Naomba kujuzwa mahitajio (gharama) za kufungua simple music studio

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,042
21,517
Salam wakuu,

Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza hapo juu. Kuna mahala hapa mjini Dodoma nilienda , katika kupiga story mbili tatu na wana kijiweni, jamaa wakawa wanalalamika kwamba mkoa wa dodoma una uhaba wa studio na hiko kitaa chao madogo kibao tu wanapenda muziki na wana ndoto za kurekodi nyimbo lakini changamoto ni studio. Unakuta studio kubwa pengine iko mjini na mainly ina base na kurekodi muziki wa injili.

Sasa napenda kufahamu wakuu, kwa simple studio, ni PC yenye requirements gani (sound card, video card etc) ina hitajika? Je, gharama za mixer (sijui wanaita sound card), microphone na vifaa vinginevyo. Kuhusu apps sina wasiwasi najua ma cubase, FL, vocoder etc.

Zinapatikana kirahisi tu kwenye torrents. Frame imeshapatikana, kingine naulizia jinsi ya kufanya chumba cha kuingizia vocal kua soundproof.

Nilishawahi kusikia kwamba unaweza ukafunga tray za mayai kuzuia kelele kama huna uwezo wa kumudu gharama za soundproof glasses.

Hivyo naomba muongozo wakuu, je kwa budget ya 1M unaweza ukafanikiwa kufungua studio complete ambayo ni simple (bila keyboard etc) ambayo ukaweza kugonga midundo na kuingiza vocals na kufanya mixing ? Natanguliza shukrani za dhati!
 
Nadhani kwenye vocals ndipo unahitaji sana kuzuia mwangwi, ila nilichogundua vocal za kwenye nyimbo uchafu wake mwingi unafunikwa na beats na effects. Mimi nina studio ya voice over na dubbing, coz mostly zinakuwa kavu kavu na raw, lazima zisiwe na uchafu wa aina yoyote otherwise zinakuwa rejected.

Nilinunua mic ya akg na soundcard ya behringer vyote kwa 610,000. Pc nilikuwa nayo. Treatment nlinunua zile foams kwa jamaa flan akikuwa nazo tu anauza nilinunua kwa 110000, jamaa aliyekuja zibandika na kunisetia nilimpa 80000. Ila bado naendelea kuiset na kununua vifaa
 
Mic 350,000/=
POPFILTER 50,000/=
Stend ya mic 50,000/=
SOUND CARD 500,000/=
MiD keyboard 500,000/=
Monitor speakers 800,000/=
Computer core i4, ram Gb4 800,000/=
Cables 50,000/=
=3100,000 /=
Hapo bado chumba, room treatment, na music equipments
 
Kuna dogo yupo Mwanza anauza vifaa vyake vya muziki.

PC alikuwa nayo HP core I 7 bt aliniuzia PC akabak na vifaa vingine.

Kama utahitaji unaweza kumchek fb Kwa jina Samjunior
 
Nadhani kwenye vocals ndipo unahitaji sana kuzuia mwangwi, ila nilichogundua vocal za kwenye nyimbo uchafu wake mwingi unafunikwa na beats na effects. Mimi nina studio ya voice over na dubbing, coz mostly zinakuwa kavu kavu na raw, lazima zisiwe na uchafu wa aina yoyote otherwise zinakuwa rejected.

Nilinunua mic ya akg na soundcard ya behringer vyote kwa 610,000. Pc nilikuwa nayo. Treatment nlinunua zile foams kwa jamaa flan akikuwa nazo tu anauza nilinunua kwa 110000, jamaa aliyekuja zibandika na kunisetia nilimpa 80000. Ila bado naendelea kuiset na kununua vifaa
Mkuu mambo vip? Asee unapatikana wapi? Ninampango wa kufanya issue za Dubbing. Please check me out 0756981717
 
Mic 350,000/=
POPFILTER 50,000/=
Stend ya mic 50,000/=
SOUND CARD 500,000/=
MiD keyboard 500,000/=
Monitor speakers 800,000/=
Computer core i4, ram Gb4 800,000/=
Cables 50,000/=
=3100,000 /=
Hapo bado chumba, room treatment, na music equipments
Eneo nililopo nmeona muamko la vijana wengi kuimba imba na wengine kwenda maeneo ya mbali kutafuta studio ya kufanya recording sasa nataka kufungua simple studio na kuwarecodia kwa bei ya kawaida ila kuwavuta wengi ila naomba wenye uzoefu wanipe changamoto ya uwekezaji huu kwa hali ya sasa kuwekeza studio mjini naona hatari coz competition n kubwa sana
 
Mic 350,000/=
POPFILTER 50,000/=
Stend ya mic 50,000/=
SOUND CARD 500,000/=
MiD keyboard 500,000/=
Monitor speakers 800,000/=
Computer core i4, ram Gb4 800,000/=
Cables 50,000/=
=3100,000 /=
Hapo bado chumba, room treatment, na music equipments
PC ya 4GB ram ni ndogo
Mimi ni I7 ya 16GB ram bado naona slow
Kwa 800,000 bado unaweza pata I7 ya 8-16GB ram. HDD ya 1TB
 
Back
Top Bottom