Naomba kujuzwa,kuku 100 wa kisasa wa mayai wanagharimu kiasi gani kufugwa mpaka wanapo anza kutaga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kujuzwa,kuku 100 wa kisasa wa mayai wanagharimu kiasi gani kufugwa mpaka wanapo anza kutaga

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ipyax, Oct 29, 2012.

 1. ipyax

  ipyax JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,194
  Likes Received: 975
  Trophy Points: 280
  Nataka kuji ingiza katika hii kazi lakini bado nafanya utafiti,kama mtu ana idea ntafurahi sana aki share nami.
   
 2. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo Milion 1 tosha kabisa
   
 3. N

  Nguto JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 280
  Nadhani uwe na milioni 2 angalau. Vifaranga tu 220,000 au 230,000.
   
 4. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  kununua kuku 100x3500 = 350,000
  banda weka LA mbao 600,000 kama upo arusha na moshi.
  madawa ni pesa kidogo kama elfu 50.
  chakula miifuko 2 mwezi wa 1 2x40,000= 80000
  mifuko 3 wapili = 120,000
  mifuko 4 wa tatu 160,000
  mifuko 5 wa nne 200,000
  nifuko 6 - 7 wa tano na kuendelea 240,000
  kuku mzima anayetaga anakula gram 120 kwa siku
  umeme ni kama wati mia ivi weka elfu 12 kila mwezi 12x5 =60,000
  usafirishaji wa chakula, plus blablaaaa
  Jumla 1,860,000 aliyesema mil2 yuko sahihi kabisa...
  then you need to have a source of income 310,000/= kwa ajili ya iyo shughulu. i ni wastani wa pesa unayohitaji kuipata kila mwezi kwa ajili ya mradi huo. ukienda taasisi za mikopo laini kama finca utaipata. kama unayo anza mara moja kwa sababu faida ikianza kutaga ni kati ya sh 1500 had 2000 kwa tray.
  sasa kuku mia watataga try 3 kwa siku then kwa mwezi ni tray 90 faida ni kama laki na elf35 ivi kwa mwezi kwa miezi 12 ya kutaga ni 1,620,000 plus kuku utawauza wakishaacha kutaga kwa let say 500,000 pesa yako imerudi. then round ya pili ndio utakula bata tu.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  uchambuzi wako makini sana hata mie nimefaidika.....
   
 6. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  asante mkuu utakuwa umesaidia wengi
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu ANKOJEI . Vipi kwa maeneo ambayo hakuna umeme, biashara hii inawezekana?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Mkuu hongera inaonekana una uzoefu mzuri na biashara hii maana umedadavua vizuri. Lakini kwasababu conditions za biashara hii sio fixed nami ngoja niongeze kidogo ninachokifahamu. Kwa upande wa production, tray 3 kwa siku maana yake ni mayai 90. Hii ni production ya 90% kwa siku (yaani kuku 90 kati ya mia wametaga). Wakati mwingine unaweza usifike huko kutegemea na namna ulivyowatunza kuku wako kwa aina ya chakula, ufuatiliaji wa ratiba ya chanjo na dawa na umakini katika kugundua magonjwa. Wataalam wanasema katika mazingira duni ya ufugaji kiwango cha juu cha production kinaweza kuwa 80% hadi 85% (yaani mayai 80 hadi 85 kwa siku). vile vile, ni kwa muda gani utaendelea kupata mayai, inategemea na aina ya kuku (breed). Breed nzuri inataga kwa kiwango cha 85% kwa wiki hadi ya 60 (yaani miezi 15) na baada ya hapo kiwango cha kutaga huanza kushuka taratibu (haimaanishi hawatagi, no! wanataga ila kiwango ndo kinashuka jinsi muda unavyozidi kwenda. Ikifika wakati production imekuwa ndogo kuliko gharama za kuwahudumia unaweza ukaamua kuwauza na kukuudishia mtaji. Idadi ya miezi ya kuendelea kupata mayai pia inategemea jinsi ulivyowatunza kuku wako. Ukiwa uliwatunza vizuri kiwango cha kutaga kinaweza kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu mara pengine hata zaidi ya miezi 18.
  Kwa hesabu ya haraka haraka ya kujua mapato na faida ni kuwa gharama za moja kwa moja (direct cost) kwa wastani ni asilimia 40 ya mapato. Unaweza ukakadiria gharama ambazo sio za moja kwa moja (indirect cost) kati ya 8% na 10% na kinachobaki ni faida. Kwa kiwango cha chini faida ni kama 50% ya mapato.
   
 9. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono uchambuzi wako wa kina
   
 10. l

  lasix JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Uko juu,thanx.nilihitaji sana ushauri wa namna hii.
   
 11. b

  ben van mike JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 471
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 33
  kweli jf kila kitu ...
   
 12. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Naipenda JF...
   
 13. p

  pachanya JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 1,031
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Naona wadau wametoa ufafanuzi mzuri hapo juu.ila kwa kuweka sawa bei ya kifaranga cha mayai ni 2300 kwa sasa (interchick).Na kwa kwa hesabu ya haraka kila kifaranga hutumia wastani wa 12,000 mpaka aanze kutaga(kuanzia mwezi wa 5).
   
 14. ipyax

  ipyax JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,194
  Likes Received: 975
  Trophy Points: 280
  Asanteni sana kwa mchango mkubwa wa mawazo,mie nipo mbeya kuna vifaranga vinatoka malawi ambavyo inasemekana ni breed bora kabisa coz huwa havipati magonjwa kirahisi.
   
 15. ANKOJEI

  ANKOJEI JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  iyo hesabu ilikuwa ya arusha dar bei zinaweza kuwa chini hata faida inaweza kuwa juu kidogo
   
 16. p

  pachanya JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 1,031
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Mkuu kuhusu aina ya kampuni unayonunulia vifaranga isikupe shida,iwe wa malawi,kenchick,interchick cha msingi ni kufuata kanuni bora za ufugaji.Pia ingekuwa vizuri ukajua gharama pia hutegemeana na mahali ulipo(gharama za chakula,dawa,bei ya mayai hutofautiana).Kuhusu suala la umeme ni kweli unaweza ukafuga kuku wa mayai sehemu isiyo na umeme na wakakua vizuri tu.Kama una swali lingine unaweza uliza.
   
Loading...