Naomba kujuzwa kuhusu kupalilia Mahindi kwa kutumia viuatilifu

Asante kwa ushauri wako. Je, hii MERAXONE inafaa kwenye ufuta? Pia napenda kujua utatumia utaalam/ujanja gani dawa isipate mimea ya mazao na kuidhuru?!
Ikinyesha mvua kubwa baada ya kupanda mahindi, unapiga dawa inaitwa MAGUGUMA. Maguguma.

Maguguma huzuia mbegu za palizi zisiote kwa mwezi mmoja hivyo wakati ikianza kuota tayari mahindi yatakuwa na zaidi ya cm 60. Palizi ikiota wakati huo nyunyizia dawa ya magugu inayojulikana kama 2'4- D.

2,4-D hii huua majani yenye asili ya majani mapana na hukausha kabisa na kufanya mahindi yakue mpaka kufikia hatua ya kuchanua na kubeba huku palizi inayokuwepo ni ile yenye asili moja na mahindi(majani membamba). Baada ya mahindi kubeba nyunyizi dawa MERAXONE.

MERAXONE huua majani ya aina zote hivyo wakati wa kunyinyizia bomba liwe chini ili kutokuunguza mahindi upande Wa juu kwenye majani. Ukipiga dawa hii majani yote yatakayoguswa na dawa yataungua na kufanya shamba kuwa huru mpaka wakati Wa kuvuna.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rukwa nadhani branch ya mufindi itakuwa karibu na wewe. Safi sana umeamua kufuatilia hizi mashine kwa undani. Usikose kutembelea maonesho yajayo ya 88 mbeya, moro au Arusha kuna mashine nyingi sana na bei zake ni za kawaida sana tofauti wengi wanavyofikiri. Ukiwa na hii mashine unaajiri mtu mmoja tu na kumpa mafuta badala ya kumlipa elfu 40 kwa acre unamlipa 10 tu, unajikuta Kama una shamba acre 30 ndani ya miezi 3 mashine imeshajinunua

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mbeya branch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi za kufyeka nafikirinzinafyeka nyasi za viwanja tu. Zinaweza kufyeka eneo ambalo halijalimwa miaka mingi kwa ajili ya kupalima??
Ya kwanza ni kupalilia/kutifua, ya pili ni kubwa kufyeka na tatu ni ndogo kufyeka. Hapo inakuja na motor 2 za kufyekea Kama unavyoziona #1 inatumia kisu (Kama feni) #2 inatumia waya. Ikiharibika spare wanazo
Hizi pia zinatumika sana kukata mpunga, za kiChina zipo na bei ni sawa na hizi Germany lkn za China ni mayai mayai sanaView attachment 1338879

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa ushauri wako. Je, hii MERAXONE inafaa kwenye ufuta? Pia napenda kujua utatumia utaalam/ujanja gani dawa isipate mimea ya mazao na kuidhuru?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Ufuta labda uwe uwe kwenye hatua ya kutengeneza matunda kisha upige kwa chini sana na kwa umakini sana.

Ukikosea tu utaunguza kila kitu, kwa ufuta hushauriwi kutumia viuagugu kwasababu upo kwenye kundi la majani mapana ambayo yanaathiriwa na dawa nyingi kuanzia 2-4D mpaka Roundup.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naomba kupata uzoefu wenu katika kilimo cha mahindi kwa wakulima hususan wenye hekal chahe,
Hivi kwa hali ya kawaida hekali moja inatakiwa kutoa gunia ngap za mahindi.

Coz mwaka juzi niliwahi kusimamia shamba la ndg angu, ambaye alilima hekali 4, kwa mbegu zile ''seedco" +mbolea ya samadi, lakin mwisho wa siku 2kapata gunia 16 hiv kamil na debe chache.

Sent using Jamii Forums mobile app
gunia 16 kwa eka 4!, pamoja na mbolea. Hiyo ni hasara kubwa sana. Tupatie ufafanuzi zaidi
1)seedco wana mbegu za aina mbalimbali tuambie jina la mbegu uliyopanda na je ulitumia vipimo sahihi vya kupandia?
2) Mbole ya samadi ulitumia ya namna gani, kuna ilikwisha oza kabisa, na kuna ambayo iko kama vumbi vumbi
3)Ulipata magonjwa gani na uliyashughulikiaje
4) Mvua zilikuwaje
Ushauri wa haraka
1) waone wataalamu wa kilimo walio katika eneo lako wakupe ushauri wa mbegu inayofaa kwenye eneo lako. Chagua mbegu zenye punje kubwa, hizo zenye punje ndogondogo hukomaa haraka na ni tamu lakini kujaza gunia ni kazi
2) Mbegu utakayonunua ina maelekezo ya namna ya kupanda - yafuate kwa ukamilifu
3)Tumia mbolea ya kupandia kama utakavyoshauriwa na wataalamu hasa DAP inafaa sehemu nyingi. Mbolea ya samadi itumike kwa uangalifu mkubwa maana unaweza kulazimika nyingi sana ili kupata virutubisho vinavyotakiwa.
 
Back
Top Bottom