Naomba kujuzwa kuhusu gari aina ya Vauxhall

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
79d7d5d5f0a8804c95ae484eb999812f.jpg

Jamani mnaojua kuhusu hili gari nijuzeni...kuna jamaa yangu anataka niuzia.
Ila kabla sijafanya nae biashara nimeona nije huku mnipe siri ya hili gari..
Je,matumizi yake ya mafuta vip?
spea zake zinapatikana kiurahisi kweli,?maana alitumiwa toka UK.
Na vip kuhusu uimara wake?

Karibuni wataalam...
 
Ukinunua Hilo litakuwa lako maisha kwa sababu spare taabu. Labda kama unauwezo wa ukiagiza na DHL na uwe na part list kwani hakuna kwenda na sample UK unaagiza na part number
 
mafuta linameza,spare zake ilala hakuna,kama mfukoni uko safi nunua tu ila kama za kuunga unga go for toyota
Mafuta sio kweli aisee! Lipo very economical. Shida ni spare parts to kibongo. Isingekuwa spare ni gari zuri sana. Nikiwa UK pande za East Greenstead ndio ilikuwa gari la host wangu so nimepanda throughout my stay
 
Kuna jamaa wanazo mbili za kubebea maiti,zile ndefu, frankly,zinawatesa mnoo,zinachemka saana yaani kila siku garage,spea wanaagiza UK direct,sikushauri.
 
Jamaa ameniambia spea zake zinaingiliana na Swift... hii ni kweli?
 
Sio kweli hili! Kama swift tu kashindwa kuingiliana na ndugu yake Chevrolet Cruise, itawezekanaje kwa Vauxhall? Labda uwe mzee wa kupiga modification kila siku, kitu ambachi kitaathiri ubora wa gari.
Kuna jamaa yangu alikuwa na Opel ikazingua akaja akafunga engine, gearbox na control Box ya Starlet. From there halikuwa gari tena! Kuondoka lazima aondokee D2, D1 haliendi hata chembe! Fuel consuption ikawa worse.
Achana na Europea Cars kama mfuko hauko vizuri na pia kama hauna subira
 
asante...
 
Kiongozi, umenigusa hapo kwenye Chevrolet Cruze na Suzuki Swift. Kimuonekano yapo kama vile yanafanana sana, nilidhani hata spare parts zake zingeingiliana, kumbe sio. Ukizingatia yametengenezwa jointly na kampuni ya Suzuki.

Je, unaijua vizuri Chevrolet Cruze? Naziona sana siku hizi lakini je, uimara, upatikanaji wa vipuri na fuel consumption ipoje? Nilipita pale ilala kufanya dodoso kidogo, jamaa mmoja akaniambia eti suzuki nisijaribu hata siku moja, sio imara na vipuri ni ghali.

Uzoefu wako tafadhali.
 
Kuna jamaa wanazo mbili za kubebea maiti,zile ndefu, frankly,zinawatesa mnoo,zinachemka saana yaani kila siku garage,spea wanaagiza UK direct,sikushauri.
Zile nazijua, za zamani sanaaaa.
 
Back
Top Bottom