Ashangedere
Senior Member
- Aug 9, 2010
- 119
- 31
Huwa napata na mshangao siku hizi ninaposikia watu wakiwasema wenzao eti kisa wameamua kuachana na mke au mume, na kuwaona kama ni malaya kwa maamuzi hayo, kuna watu wanamsema kwa mfano JLO eti kwa nini amedivorce, hivi kweli jamani sisi kama great thinkers tunaona ni vema kuishi na mtu ambaye humpendi tena ambaye umejaribu kila njia kumuweka moyoni tena na umeshindwa?? je ni haki kuishi na mke/mume ambaye unajua fika anatoka na mtu mwingine nje ya ndoa, ni haki kuvumilia mtu unajua kabisa hakupendi?? sisi kama great thinkers tufike mahali tukubali maamuzi ya watu ambayo yako wazi na ndio wanachojisikia moyoni, ndio maana ndoa nyingi zimejifia siku nyingi lakini watu wanang'ang'ania kwa sababu wanaogopa jamii. kuna thread nimeona wanamtupia madongo jlo, lakini huyu dada naona ni bora kaacha kwanza ndio kaanza hayo mahusiano yake mapya, wangapi humu ndani mnacheat halafu mnajifanya wanandoa, hiyo ndio mungu anapenda?? binafsi napenda style ya JLO coz anafuata moyo wake na ndio raha ya maisha, jamani tunaishi mara moja tu, tabu ya nini?? kama hayajakukuta mshukuru mungu wako na endelea kuomba uendelee kuwa na upendo kwa umpendae nae akupende pia, je umewahi kujiuliza mwenzako akikuchukia kabisa na akataka kukuacha utafanyaje?? utakubali au utaiganda hiyo ndoa, maana huyo ni binadamu na anaweza kubadili akili saa yoyote, hata hivyo vitabu vimesema ndoa yaweza kuvunjika kwasababu ya kukosa uaminifu lakini kuna watu wameng'ang'ania tu kuvumilia huku wakisingizia kiapo walichokula, au labda tuongeze phrase kwenye kiapo cha ndoa tuseme kwenye kuchepuka pia tuvumilie...