Naomba kujuzwa juu ya Basi zuri na nauli kwenda Songea

The King of Jews

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
478
108
Wana JF ni matumain yangu mu wazima wa afya njema,

Ninatarajia kusafiri kwenda Songea ndani ya wiki ijayo. Naomba kufahamishwa juu ya BASI ZURI NA NAULI ZAKE . Pia itakuwa vizuri nikijulishwa lodges nzuri hapo mjini.

Natanguliza shukran zangu.
 
Hiyo route kuna ;

1.Super Feo, ana gari za Kichina, Yutong na Higer. Ziko vizuri...kwenye Higer unachaji na simu yako kabisa.

2. Newforce naye anagari nzuri za kichina....Zhonghtong bus.

3. Ilyana.....huyu naye anagari nzuri za kichina. Ni Higer.


zote ni nzuri. Uchaguzi ni wako.
 
Hiyo route kuna ;

1.Super Feo, ana gari za Kichina, Yutong na Higer. Ziko vizuri...kwenye Higer unachaji na simu yako kabisa.

2. Newforce naye anagari nzuri za kichina....Zhonghtong bus.

3. Ilyana.....huyu naye anagari nzuri za kichina. Ni Higer.


zote ni nzuri. Uchaguzi ni wako.

Mkuu asante sana aisee.......
 
kukwepa usumbufu nakushauri chukua superfeo hata ikitokea hitlafu njiani wanatoa msaada haraka.

ila hao ILYANA au kwa jina lingine OTA ni majanga. Ndugu yangu aliwahi kufika njombe saa 11 asubuhi siku ya pili baada ya gari lao kuharibika moro jana yake na konda kukimbia ili abiria wasimsumbue.

Ninacho wapendea superfeo wana magari mengi sana ya ziada kuanzia coaster . pia wana ruti nyingi sana kiasi na mabasi mengi kiasi kwamba abiria huweI kulala porini.

OTA au ILYANA ni wahuni sana na hawana lugha nzuri kwa wateja , mizigo wanatoza pesa wanayo taka labda kama wamebadiŕika sasa ivi .

Newforce siwajui ninacho fahamu ni kimoja tuu Mabasi yao karibia yote ni mapya.

safari njema.
 
Back
Top Bottom