Naomba kujuzwa kuhusu Ukraine na Maluteni Kanali

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Wakuu salamu,Nina maswali mawili naomba kuuliza.

Swali la Kwanza

Nchi ya Ukraine ina kitu gani special sana hadi kupelekea kugombewa na mataifa nyenye nguvu duniani yaani marekani na urusi?

Marekani anataka kumiliki hilo eneo,mrusi nae anataka kulimikili,je ni sababu za kijasusi,kiuchumi au nini

Swali la Pili

Nchi mbalimbali barani Africa zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi kama Mali, Burkina Faso nk

Kwa mfano,kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini mali anacheo cha Luteni Kanali.Na kwa uelewa wangu ni kuwa jeshini cheo cha juu kabisa ukiacha CDF ni General.

Sasa swali langu ni hili,hawa maluteni wanapata wapi nguvu ya kupindua serikali na kuliongoza jeshi kufanya mapinduzi wakati wao sio majenerali?

Nilidhani majenerali ndio viongozi wa juu kabisa jeshini wenye uwezo wa ku mobilize jeshi kufanya tukio fulani kulingana na vyeo vyao,lakini hawa makanali wanapata wapi huu ujasiri,nguvu, ushawishi na uungwaji mkono na wanajeshi wengine?

ASANTENI KWA MAJIBU YENU

Picha 1:Luteni Kanali Paul-Henri Damiba kiongozi wa mapinduzi nchini Burkina Faso

Picha 2: Kanali Malick Diaw kiongozi wa mapinduzi nchini MaliView attachment 2103988View attachment 2103989

geoff_lea-20220126-0001.jpg
 
Wakuu salamu,Nina maswali mawili naomba kuuliza.

Swali la Kwanza

Nchi ya Ukraine ina kitu gani special sana hadi kupelekea kugombewa na mataifa nyenye nguvu duniani yaani marekani na urusi?

Marekani anataka kumiliki hilo eneo,mrusi nae anataka kulimikili,je ni sababu za kijasusi,kiuchumi au nini?

Swali la Pili

Nchi mbalimbali barani Africa zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi kama Mali, Burkina Faso nk

Kwa mfano,kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini mali anacheo cha Luteni Kanali.Na kwa uelewa wangu ni kuwa jeshini cheo cha juu kabisa ukiacha CDF ni General.

Sasa swali langu ni hili,hawa maluteni wanapata wapi nguvu ya kupindua serikali na kuliongoza jeshi kufanya mapinduzi wakati wao sio majenerali?

Nilidhani majenerali ndio viongozi wa juu kabisa jeshini wenye uwezo wa ku mobilize jeshi kufanya tukio fulani kulingana na vyeo vyao,lakini hawa makanali wanapata wapi huu ujasiri,nguvu, ushawishi na uungwaji mkono na wanajeshi wengine?

Picha ya kwanza ni Luteni Kanali Paul-Henri Damiba, kiongozi wa mapinduzi nchini Burkina Faso.

Picha ya pili ni Kanali Malick Diaw kiongozi wa mapinduzi nchini Mali.

Da Vinci XV
zitto junior
Infantry Soldier
Habibu B. Anga

ASANTE KWA MAJIBU YENU
images%20(14).jpg
Screenshot_2022-02-01_145736.jpg
 
ukraine sio kwamba inagombewa na mataifa yenye nguvu, ukraine inapakana na urusi huku ikiwa inataka kujiunga na NATO hivyo russia inaona kama ni hatari kwa usalama wao hawataki Ukraine ijiunge na NATO ndio maana wanataka hakikisho kutoka NATO kwamba hawatoruhusu ukraine ajiunge na nato ! Na kama ukraine bdo anataka kujiunga na nato licha ya matakwa ya russsia basi njia iliyobaki ni kumvamia ambacho ndo kitu urusi anataka kufanya kama njia nyingine zikishindikana

kuhusu mapinduzi ni kwamba yeyote yule jeshini anaweza pindua serikali/kufanya mapinduzi hata awe ni private tu, cha msingi ni mtu awe na ushawishi mkubwa kwa wanajeshi wenzake na ushawishi haujalishi rank ya ofisa ! askari yeyote yule mwenye cheo chochote kile anaweza kuhamasisha mapinduzi na akaungwa mkono na wenzake walio wengi bila kujali vyeo vyao sio lazima makanali hivyo akaongoza mapinduzi! ndio maana jeshini kuna maafisa wa inteijensia na maafisa wa siasa lengo ikiwa ni kukusanya taarifa ndani ya vikosi vya askari na kuwashiwishi kufikia malengo au kuwatia morali askari
 
ushamaliza
 
Big up
 
Nitajibu swali la kwanza!

Ukraine kijiografia ni nchi iliyo katikati ya mataifa ama pande mbili zenye uhasama, yaani Urusi upande mmoja, na Marekani kupitia NATO upande mwingine.

Upande wowote kati ya pande mbili hizo utakaofanikiwa kulipata ama kuliweka katika ushawishi wake eneo hilo kwa namna yeyote ile ikiwemo kivita, kidiplomasia n.k. utakuwa na nafasi nzuri ya kulitumia eneo hilo hasa kijeshi, kama upande huo utataka kufanya hivyo, dhidi ya upande wa pili. Ndio maana kuna mgogoro kuhusu Ukraine kati ya Urusi na Marekani (NATO).

Pia, Ukraine imekuwa ikitajwa kama "buffer state" na baadhi ya wachambuzi ikiwa na maana ya kwamba ni taifa huru lililopo katikati ya mataifa ama pande mbili zinazohasimiana, linalopaswa kuwa na sera za kimataifa ambazo hazifungamani na upande wowote ule (neutral) ili kuepusha migogoro kati ya pande hizo.

Hata hivyo, migogoro mingine huwa haikwepeki kwa sababu nchi yoyote inaweza kuwa na sera zake binafsi kwa vile ni nchi huru. Hili linajidhihirisha kwa Ukraine ambayo mara kadhaa imekuwa na sera zinazofungamana na nchi za magharibi likiwemo suala la kutaka kujiunga na NATO kitu ambacho Urusi inakiona kuwa ni tishio kwa usalama wake.
 
Hata hivyo, migogoro mingine huwa haikwepeki kwa sababu nchi yoyote inaweza kuwa na sera zake binafsi kwa vile ni nchi huru. Hili linajidhihirisha kwa Ukraine ambayo mara kadhaa imekuwa na sera zinazofungamana na nchi za magharibi likiwemo suala la kutaka kujiunga na NATO kitu ambacho Urusi inakiona kuwa ni tishio la usalama wake.
Kwa kuongezea tu, hata Ukraine kwa nguvu za kivita siyo nchi ya mchezo,, wanaunda makombora manowari na ndege za kijeshi,
Kiufupi USSR isingemeguka lilikua dubwana moja la kutisha sana kijeshi,,
Lakini licha ya ukraine kuwa na jeshi kubwana lenye nguvu ,, hawezi kubattle na Russia,,, lazima atakaa tu
 
shida nyingine ya ukraine haina airforce ya kuimudu urusi pia maafisa wenge wa jeshi la ukraine ni mamluki wa urusi
 
Ninajibu hili la ma-Luteni kanali:

Hivi vyeo imekuwa kama ni zali tu kwao msimu huu, lakini si vyeo maalumu vya kufanyia hayo maasi.

Cheo cha Lt col kimuundo, kinaongoza wanajeshi takribani1000, wa vyeo vya meja kushuka chini hadi private, kwa hiyo wanajichanganya na wanajeshi wa vyeo vya chini katika maisha yao ya kila siku kiurahisi zaidi kuliko majenerali ambao kuonana na wanajeshi wa chini mpaka wafanye mikutano.

Katika historia, mapinduzi ya kijeshi yamewahi kufanywa na wanajeshi wa vyeo mbali mbali jeshini wakiwemo mpaka wa vyeo vya chini kabisa kama kmf: capt Thomas Sankara wa Burkina Faso, Flt Rawlings wa ghana, Msgt Doe wa Liberia miaka ya '80 na Jenerali aliyewahi kupindua serikali ni Idd Amin wa Uganda na wengineo ambao siwezi kuwataja kwa sasa.

Ieleweke kuwa, jambo la kupindua serikali iliyopo madarakani ni kosa la uhaini na adhabu yake karibia mataifa mengi huwa ni kifo.

Kikubwa kinachowawezesha kufanikisha mapinduzi hayo ni mkakati madhubuti wa kupanga njama na kisha kuzitekeleza kwa kuvikwepa vyombo vya usalama vya jeshi visiweze kuvujisha siri kwa wakubwa, hilo la kwanza, la pili ni kupima upepo wa morali ya wanajeshi kwa serikali iliyopo madarakani, je ipo juu ama ipo chini?

Hao majenerali kula njama za kupindua serikali si rahisi sana wao kufikiria hayo, hasa kutokana na maslahi binafsi wanayopewa na Taifa.

Hivyo basi kwa mtu anayependelewa na taifa ki maslahi, ni ngumu sana kuisaliti serikali hiyo hiyo inayomlea, maana mipango hiyo ikivurugika, misukosuko inayowapata watuhuhumiwa huwa si ya kitoto.

Majenerali ni wazee wenye maadili na ni watiifu mno kwa serikali, ni watu wanaotarajia kustaafu kwenda kupumzika, si rahisi wao kujiingiza kwenye njama ambazo zikiharibika zitawaharibia maisha yao na stahiki zao zote .

Mambo hayo hufanywa na vijana damu changa wanaopenda mabadiliko wasiojali lolote mbele yao.
 
Nitajibu swali la kwanza!

Ukraine kijiografia ni nchi iliyo katikati ya mataifa ama pande mbili zenye uhasama, yaani Urusi upande mmoja, na Marekani kupitia NATO upande mwingine.

Upande wowote kati ya pande mbili hizo utakaofanikiwa kulipata ama kuliweka katika ushawishi wake eneo hilo kwa namna yeyote ile ikiwemo kivita, kidiplomasia n.k. utakuwa na nafasi nzuri ya kulitumia eneo hilo hasa kijeshi, kama upande huo utataka kufanya hivyo, dhidi ya upande wa pili. Ndio maana kuna mgogoro kuhusu Ukraine kati ya Urusi na Marekani (NATO).

Pia, Ukraine imekuwa ikitajwa kama "buffer state" na baadhi ya wachambuzi ikiwa na maana ya kwamba ni taifa huru lililopo katikati ya mataifa ama pande mbili zinazohasimiana, linalopaswa kuwa na sera za kimataifa ambazo hazifungamani na upande wowote ule (neutral) ili kuepusha migogoro kati ya pande hizo.

Hata hivyo, migogoro mingine huwa haikwepeki kwa sababu nchi yoyote inaweza kuwa na sera zake binafsi kwa vile ni nchi huru. Hili linajidhihirisha kwa Ukraine ambayo mara kadhaa imekuwa na sera zinazofungamana na nchi za magharibi likiwemo suala la kutaka kujiunga na NATO kitu ambacho Urusi inakiona kuwa ni tishio kwa usalama wake.
Pamoja sana
 
Ukrain ilikuwa ni sehemu ya Urusi kabla ya 1990. Ukraine na Russia ni ndugu kabisa. Sema kiherehere cha marekani kuingilia mambo ya nchi nyingine. Huo ugomvi wao ni kelele zaidi kuliko vitendo. Japo wanachimbana beat.
 
Ninajibu hili la ma-Luteni kanali:

Hivi vyeo imekuwa kama ni zali tu kwao msimu huu, lakini si vyeo maalumu vya kufanyia hayo maasi.

Cheo cha Lt col kimuundo, kinaongoza wanajeshi takribani1000, wa vyeo vya meja kushuka chini hadi private, kwa hiyo wanajichanganya na wanajeshi wa vyeo vya chini katika maisha yao ya kila siku kiurahisi zaidi kuliko majenerali ambao kuonana na wanajeshi wa chini mpaka wafanye mikutano.

Katika historia, mapinduzi ya kijeshi yamewahi kufanywa na wanajeshi wa vyeo mbali mbali jeshini wakiwemo mpaka wa vyeo vya chini kabisa kama kmf: capt Thomas Sankara wa Burkina Faso, Flt Rawlings wa ghana, Msgt Doe wa Liberia miaka ya '80 na Jenerali aliyewahi kupindua serikali ni Idd Amin wa Uganda na wengineo ambao siwezi kuwataja kwa sasa.

Ieleweke kuwa, jambo la kupindua serikali iliyopo madarakani ni kosa la uhaini na adhabu yake karibia mataifa mengi huwa ni kifo.

Kikubwa kinachowawezesha kufanikisha mapinduzi hayo ni mkakati madhubuti wa kupanga njama na kisha kuzitekeleza kwa kuvikwepa vyombo vya usalama vya jeshi visiweze kuvujisha siri kwa wakubwa, hilo la kwanza, la pili ni kupima upepo wa morali ya wanajeshi kwa serikali iliyopo madarakani, je ipo juu ama ipo chini?

Hao majenerali kula njama za kupindua serikali si rahisi sana wao kufikiria hayo, hasa kutokana na maslahi binafsi wanayopewa na Taifa.

Hivyo basi kwa mtu anayependelewa na taifa ki maslahi, ni ngumu sana kuisaliti serikali hiyo hiyo inayomlea, maana mipango hiyo ikivurugika, misukosuko inayowapata watuhuhumiwa huwa si ya kitoto.

Majenerali ni wazee wenye maadili na ni watiifu mno kwa serikali, ni watu wanaotarajia kustaafu kwenda kupumzika, si rahisi wao kujiingiza kwenye njama ambazo zikiharibika zitawaharibia maisha yao na stahiki zao zote .

Mambo hayo hufanywa na vijana damu changa wanaopenda mabadiliko wasiojali lolote mbele yao.
Shukrani sana
 
Kuhusu Mapinduzi elewa kwamba mapinduzi ya kijeshi yanafanikiwa sana katika nchi ambazo ni "failed states" na serikali ikishajiandaa wanajeshi hawawezi kufanya mapinduzi na na na"back" hoja hii kwa ku"cite" Coup zilizowaingiza madarakani Meja jenerali Babangida kule Nigeria na Jenerali Abacha huko huko Nigeria kuhusu hao majenerali wawili inasemwa kwamba mipango ya Coup zao ilishajulikana mapema sana na taarifa kupelekwa kwa wakuu wa nchi mfano kuingia kwa Abacha ni Babangida aliamua amuachie tu Abacha kuingia madarakani
 
ukraine sio kwamba inagombewa na mataifa yenye nguvu, ukraine inapakana na urusi huku ikiwa inataka kujiunga na NATO hivyo russia inaona kama ni hatari kwa usalama wao hawataki Ukraine ijiunge na NATO ndio maana wanataka hakikisho kutoka NATO kwamba hawatoruhusu ukraine ajiunge na nato ! Na kama ukraine bdo anataka kujiunga na nato licha ya matakwa ya russsia basi njia iliyobaki ni kumvamia ambacho ndo kitu urusi anataka kufanya kama njia nyingine zikishindikana

kuhusu mapinduzi ni kwamba yeyote yule jeshini anaweza pindua serikali/kufanya mapinduzi hata awe ni private tu, cha msingi ni mtu awe na ushawishi mkubwa kwa wanajeshi wenzake na ushawishi haujalishi rank ya ofisa ! askari yeyote yule mwenye cheo chochote kile anaweza kuhamasisha mapinduzi na akaungwa mkono na wenzake walio wengi bila kujali vyeo vyao sio lazima makanali hivyo akaongoza mapinduzi! ndio maana jeshini kuna maafisa wa inteijensia na maafisa wa siasa lengo ikiwa ni kukusanya taarifa ndani ya vikosi vya askari na kuwashiwishi kufikia malengo au kuwatia morali askari
Ni kweli kabisa Russia wameingiwa na uoga wa kumezwa na NATO,manaaake mpaka sasa kuna nchi kama nne hivi tayari ni wanachama wa NATO na wapakana nao.
 
Back
Top Bottom