Naomba kujuzwa kuhusu hili tafadhali!


K

kiparah

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2010
Messages
1,176
Likes
43
Points
0
K

kiparah

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2010
1,176 43 0
Hivi kwanini wakati timu za taifa zinapocheza mechi za kirafiki, jezi zao mgongoni hayaandikwi majina yao? Kuna sheria inazuia hilo? Maana mi soka imenipitia kushoto kidogo!
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,776
Likes
125,623
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,776 125,623 280
Hata mimi sijui, Labda hii topic ukiipeleka jukwaa la sports and entertainment utapata jibu maridhawa
 
EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
14,487
Likes
1,020
Points
280
EMT

EMT

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2010
14,487 1,020 280
Hivi kwanini wakati timu za taifa zinapocheza mechi za kirafiki, jezi zao mgongoni hayaandikwi majina yao? Kuna sheria inazuia hilo? Maana mi soka imenipitia kushoto kidogo!
Hata mimi sijui, Labda hii topic ukiipeleka jukwaa la sports and entertainment utapata jibu maridhawa
Kwa sababu taratibu za FIFA zinataka wachezaji wavae jezi zenye majina yao mgongoni pale tuu wanapocheza kwenye "Final Competitions", "Preliminary Competitions" and "Preliminary Olympic" matches. Hii ni kwa mujibu wa FIFA Equipment Regulation, Number 7 inayopatikana kwenye hii link: http://www.fifa.com/mm/document/tournament/competition/51/54/30/equipment_reg_26032010_en.pdf

Hivyo basi, kwa mechi za kirafiki ambazo siyo competitive, wachezaji wanaweza kuvaa jezi ambazo hazina majina yao mgongoni. Hata hivyo, kwenye timu zenye wachezaji ambao ni under 18, kwa kawaida haipendekezwi kuweka majina ya wachezaji kwenye jezi zao kwa sababu bado ni watoto. Hii siyo sheria bali ni ushauri kutoka kwa baadhi ya vyama vya soka ili ni kuepusha watoto hao kuwa "groomed".

Kwa kuongezea tuu, moja ya sheria za Ligi Kuu ya Uingereza inasema kuwa kila mchezaji ni lazima avae jezi inayoonyesha namba na jina lake (surnane au jina lingine baada ya kukubaliwa) mgongoni. Hivi karibuni, kulikuwa na issue moja hivi ambapo mchezaji aliyekuwa anatumia jina "Robinson" aliomba kubadilisha jina lake la mgongoni kuwa "Ravel" na kukubaliwa. Inadaiwa alibadilisha jina ili aanze maisha mapya kwenye soka.

Pia kama umeshawahi kumwoma Javier Hernández Balcázar wa Manchester United, kuna wakati anakuwa na jina "Hernández" au "Chicharito". Hata hivyo, wakati akiwa anachezea ligi kuu ya huko Mexico alikuwa anatumia jina "Chicharito" na hivyo basi alipokuja kucheza Ligi Kuu ya Uingereza alikubaliwa kutumia jina hilo japokuwa siyo "surname" yake.

Mwingine ni Kun Aguero, jina alilopewa na bibi/babu yake kwa kupenda mno kuangalia kipindi cha watoto kwenye TV kilichojulikana kwa jina hilo. Pia mchezaji ya klabu ya Fulham kwa jina Bryan Ruiz alikubaliwa kutumia jina lake la kwanza kwa sababu za kifamilia (Baba yake aliikimbia familia yao wakati yeye akiwa na umri wa mwaka mmoja tuu).

Mwingine ni Lassana Diarra aliyewahi kuchezea Chelsea, Arsenal na Portsmouth kwa kutumia jina hilo. Hata hiyo, alivyohamia Real Madrid, aliitwa "Lass" ili kutofautisha jezi yake na ile ya Mahamadou Diarra. Kuna mwingine anaitwa Christian Benitez. Hata hivyo alikubaliwa kutumia nickname yake "Chucho" kutokana na work rate yake uwanjani.

Pia Jordi Cruyff alikubaliwa kutumia jina lake la kwanza ili kumtofautisha na baba yake maarufu sana kwenye soka aliyekuwa anatumia jina "Cruyff". Yuko pia Stelios Giannakopoulos ambaye alikubaliwa kutumia jina lake la mwanzo kutokana na mashabiki wa Bolton kutopendezewa na jina lake la mwisho la Kigiriki. Lakini anapochezea timu yake ya taifa anatumia surname yake - Giannakopoulos

Inadaiwa kuwa Frabregas aliomba atumie jina "Cesc" lakini akakataliwa. Ila hilo jina hapo chini kwenye picha lilikubaliwa kutumika wakati mhusika akichezea Hull na Celtic. Kama kuna mechi inayohusisha timu za Japani halafu unaangalia mechi live na familia au watu wengine wa heshima inaweza kuwa noma.

Kwa msaada wa: Premier League first names on shirt: Ravel Morrison and others | Mail Online
 

Forum statistics

Threads 1,252,063
Members 481,989
Posts 29,794,481