Naomba kujuzwa, maamuzi yapi sahihi nikikutana na hali hii barabarani?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,262
1,220
Naomba kujuzwa: kuna Kivuko (Zebra) na taa za kuongoza magari. Je, Ikiwaka taa ya kijani, NISIVUKE, NIWASUBIRI WATU WAVUKE? AU WAO WANISUBIRI MIMI?

Niwapo barabarani huwa Najiuliza Sana juu ya hili, mwenye ujuzi WA uhakika, ANISAIDIE.
 
kwa mujibu wa shule ya udereva...alama yoyote ya barabarani inamuwakilisha askari haswa wa kitengo cha usalama wa barabarani...hivyo kitendo cha kuwa na taa za kuongozea barabara hakukupi haki ya moja kwa moja ya kuvuka kwa kufuata taa ya kijani...rejea udereva wa kujihami...!

Hivyo kulingana na utafiti utakao ufanya eneo la tukio...maana watumiaji wa barabara wako wengi na kila mmoja anayo namna ya kipekee ya jinsi anavyoona inafaa kutumia barabara.

Hivyo taa ikiwaka na wewe kama dereva makini ukiona ni salama kuvuka pita...ila ukiona kuna kizuizi kutokana na watumiaji wengine wa barabara subiri kizuizi kipite...

kosa moja barabarani linaweza kuyagharimu maisha yako....

kuwa muangarifu ajali zinaua
 
Kwa bongo, watu wengi hawajui sheria za barabarani, mara nying ni kutumia akili zako tu, kuna maeneo hawajui kuna taa wala nn wao wanavuka tu..endesha taratibu tu unapita
 
Mzee swali lako ni Zuri sana...siku zote kama dereva unatakiwa kuwa makin sana...ikiwaka taa ya kijana unapaswa kuondoka ila kwa Tahadhari kubwa sana....mtembea kwa miguu kama kaingia road unapaswa kutulia kwa jinsi yoyote mpaka Amalize kuvuka barabara,

Mfano, hapa nilipo, hakna kitu kinachoheshimiwa road kama mtembea kwa miguu ,Gari za shule, ambulance, fire na police,fanya vyovyote ila kaa mbali na hao wahusika....
 
Waenda kwa miguu wamepewa kipaumbele zaidi kwenye kuvuka barabara hata kama taa haijawaruhusu.

Taa ya kijani inakuruhusu dereva ila tu kama ni salama.

Kwa mfano kama taa ya kijani imekuruhusu wakati huohuo kuna waenda kwa miguu wanavuka, unapaswa kusubiri mpaka wamalize kuvuka.
 
kwa mujibu wa shule ya udereva...alama yoyote ya barabarani inamuwakilisha askari haswa wa kitengo cha usalama wa barabarani...hivyo kitendo cha kuwa na taa za kuongozea...
Umemaliza kila kitu! Sio unagonga mtembea kwa miguu eti kwa vile taa ya kijani imewaka.
 
Na kwa wale watembea kwa miguu wenzangu napenda kuwakumbusha kuwa makini wakati wote pale wanapotaka kuvuka barabara hata pale kwenye alama ya zebra kwani chombo cha moto ni chombo cha moto wakati wowote kinaweza kupata hitilafu ukajikuta unapoteza maisha yako au kujeruhiwa pia kumpa matatizo dereva bila kutarajia.
 
Naomba kujuzwa: kuna Kivuko (Zebra) na taa za kuongoza magari. Je, Ikiwaka taa ya kijani, NISIVUKE, NIWASUBIRI WATU WAVUKE? AU WAO WANISUBIRI MIMI?

Niwapo barabarani huwa Najiuliza Sana juu ya hili, mwenye ujuzi WA uhakika, ANISAIDIE.
Wewe unadhani ni kipi bora, kuwasubiria wapite kwanza au kuwagionga kisa taa zimeruhusu? Katika mazingira yoyote yale tatanishi bararbani, mtembea kwa miguu ana priority, anafuata mwenye basikeli halafu mwisho mwenye gari
 
Back
Top Bottom