukipashindwa unaweza kwenda Kilimanjaro kwenye kimji cha Bomang'ombe ukishindwa nenda Bukoba mjini . Nje ya hapo ukubali kubaki Dar lakini ukaishi nje ya mji ng'ambo ya pili Kigamboni ya Kimbiji
Mkoa gani ambao mtu anaweza kuishi ikiwa anajishughulisha na shughuli za mtandaoni na kuhitaji utulivu na gharama ndogo ya maisha maana kuna kupata pesa nyingi halafu ukajikuta yote inatumika kwa mahitaji ya kila siku kwani hapa nilipo (Dar) ni kama gharama ya maisha kila siku ni kubwa pesa nyingi inatumika.

So unaweza kuwa na uzoefu na mkoa gani ambao kwa mtu wa online business akaweza kuishi.

Mkoa wenye internet ya kasi especially TTCL na Tigo

Huduma za kibenk equity na rate ya exchange ya dollar iwe nafuu kidogo.

Shughuli zangu hazitegemei watu zaidi walionizunguka

Pia uhakika wa umeme.

Pia utulivu na uwezekano wa mtu kuwekeza na maana maisha yanabadilika unachotegemea leo kinaweza kukwama.

Gharama ya maisha (upatikanaji wa chakula kwa bei rahisi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh.....!!! Huko atakuwa amejitenga na Tz na kujiweka karibu na Burundi

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalizo: Ameandika hapo juu kuwa shughuli zake zinatumia mtandao zaidi na mtandao hauna mipaka unayoitaja hapa, zaidi sana kuna huduma zote za kimtandao katika wilaya hiyo ambao hauna watumiaji wengi.
 
Kwa masharti na vigezo ulivyotoa naona wilaya ya Kibondo mkoa wa Kigoma itakufaa. Gharama za maisha hasa vyakula ziko chini sana, umeme upo na mitandao yote ya simu ipo.
Kigoma maisha yapo chini ila service ni shida, mfano mitandao simu ni shida.
 
Yanda za juu kusini yaani mbeya iringa njombe songea
Chakula cha kutosha aina vyote
Hali ya hewa ni baridi kipindi chote cha mwaka mazingira kijani fursa za kilimo na biashara

Njombe. Wilaya makete pazuri sana milima mashamba biashara hali ya hewa baridi ila ndio mkoa na wilaya inayoongoza kwa ukimwi kama una familia usiende

Songea kwa familia panakufaa wilaya mbinga kitu kipo

Sent using Jamii Forums mobile app
Makete wakinga wenyewe wamepakimbia we jamaa.Makete ndio wilaya ngumu zaidi Njombe ipo periphero haina barabara nzuri.Makete unaweza fananisha na wilaya ya Ileje kwa mbeya ya zamani.
 
Dar es Salaam bhana usihangaike. huko Moshi hata Mwamposa kulimshinda hadi alipokuja Dar es Salaam.
juzi alirudi Moshi kuja kutest mitambo akajikuta amekula vichwa 20
Kiuhalisia mji ni Dare es salaam tuu, Kwa hapa Tanzania , miji mingine utasota Sana mpak network ya maisha ije isome shidaaa, miji mingine ukitoboa watu wote wanakufahamu unakuwa monitored vibaya sana, Dsm watu ni wengi hata ukitoboa huwez julikana kama umetoboa , usinitch mdogo , DSM mzunguko wa Pesa ni mkubwa sana ni wewe Tu kuongeza speed, miji mingine ina changamoto ya ukabila asikudanganye mtu, ila kama kazi yako ya kujifungia chumban tuu , nenda Moshi
 
Back
Top Bottom