Naomba kujuzwa kozi fupi VETA

Remotex

Member
Oct 3, 2020
60
104
Wadau poleni na majukumu. Naomba mnishauri.

Ninamjomba wangu (mtoto wa dada yangu) mwakani Inshalah nataka nimpeleke akasome VETA kozi fupi miezi mitatu mambo ya Uchomeleaji vyuma (Welding) Nilimtuma akafwatilie juzi wakamjibu amechelewa kujiunga mwaka huu na usaili umeshapita hadi mwakani tena, mwezi wa kumi. Nimeona asikae mtaani mpaka mwakani mwezi wa kumi kusubiri usaili alafu ajiunge mwaka 2023,kozi ndefu ni mbali sana na nikupoteza muda kukaa mtaani.

Sasa nachotaka kujua akisoma hiyo kozi miezi 3 atakuwa sawa na wale waliosoma miaka miwili? na je kama hatokuwa sawa kwanini sasa natakiwa kulipa ada mara sita zaidi ya ada ya wale wanaosoma miaka miwili? maana wale wanaosoma miaka miwili ada yao ni 60,000 tena kwa Mwaka mzima.

Nitashukuru kwa mawazo yenu naomba kuwasilisha.
 
Nina wasiwasi na ubongo wako wa kufikiri ivi mtu wa kusoma kozi miaka 2 atakuwaje sawa na mtu aliyesoma voda fasta ya miezi 3? Jaribu kufikiri mara mbilimbili mkuu.

Hiyo ni short course tu mkuu hawezi kuwa sawa na mtu aliyesoma muda mrefu
 
Nina wasiwasi na ubongo wako wa kufikiri ivi mtu wa kusoma kozi miaka 2 atakuwaje sawa na mtu aliyesoma voda fasta ya miezi 3? Jaribu kufikiri mara mbilimbili mkuu
Hiyo ni short course tu mkuu hawezi kuwa sawa na mtu aliyesoma muda mrefu
Ondoa shaka kabisa na ubongo wangu asilimia mia. Fikra zangu zimekwama hapa, kama hawawezi kuwa sawa kwanini waweke 360,000 miezi mitatu na 120,000 miaka 2? Yani kwa mantiki hiyo ya ada hiyo miezi mitatu inanondo za kutosha kuliko miaka miwili. Sasa mimi ndio naanza kwa na wasiwasi na ubongo wako ulivyo mzito kufikiri na kutoa majibu mepesi mepesi bila kushirikisha Medulla Oblongata. Cheza na number hizo mkuu alafu njoo na majibu yaliyoshiba, sio kuanza kukashifu watu uwezo wao wa kufikiri, wakati wewe ndio zero brain
 
na wajibu hapa wote msioelewa hii.
Ipo hivi unaposikia kozi ya muda mfupi maana yake watu wanadeal na mafunzo ya kozi hiyo tu. Kama ni magari utasoma magari Hadi siku ya Mwisho.
Ila kozi ya muda mrefu (FTC) hii ni mixer ya masomo zaidi ya 7 ikiwemo math na physics aliyoikimbia.

Kozi ya Muda Mfupi sasa.
*Miezi 3 ya mwanzo ni basic.
*Mi 3 inayofuata ni intermid.....
*Mi3 ya Mwisho ni Advance....
Hii yote 9 ni sawa na aliyesoma level one. Yaani kwa FTC ni mwaka mmoja.

Kama ana-kichwa chepesi atatoboa hata kwa coz fupi.
Nilishasoma Veta Ufundi Bomba kwa kozi hizi Fupi. Na mtu nikimwambia mimi nina (FTC) hawezi kubisha, Kwenye nyumba hizi za kawaida ndo napiga kama na nawa
 
Haya ndio majibu yalioshiba na yenye logic... Now it makes sense ahsante sana mkuu...
 
Wadau poleni na majukumu. Naomba mnishauri.

Ninamjomba wangu (mtoto wa dada yangu) mwakani Inshalah nataka nimpeleke akasome VETA kozi fupi miezi mitatu mambo ya Uchomeleaji vyuma (Welding) Nilimtuma akafwatilie juzi wakamjibu amechelewa kujiunga mwaka huu na usaili umeshapita hadi mwakani tena, mwezi wa kumi. Nimeona asikae mtaani mpaka mwakani mwezi wa kumi kusubiri usaili alafu ajiunge mwaka 2023,kozi ndefu ni mbali sana na nikupoteza muda kukaa mtaani.

Sasa nachotaka kujua akisoma hiyo kozi miezi 3 atakuwa sawa na wale waliosoma miaka miwili? na je kama hatokuwa sawa kwanini sasa natakiwa kulipa ada mara sita zaidi ya ada ya wale wanaosoma miaka miwili? maana wale wanaosoma miaka miwili ada yao ni 60,000 tena kwa Mwaka mzima.

Nitashukuru kwa mawazo yenu naomba kuwasilisha.
Ila muda bado upo,jaribu na vyuo vingine vya ufundi vya private napo ni vizuri tu
 
Back
Top Bottom