Naomba kujuzwa Mkoa na Wilaya Bora ya kuishi kwa utulivu na kuwa na maendeleo

May 24, 2015
9
3
Mkoa gani ambao mtu anaweza kuishi ikiwa anajishughulisha na shughuli za mtandaoni na kuhitaji utulivu na gharama ndogo ya maisha maana kuna kupata pesa nyingi halafu ukajikuta yote inatumika kwa mahitaji ya kila siku kwani hapa nilipo (Dar) ni kama gharama ya maisha kila siku ni kubwa pesa nyingi inatumika.

So unaweza kuwa na uzoefu na mkoa gani ambao kwa mtu wa online business akaweza kuishi.

Mkoa wenye internet ya kasi especially TTCL na Tigo

Huduma za kibenk equity na rate ya exchange ya dollar iwe nafuu kidogo.

Shughuli zangu hazitegemei watu zaidi walionizunguka

Pia uhakika wa umeme.

Pia utulivu na uwezekano wa mtu kuwekeza na maana maisha yanabadilika unachotegemea leo kinaweza kukwama.

Gharama ya maisha (upatikanaji wa chakula kwa bei rahisi)
 
Umeongea vema sana, kuna maisha fulani unapata pesa nyingi lakini zote zinaishia kwenye mahitaji ya kila siku.... na hapo wala hufurahii maisha bali ni struggles tu.

Ila hapo kwenye ‘exchange rates’ kumbe zipo tofauti mkoa kwa mkoa..?
 
Exchange rate inakuwaje tofauti kila mkoa.
Yote uliyosema utayapata Moshi kama huendi kuwekeza. Kama unaenda kuwekeza ile sio sehemu sahihi ya wewe kuishi. Pia kipindi cha mvua inaboa sana kunakuwa na tope na mvua za ovyo tu.
Arusha sijawahi ikubali kwa kuishi labda kutembelea kwa siku chache.
Muhimu hakuna jamii ya kipuuzi, kuna wilaya nyingine ukipita tu unaona maisha ya ajabu lakini Moshi hakuna ujingaujinga.
Kama kazi zako ni za indoor kule kuna maisha.
 
Mkoa gani ambao mtu anaweza kuishi ikiwa anajishughulisha na shughuli za mtandaoni na kuhitaji utulivu na gharama ndogo ya maisha maana kuna kupata pesa nyingi halafu ukajikuta yote inatumika kwa mahitaji ya kila siku kwani hapa nilipo (Dar) ni kama gharama ya maisha kila siku ni kubwa pesa nyingi inatumika.

So unaweza kuwa na uzoefu na mkoa gani ambao kwa mtu wa online business akaweza kuishi.

Mkoa wenye internet ya kasi especially TTCL na Tigo

Huduma za kibenk equity na rate ya exchange ya dollar iwe nafuu kidogo.

Shughuli zangu hazitegemei watu zaidi walionizunguka

Pia uhakika wa umeme.

Pia utulivu na uwezekano wa mtu kuwekeza na maana maisha yanabadilika unachotegemea leo kinaweza kukwama.

Gharama ya maisha (upatikanaji wa chakula kwa bei rahisi)
Wilaya zote ziko tulivu na zina mabenki.
 
Back
Top Bottom